Hakuna kiongozi yeyote Zanzibar atakaeruhusiwa kwenda kumpokea Rais Obama,na hata hao wa Bara watachujwa

Written by  //  29/06/2013  //  Habari  //  Maoni 21

Dar es Salaam. Wakati magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa Rais huyo ni kabambe na hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Pia alisema shughuli za kumpokea Rais Obama, anayetarajiwa kutua Jumatatu saa 8:40 mchana, zitaanza asubuhi kwa maofisa wa Marekani kushika majukumu yote katika uwanja huo, ikiwemo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo, kwa maana wafanyakazi wa uwanja huo kuwa likizo kwa siku mbili.

“Wamesema kuwa wao watasimamia kila kitu kuanzia wageni watakaoingia na kutoka na wataamua nani aingie na kutoka,” alisema Malaki.

Imebainika kuwa hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwemo viongozi watakaompokea pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.

“Wenyewe wana orodha yao na wanajua nani atakuwepo au hatakiwi kuwepo katika kundi la wageni watakaompokea Rais Obama,” alisema na kuongeza:

“Nilimuuliza Ofisa Usalama wa Marekani iwapo nitaweza kumwona Rais Obama, akaniambia: Utamwona ukibahatika kuwepo kwenye orodha.”

Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe naye alikiri kuwa mawaziri wanaotakiwa kuwepo katika msafara wa kumpokea Rais Obama ni wachache watakaochaguliwa tu na Wamarekani, baada ya kuyapitia na kuyachunguza majina hayo kwanza kabla ya kuyakubali.

“Hii sijawahi kuiona, hata sisi wenyewe tunateuliwa na wakishayapitia wataamua, nani aende au asiende,” alisema Chikawe.

Kuhusu Mtunzi

ukweli usemwe

View all posts by

Maoni 21 katika "Hakuna kiongozi yeyote Zanzibar atakaeruhusiwa kwenda kumpokea Rais Obama,na hata hao wa Bara watachujwa"

 1. jazba ni udhaifu 29/06/2013 kwa 6:35 mu ·

  hii ni hali ya kujidhalilisha na kudhihirisha kuwa watanzania ni mamwehu wasioweza kujiamini kwa hio hatuwezi kuaminiwa.
  nna imani kuwa huko senegal na s.africa hawatofanya aibu kama hii ya kuichota nchi nzima kwa siku mbili wao ndio wanauamuzi wa hali hii,hii ni kashfa kubwa lakini ukiwa maskini na mnyenyekevu huwezi kujua ukubwa wa kashfa hii

  • serelly 29/06/2013 kwa 10:01 um ·

   NILIAHIDI NATIMIZA BI IDHINILLAH.

   Naomba radhi kwa kuyaweka hapa maelezo, lengo ni kutimiza ahadi yangu. Rejea katika mada juu ya Uraia wa Bw. NASSOR SALUM JAZIRA.

   Nimejitahidi kumfuatilia huyu jamaa kwa kina na kwa njia tafauti ikiwemo kuzungumza na watu walioko KENGEJA-PEMBA na kwa bahati nzuri kabisa watu wawili miongoni mwa watu niliozungumza nao ni jamaa zake wa damu kabisa kabisa ambao kwa upande wangu ni marafiki wangu wa pete na kidole. Nilihofia kuwa damu ni nzito kuliko maji. Lakini alhamdulillah jamaa ni Wazalendo kuliko hata mimi mwenyewe maana walikuwa serious kiasi kwamba Mimi mwenyewe nilijiona sijafikia climax kabisa, cha ajabu mmoja wao ni Mwanamama {a woman} na alikuwa so straight foward and to the intended points. Bado ZANZIBAR ina watu hai ingawa sio wote lakini wapo wengi ukilinganisha na mazoba.

   1. Kwanza kabisa Huyu jamaa jina lake halisi ni NASSOR SALUM ALI na sio NASSOR ISSA ALI kama kipande cha Uraia wake wa KENYA kinavyoonesha hapo juu.

   Je! Ni kwa nini Kwenye kadi ya Uraia wa Kenya kajiita NASSOR ISSA ALI? Nitajibu chini huko.

   2. Huyu Ndugu NASSOR SALUM ALI ni mzaliwa wa KENGEJA, amesoma katika skuli ya KENGEJA mpaka FORM III ambapo kama mnavyojua kuwa ilikuwa ndio mwisho wa elimu ya Ordninary Level “O Level”. Kwa mujibu wa wadadisiwa hatukupata data zinazoonesha kuendelea kwake kielimu zaidi ya hapo, kwa hivyo tuko silent.

   3. Baada ya Masomo yake alielekea nchini KENYA (Mombasa) ambako Baba yake mdogo {Ammy} anaishi mpaka hii leo, Baba yake huyu mdogo anaitwa Bw. ISSA ALI. Huko alioa binti wa Kikenya na kupata watoto wawili wa kike, bahati mbaya Mke huyu alimuacha (kamtaliki) na aliporejea nyumbani Zanzibar binti yule alibakia na watoto huko huko kwao nchini KENYA.
   Lakini baadae ndugu yake mmoja ajulikanae kwa jina la Bw. SULEIMAN SALUM ALI alikwenda kuwachukua wale watoto nchini KENYA na kuamua kuwalea katika VISIWA VIZURI VYA ZANZIBAR lakini baadae Mama yao aliamua kuja kuwachukua na Kuwarudisha nchini KENYA ambako hadi hii leo wanaendelea na maisha yao. Allah awape maisha mema na awatunze ili awaridhie. Ameen. Ni wana wetu.

   4. Kuhusu kuoa mtoto wa Mh. PANDU AMEIR KIFICHO, jambo hili limetupa taabu sana ingawa tulijaribu kumtafuta mtoto fulani wa kiume wa Mh. Spika ambaye alhamdulillah ni Muislamu na Mzalendo safi lakini hatukufanikiwa kumpata ili kulitolea maelezo jambo hili.

   Hata hivyo utafiti wetu ulingundua kuwa Bw. NASSOR SALUM ALI anataarifa inayofanana na hiyo, kuwa baada ya kurejea nchini ZANZIBAR, mbali na kumuoa binti mmoja ajulikanae kama AZZA (hatukuipata nasabu yake) ambae baadae aliachana nae kisha alioa katika familia ya Mh. Dr. OMAR ALI JUMA (almarhoum) binti huyu anajulikana kama Bi. ZUHURA MGENI MWALIMU ambae mpaka sasa anaendelea kuishi nae na wamebatika kupata watoto takriban watatu kama sijakosea.
   Hata hivyo Bw. NASSOR SALUM ALI aliwahi kumuoa binti mmoja ajulikanae kama Bi. NURU lakini pia ameshamwacha (treaty breaker), sasa huyu ndio tulitia masha kuwa labda ni katika familia ya Mh. PANDU AMEIR KIFICHO lakini we haven’t managed to collect the data in the field.

   5. TUKIMREJEA YEYE MWENYEWE, Information of our interest ilikuwa ni:
   a) Baba yake ni Bw. SALUM ALI (MZANZIBA- KENGEJA) kashafariki Dunia, Allah amrehemu, amzidishie kheri zake na amsamehe makosa yake. Ameen.
   b) Mama yake ni Bi. MKUBWA WA JUU BINT SULEIMAN (MZANZIBAR-KENGEJA) Yuko hai, Allah ampe maisha marefu na mwisho mwema. Ameen.
   c) Bw. NASSOR SALUM ALI amezaliwa ZANZIBAR katka kijiji cha KENGEJA.
   d) Kweli amewahi kuishi nchini KENYA tena kwa muda mrefu tu.

   6. ENEO TETE KUHUSU Bw. NASSOR SALUM ALI:
   a) Kwa sasa anauraia wa KENYA tu bila ya kuwa na ule wa TANZANIA?
   b) Aliukana Uraia wa TANZANIA ili apate ule wa KENYA na baadae kurejea TANZANIA bila ya kuchukua tena Uraia wa TANZANIA? Na hivyo ni MKENYA ama?
   c) Je! kwa sasa anauraia wa nchi mbili TANZANIA na KENYA? Kama ni hivyo Sheria ya Uraia TANZANIA inasemaje?

   Kuhusu jina lake kuwa ni NASSOR ISSA ALI kwenye kadi ya uraia wake wa KENYA ni kuwa alighushi na kuzidanganya Mamlaka nchini Kenya ili apate haki zote za MKENYA, na ili kulirahisisha hilio aliamua kulitumia jina la Ammi yake ambaye yuko humo nchini KENYA kwa muda mrefu na bila shaka ameshakuwa mwenyeji, na kama lingetokea la kutokea ingekuwa rahisi kumkingia kifua kwa kusema huyu ni mwnangu wa kumzaa. Hawa ndio viongozi wetu tuliowakali vinywa wazi ili watushibishe haki kupitia utawala wa Sheria. Watu wa Raha Leo mpo?

   7. Mwisho nini kifanyike? Na nani akifanye? Nawaachia wanaukumbi.

 2. kada wa ccm 29/06/2013 kwa 6:43 mu ·

  @ Bin nassor

  Huyu OB amekuja kupokewa au amekuja kwa ziara ya Tanzania?
  kama amekuja kupokelewa na viongozi hilo ni tatizo kutengwa kwa viongozi wa Zanzibar lakini kama amekuja Tanzania hata huko Bara ni Tanzania

  Cha kujiuliza zaidi amekuja kwa lengo gani,kama kuiba rasilimali za Tanzania kama wanavosema wanasiasa uchwara ataiba za Bara sio za Zanzibar, au mnataka aje na zanzibar aje aimalize mikarafuu na minazi nmanake zanzibar hamna cha kumpa Obama

  Obama amekuja kwa sababu amevutiwa na sera za chama tawala (CCM) za kudumisha demokrasia,Amani,Utulivu,na mshikamano vile vile kwa kukipongeza chama kwa kutekeleza miradi yote mikubwa ya MCC ukiwemo umeem wetu mpya wa kutoka Dar-Fumba mpaka mtoni..na kule Pemba kutoka Tanga…hongera CCM kwa sera zenu nzuri za kuleta maendeleo na sayansi na technologia

  na support viongozi wa zanzibar kutochaguliwa kumpokea Obama kwa sababu wana shughuli muhimu za baraza la wawakilishi ambazo ni bora kuliko huyo Obama…hizo za barazani ni sawa na maisha yetu

  Viongozi wa znz msivunjike moyo kwa hili endeleeni kupiga kazi kwani nci ipo imara na chama tawala kipo Imara kuhakikisha zanzibar ipo juu juu juu zaidi kama ilivo kuwa sa ivi,na juzi tu chama kikiongozwa na Dr.Ali Mohamed Shein chini ya sera za CCM wameweza kuweka taa za barabarani mjini Zanzibar katika phase ya kwanza baadae zitawekwa zanzibar yote na kuwekwa na Pemba kuanzia Mkoani hadi Chake na maeneo mengine huko Pemba…

  Hongera chama,na wale waliokua hawapo znz wambieni kama kuna taa mpya za solar mji mzima unag`aaaaaaa CCM OYEEEEEEEEEEEEE

  • serelly 29/06/2013 kwa 11:22 um ·

   @kada wa CCM

   Mimi ninadhani TAA MPYA hazitadumu kwa sababu hamjatupeleka amani na watoto (wanafunzi) kwa ajili ya kuzizundua wala hamkumwalika angalau basi Mh. Mwai Kibaki ili aje kujionea jinsi tulivyompita kwa maendeleo ili angalau na yeye akapele mifano ya mataa kama haya kule Nairobi ambako kunaoneka ni giza kushinda miji mizuri ya hapa kwetu Zanzibar ambapo miji mingi kati yake serkali ya CCM imeijenga kwa plan za kisasa zinazoonesha thamani na maana halisi ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar 1964.

   Mfano ni mji bora wa Jang’ombe ambao barabara zake ni pana, zilizojaa mataa ya kisasa, nyumba zake ni za plan za kileo zinazokidhi viwango vya kimataifa, ambapo kila nyumba inaweza kufikiwa na gari yoyote ile hata kama ni pana vipi hususan wakati wa dharura ya maradhi au moto, kwa kweli mji huu unapendeza sana machoni mwa wenyeji na hata wageni wanaupenda sana. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI. KIDUMU.

   Vile Mh. Mwai Kibaki mngempeleka katika kitovu cha mji wa Zanzibar ambapo pia ni kituo kikuu cha magari yote ya abiria kijulikancho kama Kituo cha Darajani, ambapo Mheshimiwa Mwai Kibaki angeweza kujionea mwenyewe na kujifanza jinsi serikali ya CCM cha Mapinduzi ilifanikiwa kuunda Baraza letu la Mji ZMC (Manispaa) na namna linavyofanya kazi kwa ustadi na weledi wa hali ya juu kabisa. Kwa sababu eneo hili kikawaida huwavutia wengi hususan nyakati za asubuhi majira ya saa kumi na mbili asubuhi 6:00 A.M mpaka saa mbili mbili za asubuhi 8;00 A.M, hii ni kwa kuwa nyakati hizi eneo la Darajani hutoa harufu bora, mwanana yenye siha njema ambayo fumfanya mwananchi wa kawaida pamoja na wageni wengi wakiwemo watilii wakae kwa muda ili kuifaidi harufu hii ya miasumini ipendwayo na Wanzibari waliowengi. Kumbuka eneo hili liko karibu mno na makao makuu ya chama cha maendeleo CCM-ZANZIBAR chini ya umakamu Mwenyekiti wa Balahau, Mkwe wangu, na Swaahibu wangu Dr. Shein ambae yuko imara katika kuijenga Zanzibar njema atakae aje chini ya kauli mbiu yake ya “MIMI SIMUOGOPI MTU” kauli hii naipenda sana maana ni ya kitaalamu, kisomi, kihekima na yenye busara zilizotukuka. NGUVU MPYA, ARI MPYA, KASI MPYA ( KWA KWENDA NYUMA)

   CCM MONYEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!
   MONYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!

   MAPINDUZIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII!
   PAA WIMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA! Ukirudi chini ushakufa.

   CCM ni CANCER ya maendeleo ya Zanzibar.
   Na tiba mujarabu ya CANCER ni kukata kiungo husika.

   Nawasilisha.
   SERELLY.

 3. Abdul 29/06/2013 kwa 6:44 mu ·

  huyo sheni atawekwa kundi gani

  • serelly 29/06/2013 kwa 11:39 um ·

   @Abdul

   Awekwe kundi gani? Yeye si anajulikana JUHA, kwanini yeye kaona bora kujipendeza kwa Watanganyika kuliko kuwa na mamlaka yake kamili. Hujamsikia pale aliposema kwamba yeye haoni tabu kupeperusha bendera ya Tanzania-Tanganyika anapokuwa nje ya nchi? Ndio hayo sasa wanaume wakija Nchini wanaifata ile bendera anayowaonesha kule kwao ya Tanzania-Tanganyika.

   Wewe si “HUMUOGOPI MTU”?? Nende basi Dar kwa ubabe eti ukampokee Obama uone cha mtema kuni. Aibu hii.

   Kikwete uzi huyo huyo mwnangu usije ukamuombea shavu la kuja hapo mjini kuona na Mjomba Obama, achananaye.

   Shein Hilooooooooooooooo! Sheiniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Halijaitwaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Uitwee! Hakuiti mtu kule. Kaa Vuga hapo usikilize sauti za watoto wetu wanapotibia pale mabaoni.

   Yeee! Seif Ali Iddiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
   Moh’d Abouduuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu! Vipi kimbele mbele upo?. Kaaa chini hakuna kwenda Dar-es-Salaam kwa Mjomba Obama. Viongozi wa Mikoa hawahusiki.

   Sasa labda mtajifunza maana halisi ya Mamlaka Kamili ya Zanzibar. Ukisikia serikali mbili ndio hizo. Mabichwa mtuliage na mkubaligi maneno ya wakubwa.

 4. Ghalib 29/06/2013 kwa 7:31 mu ·

  Na asije bwana hatumtaki kabisa kwani yeye kama nani ? Tunachotaka mamlaka kamili ya zanzibar, Hawa mayahudi ndio waliwauwa mababu zetu 1964 mapinduzi kwa kushirikiana na kibaraka nyerere, hawa hawa ndio walio iyondoa zanzibar UN.

  Lakini tutapambana nao mpaka zanzibar wataiyacha huru, tumechoka nao kabisa, Obama amekuwa akijisifu sana juu ya ndege zake ambazo zisizo tumia rubani na kwa kufanya kazi nzruri, muuwaji mkubwa.

  Mungu awalaani hawa. hatuwataki na wasijeee, viongozi wa zanzibar musiwe na tamaa, obama hatusaidii lolote duniani na akhera , kazi yake ni kupigana na waislamu tu na kuwaibia rasilimali zao.

  OB ujio wake wa Tanganyika ni kuja kuangalia rasilimali wapi atapata pa kuiba, musisahau ile Project ya kigamboni ipo chini ya mzamini marekani, na uchimbaji wa Uranium huko tanganyika ni wamarekani wenyewe. Wacha wachete si wamelala watanganyika.

 5. MKWELI 29/06/2013 kwa 8:36 mu ·

  @ Kada wa ccm

  Mimi ningalitaka kujua kama wewe umekwenda skuli kusoma na kama umekwenda jee umefika hadi darasa gani?

  Na vipi jee ulipokuwa unaandikiwa hii comment ulikuwa umepakatwa? maana haieleweki.

  Kuna usemi kuwi mtu hawi kada wa ccm sharti atiwe. sawa kada endelea kutiwa na hao wanaokuweka mjini kwa maslahi yao na kwa raha yako.

  Zanzibar kwanza upuuzi wa kikada baadae.

 6. zamko 29/06/2013 kwa 8:40 mu ·

  @ Nanukuu. hapo chini

  “Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe naye alikiri kuwa mawaziri wanaotakiwa kuwepo katika msafara wa kumpokea Rais Obama ni wachache watakaochaguliwa tu na Wamarekani, baada ya kuyapitia na kuyachunguza majina hayo kwanza kabla ya kuyakubali…”

  Hapa inaonyesha kwamba majina ya Mawaziri watakaokuwepo ni Wale WAKRISTO TU na Wale walioiga majina yakiyahudi.. Akina Ambroose… Hapa hutaona muislamu waziri kushirikishwa kwani Imani za Wamerakani na Mfumo Kristo wanaona Waislamu ni “EVAL DO”

 7. fey 29/06/2013 kwa 9:16 mu ·

  Na itakuwa vizuri Kama hawatashiririkishwa waislamu kwani haifai hata huyo muislam kuwepo kwenye ziara yake huyo, kazi zao kuuwa waislamu duniani na kueneza ugay, yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu wao wanayafungia kibwebwe almuradi waende against.

 8. Wamtambwe 29/06/2013 kwa 9:21 mu ·

  @ Kada wa CCM
  Mimi nataka kukuuliza kwani taa za Barabarani zatiwa kwa Sera au kwa kutumia pesa za walipa kodi?
  Pili taa za Barabarani zinaashiria maendeleo au maendeleo yanaashiriwa na pato la wananchi?
  Ni kwa kiasi gani umeme unaotoka Bara unawanifaisha Wazanzibari ikiwa gharama za kuuleta hapo Zanzibar tunazilipa wenyewe na halafu isitoshe tunaulipia ghali ukilinganisha na hayo mapatowenyewe ambalo shirika la umeme linakusanya na ukilinganisha na bei anayoilipia mwanachi wa kawaida Tanganyika?

 9. nassor2 29/06/2013 kwa 10:31 mu ·

  Ikiwa viongozi wa Zanzibar hawatoalikwa ni bora kwasabu hakuna haja ya kumpokea huyu killing mashine,hawa walitangaza vita vya MSALABA baadae wakabdilisha jina la TERRORIST lakini lengo ni lilelile,ndio wameziharibu nchi za waislamu nakuwauwa kwa muamilioni na mpaka leo wanaendeleza ajenda yao,kwahiyo ikiwa Zanzibar hawatoalikwa wasisikitike bali washukuru kutomuoa.
  Jengine hawa jamaa wanakuja kukagua mradi wao wa URANIUM na sio kuitembelea Tanzania nandio maana watawachuja watu watakaofuatana na Obama,wao hawajali mtu wala nchi wanajali maslahi yao tu,kama hakuna jambo lenye faida na wao ktk nchi yako hawakujui hawa, aidha una kitu au wanataka kukutumilia kwa hivyo tusifurahie kuja kwao bali tuwe na hadhari nao.
  URANIUM kwao ni mali sana kuliko ALMASI. (KILLING MASHINE.)

 10. nuramo 29/06/2013 kwa 1:23 um ·

  Upumbavu mtupu yaani sehemu nyeti za ulinzi wanapewa wwageni kwa muda wa siku mbili,nahisi ndege za nchi za kiarabu siku hiyo zote watu watadundishwa na watanyanyaswa hapo uwanjani hadi watie akili na pengine baadhi ya ndege nyengine zitaambiwa zisitue Tanzania zikatue Kenya.

  Kumbe ndio Maana upuuzi huu Zanzibar hatuutaki nchi kukabidhi watu kihiyari wacha aishie huko huko Bara,hata waandishi wa habari naona watapigwa bao

 11. nuramo 29/06/2013 kwa 1:27 um ·

  Mi wasi wasi wangu pengine hata hiyo siku ya kuja Obama sio atakuja siku nyengine kabla kisha aingie mitini bila kujua

 12. mohamed 29/06/2013 kwa 5:34 um ·

  Anakuja kuzidisha mipaka ya bahari ili wabongo wachimbe mafuta,kama hamuamini subirini,ki ukweli hawa jamaa USA wanaongoza ulimwengu kwa ubabe,ninachoshangaa mimi kwanini Obama kaja Tanzania?kwa madhumuni gani na malengo gani na kufata nini?tusubiri baada ya mwezi kuondoka kwake kitajiri nini alichojia bongo.

  Kazi kwao

 13. mohamed 29/06/2013 kwa 5:45 um ·

  Halafu mnatubania pua “Tanzania nchi nchi”mavi ya kenge,nchi inapangiwa kila kitu na wageni,mpaka mavi wananawisha ,hii kali wabongo muflis

 14. rayun 29/06/2013 kwa 9:14 um ·

  @kada wa ccm
  wew kweli ni kada wa ccm, mana ujinga umekujaa
  note: ukipeleleza weng wa makada wa ccm ni majahil murakkab

 15. mzaliwa 29/06/2013 kwa 9:40 um ·

  Zanzibar mnavaa majoho,kanzu.kofia,wanawake mitandio hata maskulini,adhana kila pembe ya Zanzibar miskiti kila mwendo wa dakika 15 na mengine mengu ya kujulisha ni Waislamu,
  Obama watu wa aina hii huwapiga vita na kuita magaidi ndio maana hata UN hawashuhuliki na Zanzibar kunyang’anya kiti chake kwani wanajua litakua Taifa lenye nguvu za kiislam,
  Sasa wache Tanganyika wapigane mikia madume kwa madume,sisi tutafata alivo tueleza Mtume (s.a.w) tuowe wanawake mwisho wanne kama unaweza kuwapatia wote mahitaji yao sawa.
  Na asifike huku kabisa.
  Zanzibar huru.

 16. tuachiwe 29/06/2013 kwa 11:08 um ·

  Angalau Afrika Kusini Kapata maandamano japo madogo.
  Lakini Watanganyika wao ndio wanakubali kudhalilishwa.
  Ni kheri Asende huko Zanzibar, maana hii inakaribia na kufuru.
  Subhana Allah!!!

 17. Alberta 30/06/2013 kwa 6:00 um ·

  Bora asende kule Zanzibar manake akienda wale mazombi ya kule kina Shweni na Dudu vule IDD watakubali watufanye wote mashoga.

Comments are now closed for this article.