Harambee! Saidia watu wa Tumbatu, unachokitoa utakikuta kwa Allah

Written by  //  04/04/2016  //  Matangazo, Habari, Misaada  //  Maoni 5

Picture4

Assalaam alaykum ndugu Wazanzibari popote pale mlipo, kama mnavyojua kwamba ndani ya wiki hii kuna vitendo vya kihalifu vimefanywa na vikosi vya SMZ na hujuma kubwa wamefanyiwa ndugu zetu wa Tumbatu, wengi wao kwa sasa hawana makaazi, wanapata hifadhi kwa jamaa zao, hili si la mmoja leo kwao kesho kwako, utakachoitoa utakikuta mbele ya Allah.

Kwa hivyo yoyote alijaaliwa anaweza kufikisha mchango wake kwa viongozi waliopewa dhamana hiyo na inshaa Allah sadaka zao zitafika, Bonyeza hapa kuwasiliana na wahusika.

Kuhusu Mtunzi

BLOGGER/DEVELOPER/JOURNALIST/BROADCASTER

View all posts by

Maoni 5 katika "Harambee! Saidia watu wa Tumbatu, unachokitoa utakikuta kwa Allah"

 1. sadimba 04/04/2016 kwa 4:12 um ·

  Hebu tumuangalie Maulidi Juma alivyozungumzia jinsi gani pesa inaweza kumgeuza mtu:

  Pesa

  Pesa ndilo pambo la uliwenguni,
  Kisha ni urembo nimeziamini,

  Na ambalo si kosa wala si la kombo,
  Dunia ya sasa sio ya kitambo
  Bila ya mapesa halinogi jambo.

  Pesa si mkanda na wala si jivu,
  Pesa ni upanga huuwa wekevu,
  Kwa pesa mjinga huitwa mwerevu.

  Zina mahadao pesa duniani,
  Hupunguza nyoyo utu na imani
  Kwa pesa nguguyo hujui ni nani.

  Pesa ni ushingo wenye sumu kali
  Hugeuza bongo kufuata muhali,
  Kwa pesa muongo huitwa mkweli.

  Zimepeka mbio pesa wengi watu,
  Wakawata kwao ikawa si kitu,
  Pesa zina cheo cha ulimwenguni.

  Pesa hukuwata hugeuza nia,
  Ukambasa nta hali waumia,
  Kwa pesa hujuta mja akalia.

  Henyi watukufu hapa ni tamati,
  Ingawa sikufu naloyatafiti,
  Pesa kuzisifu zataka wakati.

 2. bokoboko 04/04/2016 kwa 5:47 um ·

  SUALA LANGU TUNASAIDIA KUPATA MAKAAZI KUJENGA NYUMBA ZAO AU KWANZA NI MSAADA WA DHARARURA KUJIHIFANYI, NASEMA HIVYO KWASABABU KAMA WATATENGENEZEWA NYUMBA ZAO MAZOMBI SI WATAZIVUNJA TENA HALI HAIJATULIA MIMI NAONA WAPEWE MSAADA WA DHARURA KWANZA BAADAYE TENA WASAIDIWE KUANZA MAISHA TENA. WALLAHI CCM MADHALIM LAKINI MUNGU YUPO ATAWALIPA HAYO WANAYOYAFANYA NI MAMBO YA KINYAMA NA KIKATILI KABISA WASHENZI HAO KUNA SIKU NA SISI TUTAWAONESHA TU JAPO TUTAKODI MAJESHI TUTALIPIZA KISASI TU WAJUE HILO TENA KARIBUNI WAJIAANDAE

 3. sadimba 06/04/2016 kwa 4:43 mu ·

  Usistaajabu kumuona mtu anasema jambo lolote hata kama ni la kumuasi mwenyezi mungu sababu ya pesa, kila mtu anapata pesa kutokana na kazi yake ni juu yetu kuitathmini kazi hii ni halali au haramu. Kuna watu wanalipwa kwa kuja humu barazani ilimradi aseme ndio malipo yake yanatimia, binadamu tujichunge laani unayoielekeze kwa mtu ambae sie mlaanifu hukurudi mwenyewe.

  Wale wanaopata hisia za kibinadamu lamsingi ni kuna misaada ya aina mbili msaada wa kujikimu na wa kumuwezesha, msaada wa kujikimu ni huu ambao utawafanya waathirika waweze kupata huduma za msingi ambazo wamezikosa kutoakana na uharamia ulioratibiwa na chama chetu chakavu. Baadae ufuate msaada wa kuwawezesha kurudi katika hali zao za kawaida za kimaisha.

Comments are now closed for this article.