Wapenda Taarabu za kale.

Written by  //  09/10/2014  //  Burudani  //  Maoni 4

Kwa mnaopenda Taarab ,mnaweza kutembelea hii streaming na utaburudika kwa nyimbo za kale za taarabu za Zanzibar,just unaweza kuweka browser pekee na kuiminimize.

http://tunein.com/radio/Bongo-Radio—Taarab–Mduara-Channel-s149152/

Kuhusu Mtunzi

Mmetuchota akili na kutuzuga lakini mumesahau kuwa macho yetu yanawatizama wapi mnatupeleka-Salamu kutoka Tarime.

View all posts by

Maoni 4 katika "Wapenda Taarabu za kale."

 1. Tafrani znz 09/10/2014 kwa 4:02 um ·

  Huu sio muda wa tarabu usituzinguwe. kama umetumwa msg yako haijafika hapa.

 2. sabra 09/10/2014 kwa 4:06 um ·

  Sawa sawa tarabu washacheza mabibi na mababu. Sio sie kizazi kipya.

 3. Kamwene 09/10/2014 kwa 4:36 um ·

  @Tafrani znz na sabra ,kama unazijua taarabu za kale ,basi unapozisikiliza kwa mida hizi huwa zinakuzidisha mori wa kuipenda Zanzibar na unakuwa kama unaiona ni jinsi gani watu wakiishi kwa wasaa na wapi leo tulipo ,yaani zinakujia hisia nzuri tu za Nchi yako na si vinginevyo..

 4. jazba 09/10/2014 kwa 8:56 um ·

  MWENYE UWEZO WA KUPOST HAPA TAFADHALI IWEKE HII MADA HAPO JUU ILI WADAU WAICHANGIE HAPA

  Sitta adanganya umma

  Katiba iliyokabidhiwa kwa rais ina utata
  Kilio cha Katiba Mpya sasa kuanza upya

  Na Yusuf Aboud
  SHEREHE za kumkabidhi rais “Katiba Inayopendekezwa,” zimeingia dosari kutokana na kasoro nyingi, ikiwemo ya kutopatikana kwa theluthi mbili za wajumbe kutoka Zanzibar, MAWIO limeelezwa. Katika mfululizo wa vitimbi vilivyoleta kasoro:
  Mjumbe mmoja wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye anatoka Zanzibar, amefanywa kuwa mjumbe wa Tanzania Bara.
  Wajumbe waliokuwa nje ya nchi, inaonyesha wanadaiwa kupiga kura kabla ya siku yenyewe.
  Wajumbe waliokataa vipengele kadhaa katika andiko la mwisho la Katiba inayopendekezwa, wamechukuliwa kuwa wamekubali mapendekezo.
  Wajumbe waliokuwa Hijja Makkah, nchini Saudi Arabia; na mmoja aliyeko nchini India, wanadaiwa kupiga kura tarehe 28 Septemba 2014; wakati siku ya upigaji kura kwa Katiba inayopendekezwa, ilikuwa 29 na 30 Septemba.
  Wajumbe wote walioko nje, wanaonekana kupiga kura kwa ibara zote na siyo kwa utaratibu wa uliotumika Dodoma.
  Tarehe 28 Septemba 2014, ambayo ni siku wajumbe waliokuwa nchini Saudi Arabia wanadaiwa kupiga kura, ilikuwa Jumapili.
  Taarifa kutoka nchini Saudi Arabia zinasema Ubalozi wa Tanzania nchini humo, ambao ulitajwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samwel Sitta kuwa ungesimamia zoezi zima la upigaji kura kwa wajumbe waliokuwa huko kwa ibada ya Hijja, ulijivua mapema jukumu hilo.
  Barua kutoka ubalozini inasema, “…kwa hivyo, kwa mazingira ya Ibada ya Hijja huko Makkah na katika viwanja na sehemu tukufu za Mina, Arafat na Muzdalifa; ni vigumu kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kuweza kupiga kura wakiwa huko.”
  Akiandika kwa msisitizo, ofisa wa ubalozi anasema, “Wanaoruhusiwa kufika huko ni mahujaji tu, ambao wanakuwa na vitambulisho maalum katika vikundi vyao; na kunakuwa na ulinzi wa hali ya juu.”
  Aidha, ubalozi unasema, “Hijja ya mwaka huu imekuwa na ulinzi mkali kutokana na nchi ya Saudi Arabia kuwa katika vita dhidi ya magaidi wanaojiita wa Himaya ya Kiislamu (ISIS), huko Iraq na Syiria. Serikali ya Saudi Arabia imetangaza wazi kuwa mtu yoyote asiyekuwa Hujaji hataingia katika eneo la Haram na kwingineko. Hii ndiyo hali halisi.”
  Haijafahamika wanaoitwa wajumbe-mahujaji kutoka Tanzania, ambao wanadaiwa kupiga kura, walikuwa wapi wakati wanapiga kura zao; wakati ubalozi umekwishatoa maelezo kuhusu kutoweza kusimamia zoezi hilo katika mazingira ya Hijja.
  Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inataka, ili Katiba inayopendekezwa kwa wananchi iweze kupitishwa na “Bunge la Katiba” na kwenda kwa wananchi kwa ajili ya kura ya maoni, sharti ikubaliwe kwa theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar.
  Ni hapa ambapo Mjumbe wa Zanzibar alifanywa kuwa mjumbe kutoka Tanzania Bara kwa sababu ambazo hazijaelezwa. Wachunguzi wa mambo wanasema ilikuwa “kupunguza kura ya hapana kutoka Zanzibar” kwa kuwa mjumbe huyo “alionyesha dalili zote za kukataa mapendekezo.”
  Mjumbe huyo ni Maulida Komu (Anna Komu), mbunge Viti Maalum, kutoka Chama cha Demekrasia na Maendeleo (Chadema).
  Jana, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Rais Kikwete alitarajiwa kukabidhiwa “Katiba Mpya Inayotarajiwa.” Hatua hii inakuja baada ya Sitta, aliyekuwa mwenyekiti wa Bunge Maalum, kutangaza kuwa mchakato umekamilika.
  Katika mchakato huu, maoni mengi ya wananchi yameachwa; msingi wa katiba umebomolewa; na muundo wa serikali tatu ambao ulipendekezwa kuwa bora kwa maendeleo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, umetupiliwa mbali.
  Maelezo yaliyomo katika barua ya balozi nchini Saudi Arabia, yanaongeza utata juu ya kinachoitwa mahujaji kupiga kura.
  Kwa mfano, akiandika kwa mwenyekiti wa bunge hilo, mjumbe kutoka Zanzibar, Dk. Maua Daftari anasema, “Nakiri kukubaliana na vifungu vyote vya Katiba kama tulivyopitisha.”
  Andishi la Dk. Daftari lililoambatanishwa na “fomu ya kupigia kura,” liliandaliwa na kutumwa tarehe 28 Septemba. Inaonyesha kuwa Dk. Daftari anakubaliana na mapendekezo juu ya ibara zote za katiba.
  Hata hivyo, katika andishi lake kwa mwenyekiti wa Bunge Maalum, Hassan Salim Turky, anayedaiwa kupiga kura akiwa hospitalini Chennai, nchini India, hakutamka iwapo amepiga kura ya ndiyo au hapana.
  Amesema, “Mhe Mwenyekiti, kwa heshima kubwa naomba nikupongeze wewe binafsi pamoja na makamu wako wa mwenyekiti na Kamati ya Uongozi ya Bunge kwa namna mlivyoniwezesha kutumia haki yangu ya kidemokrasia na kuweza kupiga kura yangu nikiwa hapa Chennai, India hospitalini.”
  Amesema, “Nawapongeza sana na nawatakia kila la kheri waheshimiwa wajumbe wenzangu wa Bunge la Katiba katika kufanikisha kazi hii kubwa inayotukabili hivi sasa.”
  Hayo yanaandikwa wakati Mjumbe anayedaiwa kutumwa katika nchi hizo, ili kupigisha kura, ametajwa kuwa ni Suleiman Haji Suleiman. Haijafahamika alifanya nini Saudi Arabia ambako hakukuwa kunaingilika na tayari kulikuwa na msimamo rasmi wa ubalozi wa Tanzania.
  Suleiman Haji Suleiman ni mwandani wa kinachoitwa, “mtandao wa urais” wa Shamsi Vuai Nahodha.
  Tofauti ya muda kati ya India na Saudia, ni zaidi ya saa nne; tofauti kati ya Tanzania na India, ni saa tano na tofauti kati ya Tanzania na Saudi Arabia, ni saa moja.
  Gazeti hili limeshindwa kufahamu iwapo Suleiman alitumia ndege binafsi kusafiri kwenda India kupigisha kura mtu mmoja; na kisha kuondoka siku hiyohiyo na kufika Saudi Arabia kufanya kazi hiyohiyo (ambayo balozi aliishaeleza kuwa haiwezi kufanyika).
  Maulida Komu aliyefanywa mjumbe kutoka Tanzania Bara, ndiye aliyekuwa mgombea mwenza wa Freeman Mbowe katika uchaguzi mkuu mwaka 2005.
  Ni katika kipindi hicho, utata juu ya utaifa wake Visiwani, uliibuka na kuhojiwa mahakamani, baada ya Mchungaji Christopher Mtikila kufungua kesi kupinga mwanasiasa huyo kuwa mgombea mwenza kwa kile alichodai, siyo raia kutoka Zanzibar.
  Mahakama Kuu ya Zanzibar, baada ya kusikiliza pande zote mbili, iliridhika kuwa Maulida anatoka Zanzibar.
  Akizungumzia utata wa kura, Ismail Jussa Ladhu amesema, “Kura zilizopigwa kupitisha Sura ya Kwanza hadi Sura ya Kumi ya Rasimu ya Katiba, hazikupata theluthi mbili. Hii ni kwa sababu, katiba hii haipelekwi vipandevipande kwa wananchi. Inapelekwa yote.”
  Amesema, “Siku ya kwanza ya kupiga kura, wajumbe saba (7) wlikataa katiba. Siku ya pili aliongezeka mwanasheria mkuu wa serikali. Jumla yake ni wanane (8). Wajumbe wa UKAWA wamewataja kuwa wako 65; ingawa sisi tunajua wako 66. Mjumbe mmoja hakupiga kura.”
  Jussa anasema, kwa hesabu ya wajumbe 219, theluthi mbili ni wajumbe 146. Wajumbe ambao hawakupiga kura na wale waliokataa vifungu vya katiba, jumla yao ni 74. Hivyo katiba ya Sitta na CCM yake imepitishwa na wajumbe 145, badala ya 146 wanaotakiwa kwa mujibu wa sheria.”
  UKAWA unaundwa na vyama vya NCCR- Mageuzi; Chama cha Wananchi (CUF); Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), National League for Democracy (NLD); Democratic Party (DP) na baadhi ya wajumbe kutoka kundi la 201 la wajumbe walioteuliwa kutoka asasi za kijamii.
  Utata wa kura unaongezeka pale mjumbe aliyetumwa kwenda India na Saudia Arabia kuwapigisha kura wajumbe wa Bunge Maalum, kupigisha kura hizo kwa siku moja katika nchi zote mbili.
  Kwa mfano, Dk. Daftari; Asha Dodoo Mtwangi; Shawana Bukheti Hassan; Salim Turky na Amina Andrew Clement, wote wanadaiwa kupiga kura zao tarehe 28 Septemba 2014.
  Wakati Dk. Daftari akionyesha kukubaliana na vifungu vyote vya katiba iliyopendekezwa na Turky kutosema lolote; Bukheti alisema, “…sina pingamizi juu ya Ibara yoyote ile kwa yale ambayo yamo kwenye rasimu hiyo.”
  Kauli kuwa anakubaliana na yote yaliyomo katika “rasimu,” inaweza kutafsiriwa kuwa, kile ambacho mjumbe anakubaliana nacho, ni “Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba” na siyo katiba iliyopendekezwa.”
  Rasimu ya Jaji Warioba, ilipendekeza kuwapo Nchi Moja yenye Shirikisho la Serikali Tatu – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  Muundo wa Muungano wa serikali mbili, uliosheheni malalamiko ya miaka 50 ya “Tanganyika kuvaa koti la Muungano” na Zanzibar kugeuka “koloni la Tanganyika,” umekuwa uking’ang’anizwa na CCM; na ndio Sitta amefanikisha katika hatua ya mwisho.
  Aidha, “Katiba inayopendekezwa,” imepatikana chini ya vitisho, matusi, kejeli na ghiliba za viongozi wa CCM na serikali. Hata mwanasheria mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, aliyekataa vifungu vingi katika andishi la mwisho, tayari amefukuzwa kazi na Rais Mohamed Shein.
  “Huu ndio wakati mwafaka kwa wananchi kuanza kufikira kuwa na Katiba Mpya. Hiki ni bomu,” ameeleza Tundu Lissu, mwanasheria wa Chadema huku akiahidi kuzunguka nchi nzima kuelimisha wananchi jinsi ya kukataa “hatari iliyoandaliwa na Sitta.”
  Chanzo: Mawio
  Mwisho.

Comments are now closed for this article.