Francis Mutungi ndio mtatuzi wa mgogoro wa CUF

Written by  //  19/03/2017  //  Habari  //  Maoni 3

Leo nimeangaza njia za kutatua mgogoro ndani ya Chama cha Wananchi CUF. Kawaida huwezi kutatua tatizo bila ya kujuwa chanzo chake.

Asili ya mgogoro wa CUF ilianzia pale aliyekuwa Mwenyekiti wake Ibrahim Lipumba kutaka kurudi kwenye uongozi baada ya kujiuzulu nafasi yake. Ilichukuwa takriban miezi 8 akiwa nje ya utendaji wa chama alipokuja na wazo la kubadili uamuzi wake. Hadi hapo hapana kosa wala ubaya.

Ubaya ulianzia pale alipovamia mkutano mkuu ambacho ndio kikao kikuu cha chama, na wakati yeye hakuwa Mjumbe wala hahusiki nanacho. Hili ndio kosa la kwanza, kuwazuwia wanachama kufanya maamuzi na muelekeo wa chama chao kisha kuwajengea khofu, kuleta vurugu, uharibifu nk. Hapa ilistahiki vyombo vya sheria vifanye kazi yake.

Muda wote huo Lipumba alikuwa anajitambua kuwa sio Mwenyekiti wa CUF. Msumari wa mgogoro uligongomewa na Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi, kwa sababu anazozijuwa, alipompa Lipumba mamlaka. Akitupilia mbali hoja kwamba Lipumba amejiuzulu, mkutano mkuu umeridhia kujiuzulu kwake, na Baraza Kuu lishafuta uwanachama wake.

Lakushangaza kwenye website ya Ofisi ya Msajili wanamtambua Lipumba kama Kaimu Mwenyekiti. Cheo hicho kimeanza lini, kwa katiba gani na lini kitasita. Haya ni baadhi tu ya maswali niliyojiuliza. Wewe msomaji unaweza kuongeza.

Hapo ndio nilopohukumu kuwa utatuzi wa mgogoro huu uko chini ya mamlaka Msajili wa Vyama. Ingawa katika majukumu yao hawakulisema hili, lakini ni kwa vile Msajili ndio chapuo yake.

Ofisi ya Msajili inasema inashughulika na kazi za: kusajili vyama vya siasa, kugawa ruzuku kwa vyama, kufuatilia mapato na matumizi ya vyama, kusimamia utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa pamoja na kuwa secretariats ya Baraza la vyama vya siasa. Hivyo utatuzi wa mgogoro umo mikononi mwao.

Naomba kwa pamoja tushirikiane tumtake Jaji Francis Mutungi kuweka sawa pale alipokosea/alipokusudia juu ya mgogoro wa CUF. Laiti ingekuwa si kujichomeka yasinge fikia haya. Hivyo tumtake ajichomoe kwa kufuta yale maelekezo yake yaliyochochea.

Kwa mujibu ya website Lipumba na Kaimu Mwenyekiti, kukamatwa nafasi kuna muda wake, Lipumba hana viongozi kutoka Zanzibar, wote wamefukuzwa uanachama. Na yoyote atakeyemteuwa atafukuzwa uanachama, hivyo ataishia wapi?

Msajili turudishie nidhamu ya chama chetu

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 3 katika "Francis Mutungi ndio mtatuzi wa mgogoro wa CUF"

 1. zamko 19/03/2017 kwa 9:28 mu ·

  @ Ashakh

  ahsante kwa makal yako lakini Kichwa cha Habari naona hakifanani na Ulichokiandika. samahani lakini. Mimi Ningekuomba uandike Kichwa Hiki.. ” Ni sheria ipi yampa Mutungi kuingilia Utendaji wa CUF”

  Jengine tayari umeshasema kwamba msajili wa Vyama kajichomeka ndani ya Maamuzi ya Chama na Tunajuwa kwa sababu gani . Nikutaka Kumuondoa Maalim Sefu madarakani ili CCM iendelee Kututawala Kiharamu . Kwasababu imevunja katiba ya nchi. sasa tena unakuja na heading inayomtaka yeye Mutingi Mtumishi wa CCM alieteuliwa hapo kwa dhamira moja tuu nayo Kuichafua CUF na Ukawa. Kwasababu CCM wanajuwa Zanzibar hawana kura hata kama CUF itakufa kama Sefu Ali Iddi alivokusudia.

  Lakini naamini hio 2020 wanayojilabu kama CCM Watashinda Ushindi wa Kishindo Visiwani bac mimi nasema ni Ndoto za mchana. Wazanzibari watahiari watie kura zao kwa Chadema ikiwa kama CUF haitokuwepo .

  Nnanukuu setence yako
  “Ofisi ya Msajili inasema inashughulika na kazi za: kusajili vyama vya siasa, kugawa ruzuku kwa vyama, kufuatilia mapato na matumizi ya vyama, kusimamia utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa pamoja na kuwa secretariats ya Baraza la vyama vya siasa. Hivyo utatuzi wa mgogoro umo mikononi mwao.”

  Kutokana na sheria na kazi za Msajili wa vyama kama zinavoonekana hapo chini. mimi nasema jibu la kulitatua tatizo hili tunalo sisi Wazanzibari.

  mimi sitaki kumwaga Mtama kwenye kuku wengi. Lakini unaweza kulipa hata pesa tatizo hili likaondolewa.

  Mgogoro wa CUF umewekwa na watu 3.
  Sefu Ali Iddi
  Mutungi.
  Lipumba.
  Vichwa vitatu vya Watu hawa Vikiondoka Basi tutaweza kufanya Jengine la maana. Kwasababu hawa wametufanyia Dharau ya hali ya juu sisi Wazanzibari.

  Umesikia Kukiwa na 2 state of Israel tena tokea alipoondoka Isak Rabin?
  hao wote Wanaojitia mapatano ya Two State of peace Deal. Ni waongo.
  Hivo Choice is ours.

  na nakwambia Miaka 5 ikesha CUF itakuwa imefutika katika Macho ya Wazanzibari lakini naamini Kwamba Tukikaa Pamoja tutapata Njia mbadala. Kwani CUF ni Chama tuu kinaweza kuja na kuondoka.

 2. Piga nikupige 19/03/2017 kwa 4:11 um ·

  Msimamizi mkuu wa mgogoro wa kupikwa ndani ya CUF ni Magufuli, huyu ndiye kinara wa kila mipango miovu inayo pangwa na Mutungi,Limpumba na kundi lao. Magufuli hana haya, aibu wala utu katika kuiangamiza CUF kila hatua inayo fanyika katika hujuma basi mna mkono wake. Kama kuna adui wa CUF namba moja basi ni Magufuli.

 3. MAWENI 19/03/2017 kwa 9:29 um ·

  Wapishi wa vurugu liliopo hivi sasa ni Kikwete , Mkapa, na Mzee rukhsa wakisaadiwa na ” Usalama wa Taifa”. Hao Wazanzibar wa Zanzibar wanawatumikia mabwana tu. Kwani Zanzibar ni koloni .
  Tokeya 1964 walipiga marufuku upinzani wa aina yoyote. Waliuwa, walifunga, walitesa, wakawafukuza wazanzibari nchini kwao. Jee imezuiya wazwnzinabri kudai haki ya nchi yao?
  Uhuru, Haki, na Mamlaka kamili. Haki haipotei wala haizami.
  Iko siku Zanzibar itarudisha mamlaka yake kamili na kuwa dola huru katika jamii ya dola uhru zenye mamlaka kamili Duniani.

Comments are now closed for this article.