Malinzi aahidi kuipatia Zanzibar uanachama Fifa

Written by  //  22/11/2013  //  Michezo  //  Maoni 18

jamal_malinzi

Na Salum Vuai, Zanzibar
WIKI tatu tangu Jamal Malinzi achaguliwe kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana aliwasili Zanzibar na kufanya mazungunmzo na uongozi wa Chama cha Soka (ZFA), na kuahidi kulivalia njuga suala la kuipatia Zanzibar uanachama wa Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA).

Katika mazungumzo hayo Malinzi alizungumzia suala la Zanzibar kupata uanachama wa FIFA na CAF ambapo, alisema kuwa katika uongozi wake atahakikisha kuwa analishughulikia suala hilo, ili kuona kwa jinsi gani ataweza kulimaliza kwa Zanzibar kupata uanachama.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa VIP uwanja wa Amaan, Malinzi alisema katika kipindi chake cha uongozi TFF, atahakikisha Zanzibar inapata uanachama wa FIFA pamoja na ule wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kwa sasa, Zanzibar ni mwanachama shirikishi wa CAF, ambapo klabu zake zinazotwaa ubingwa wa ligi kuu na nafasi ya pili, huiwakilisha kwenye ligi ya mabingwa na Kombe la Shirikisho.

“Kwa kushirikiana na wenzangu TFF na ZFA, tutalishughulikia suala hilo ili kuona jinsi tunavyoweza kulimaliza kwa Zanzibar kupata uanachama wake FIFA na CAF,” alieleza Rais huyo.

Aidha, Malinzi alisema umefika wakati sasa ZFA ikawa na mwakilishi wake ndani ya Kamati Tendaji ya TFF, na kueleza kuwa, akisema atapeleka pendekezo katika kamati hiyo, ili kuifanyia marekebisho katiba ya shirikisho katika mkutano mkuu ujao.
Alifahamisha kuwa, marekebisho hayo yatafanyika kwa lengo la kuingiza kifungu kitakachoipa Zanzibar nafasi hiyo katika Kamati Tendaji ya TFF.

Juu ya muundo wa timu za Taifa za Tanzania kwa wachezaji walio katika umri tafauti, Malinzi alisema hivi karibuni, kutafanyika kikao maalumu cha jopo la walimu wa michezo hapa Zanzibar, kwa lengo la kupanga mikakati ya kuimarisha timu hizo.
Kwa upande wa ligi ya Muungano ambayo imekufa kwa miaka mingi baada ya Zanzibar kupata nafasi ya kushiriki yenyewe katika michuano ya CAF, alisema atahakikisha ligi hiyo inarudi tena japo kwa misingi mipya badala ya ile ya zamani.
Katika hatua nyengine, Rais huyo aliyerithi nafasi ya Leodgar Tenga aliyemaliza muda wake, alisema TFF hivi sasa iko katika mipango ya kuutumia utalii katika kuinua michezo, kwa kuwalika magwiji wa soka wa zamani pamoja na klabu maarufu duniani.
Itakumbukwa kuwa, miaka miwili iliyopita, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Ali Juma Shamuhuna, aliongoza ujumbe mzito jijini Geneva, Uswisi kuiombea Zanzibar uanachama wa FIFA, lakini ombi hilo liligonga mwamba ikielezwa kuwa nchi hiyo haitambuliwi kimataifa kwa kuwa inabebwa na Tanzania kupitia TFF.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wote wa juu na wengine wa ZFA akiwemo Rais wake Ravia Idarous Faina.

Zanzinews

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 18 katika "Malinzi aahidi kuipatia Zanzibar uanachama Fifa"

 1. Ashakh (Kiongozi) 22/11/2013 kwa 7:46 mu ·

  Ukisikia UKOLONI ndio huo. Yaani hadi wao wakubali ndio wakatuombee kujiunga na jumuiya kama hizi ambazo hata kisiasa hazimo. Haya mabwana mabepari wetu nendeni mukatuomee sisi letu ni kufanikiwa tu.

  Kinachonishangaza na ileile janja ya nyani. Sasa ikiwa tunakwenda kuombewa uanachama kuna haja gani ya kubadilisha vifungu vya katiba yenu hali ya kuwa hatuhitaji tena kuingizwa.

  Huu si ndio ujuha. Zanzibar ikiwa mwanachama kuna haja gani ya kupeleka mjumbe TFF? Tena basi kasema kuwa ligi ya muungano imekufa kwa vile Timu za Zanzibar zinashiriki kombe la Afrika, halafu anarudi kulekule kwenye athari za kikoloni.

  Msimamo ni huohuo TFF ni chama cha mpira cha Tanganyika, hakuna haja ya mjumbe kutoka Zanzibar kushiriki. Ni chama chao wapange mambo yao, ya Zanzibar waachiwe wenyewe.

  safari yetu haiko mbeli tutafika, na Zanzibar itakuwa mwanachama wa FIFA, inshaallah.

 2. ssba 22/11/2013 kwa 8:19 mu ·

  Mijitu ya kwetu wataikimbia hiyo nafasi ya tff badala ya kudai fifa

 3. Ghalib 22/11/2013 kwa 11:01 mu ·

  @academi

  Ahsante kwa kutoa jibu, ukweli ni kwamba TFF wajitoe kamaTanzania waingie kama Tanganyika, Zanzibar itapata wenyewe kujiunga na fifa bila ya kuombewa.

  Acheni kupumbazwa wazanzibari, watanganyika wanajifanya wao wako top eti watatuombea , pumbav

  • mwidady 30/11/2013 kwa 4:41 um ·

   umesema kweli wangu.

 4. Finga ya pwani 22/11/2013 kwa 11:05 mu ·

  Mimi najaribu kuangalia uhusiano uliopo kwenye uongozi wa TFF hata Malinzi akaja Zanzibar na kufanya mkutano na viongozi wa ZFA. Malinzi kagombea na kuchaguliwa na watanganyika na Zanzibar haikuhusika na kumpigia kura wala kuhesabu hizo kura zake lakini baada ya kuchaguliwa anakuja Zanzibar nakujidai kwamba atahakikisha kwamba Zanzibar inapata uanachama wa FIFA na CAF hii hapa kweli kuzibana macho. Huu ni usanii mtupu ikiwa waziri wa serikali ya Zanzibar alishindwa aweza yeye Mtanganyika kwa maslahi ya Zanzibar. Tungoje tuone kwani imani yangu mimi ni kutafuta mamlaka ya visiwa vya Zanzibar yote hayo ya kisanii yatakwisha. Mamlaka kamili ndio suluhisho la michezo, kilimo, mifugo, biashara, elimu, uraia na uhamiaji na mengineo. Ila tukiangalia na kuwasikiliza akina Malinzi na wezao CCM kila kitu hatutokifanya.

 5. Wamtambwe 22/11/2013 kwa 12:26 um ·

  Hilo suala sio la FIFA, bali ni suala la kisiasa. Kutupatia uanachama wa FIFA maana yake Zanzibar ni nchi huru na Maana yake Muungano haupo tena au ni Mkataba kama ilivyo kwa EU.
  Sasa sielewi ubavu huo kaupatia wapi?

 6. Multiways 22/11/2013 kwa 1:15 um ·

  ninavyoamini mm hawezi kuiombea zanzibar kwenye fifa wala caf,,hii ni kutokana tff haihusian na zfa,,kwamaana mambo ya mpira hayamo ktk hatamu ya muungano,,inaonekana alisema hayo bila ya kuzingatia mising ya muungano

 7. rasmi 22/11/2013 kwa 3:01 um ·

  Ahsante academi kwa kumwaga darasa. Nadhani hawa Tanganyika United wameshaanza kuona kwamba Zanzibar inajipapatua sasa tuendelee na ujanja zaidi, kama alivyosema Ghalib hapo hapa kila mtu ni kivyake tu wasituletee zao. Tokea lini michezo limekuwa ni katika makubaliano ya huo wanaouita muungano!

  Malinzi aende akaombe Tanganyika ijiwakilishe kama Tanganyika na sisi automaticaly tutakua hakuna kipingamizi.

  Alipoenda waziri Shamuhuna kuomba Zanzibar iwe na uwakilishi wake ni wao wao ndio waliolkuwa mashawishi tusipate, iweje leo!

 8. mohamed 22/11/2013 kwa 5:18 um ·

  Hakuna lolote hapa mavi matupu.

 9. pandu33 23/11/2013 kwa 5:12 mu ·

  Tunajitia falsafa ndefu kujifanya kuwa kama majuha ,hamjitambui kuwa toka 1964 april nchi ishauzwa na mnunuzi mfallme nyerere,zanzibar haiwezi tena kujulikana ki international mpaka wajikombowe wenyewe na huo unoitwa muungano ambao sisi na wengine ndio tunafaidika ,tizama udhalilishati wa daraja la mwisho leo mtu kama huyo malinze anakuja zanzibar anakaa na hao mijuha anawaambia o.k majuha kama mnataka kujiunga na fifa basi mm nitakupelekeni ,bado hamjijui kuwa nyinyi hamna nchi na hao ndio mabwana mpaka watakapo amua ndio hivo hivo, mm fikra zangu kabla ya hiyo fifa haya mashindano ya east and cenral wazanzibari wangeinsist lazima iweko nchi tanganyika sio tanzania bara atleast watu wengine wangefahamu ada hii tanzania ndio tangayika kumbe,, ,tuombe mungu mwenyezi mungu aturejeshee nchi yetu na ikiwa tumekosa mwenyezi mungu atuondoshee madhila haya ya rabii,na lamwisho nasema tuondoshe tafauti zetu tuwe kitu kimoja sote kwa manufaa ya nchi yetu.

 10. kifuudume 23/11/2013 kwa 2:44 um ·

  Porojo za watanganyika ivi anauwezo gani wa kuimbea Zanzibar Kwenye FIFA,
  maneno ya wengi ujua wa hao vibaraka wao. walikuwa hawana haja hata yakuaawamsikiliza

  Zanzibar hao wanaoshuhulikia mipira wameshinwa kuipeleka fifa iwe leo.

 11. salali 23/11/2013 kwa 3:42 um ·

  Nihaki yetu kuwa wanachama wa FIFA sio ombi acheni kutuletea usanii.

 12. buhanan 24/11/2013 kwa 4:36 mu ·

  Ndugu Jamal Malinzi Rais wa Shirikisho la Soka(TANGANYIKA) (TANGANYIKA) (TFF), TUACHIE TUPUMUE NA HAKUNA ALIEKUTUMA ACHANA NA ZANZIBAR.Mwiba ulupoingia sasa unatokea pale pale usijidanganye bure .Zanzibar Kupata Uanachama FiFa ni haki yao na sio FIFA tu bali uanachama wa mahala popote Duniani wanapotaka kujiunga kwa MASLAHI Ya ZANZIBAR wanayo haki bila ya kuingiliwa na Tanganyika na jirani zake .Usijipendekeze bureeee kwa Wazanzibari hatuna haja na weye na wao achana na sisi .Mwisho Chumbeeeeee.

 13. zamko 24/11/2013 kwa 7:07 um ·

  @Academi.

  umefafanua vitu vizuri sana na vya muhimu katika Uwanja wa Utamaduni wa Mpira.. Lakini kwa upande wetu sisi Wazanzibari. Hata ikiwa Zanzibar itaingia kwenye FIFA. Basi hatuna tutapofika.. Kwa Ubinafsi wetu na Uchoyo…

  Mfano itizame hiyo ZBC- zanzibar Boadcasting jinsi inavotumiliwa na Akina BORAFYA Silima, Seif Ali Iddi, Na UVCCM.. Kweli ni Nchi gani itakayokubali kufanya kazi na watu kama hao?.

  @Ghalib.
  Nikweli unayosema.. Kinachotakiwa ni Tanganyika kujivua koti la Muungano na kuwa kama Tanganyika na kuiacha Zanzibar ikaingia kama Zanzibar.. Hakuna Mtu hata mmoja mwenye uwezo yakuiombea Zanzibar kujiunga kwenye FIFA… Huyu MALINZI asijitie Ukubwa wa Nzi..

  Sisi wazanzibari tumezoea kuja kudanganywa na Watanganyika ambo ndio Tunao wakumbatia nakuwaramba M…..ko yao…

Comments are now closed for this article.