Fomu za kugombea uongozi wa CCM zadoda Zanzibar ~ vijana wazisusa

Written by  //  01/05/2017  //  Habari  //  Maoni 3

DSC_1592

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk Ali Mohamed Shein wakinong’ona na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini,Unguja, Mohamed Raza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu mbali mbali za mpira wa soka. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Skuli ya Dunga, Kusini Unguja 28/4/17 :Picha na Ikulu ya Zanzibar.                             

Na Haji Mtumwa – Mwananchi
Jumatatu, Mei 1, 2017

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewaambia vijana na makada  waliosusia kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho, kuwa ni aibu kutoa kauli ya namna hiyo kwa nchi yao.

Kauli hiyo ya Dk Shein imefuatia ile ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Sauda Mbamba aliyesoma taarifa ya mkoa huo mbele ya Dk Shein katika hafla maalumu ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vijana wa Jimbo la Uzini, akisema vijana wengi hawachukui fomu hizo.

Ikiwa ni kama majibu kwa vijana hao, Dk Shein amesema suala la msingi ni kuwa na uzalendo ambao ndiyo mwongozo sahihi katika kulinda heshima na nidhamu ya mtu kwenye jamii na taifa kwa ujumla.

“Kilio kikubwa cha vijana hao inawezekana ikawa ni suala la ajira, lakini suala hilo ni gumu kwani haiwezekani kila mtu kuajiriwa na serikali kama wengi wanavyotaka,” alisema Dk Shein.

Makamu huyo wa Mwenyekiti wa CCM amesisitiza ajira ni changamoto kubwa kutokana na kuwa kwa sasa idadi ya watu visiwani humo ni kubwa hali inayosababishwa na Wazanzibari kuzaliana kwa wingi ikilinganishwa na nchi nyingine.

“Hivi sasa Zanzibar tumeongezeka sana na hili linachangiwa na sisi wenyewe kwa kuzaa sana, hivyo ni vigumu kila mmoja kupata ajira serikalini kwa kuwa utaratibu wa ajira hauko hivyo,” alisema Dk Shein.

Awali, Sauda alimwambia Dk Shein kuwa pamoja na chama kutangaza kwa vijana kuchukuwa fomu za uongozi, bado fomu hizo zimedoda matawini.

Pia, Katibu huyo wa Mkoa wa CCM alisema jambo hilo linahitaji nguvu ya pamoja ya viongozi wakuu wa chama hicho kuwashawishi vijana kuchukuwa fomu hizo, ili kuomba uongozi katika ngazi za CCM.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 3 katika "Fomu za kugombea uongozi wa CCM zadoda Zanzibar ~ vijana wazisusa"

 1. Kamshuu 01/05/2017 kwa 5:22 um ·

  Duuuu
  Duuuu!!!
  Duuuuuu!!!!
  Duuuuu!!!!!!
  Duuuu!!!!
  Tunapata aibu sasa tufanye ss tutachukuwa watu kutoka bara
  Natutafanya kama wanaushi hapa basi ndio ivo

 2. abuu7 01/05/2017 kwa 6:02 um ·

  Sababu si wingi wa watu.si mseme tu hamna barka.kwa uchafu mnao fanya

 3. Jino kwa Jino 02/05/2017 kwa 4:52 mu ·

  Huyu sheni chizi nini ? Anakufuru kwa kusema watu wanazaliana ovyo hiyo si moja wapo wa neema ktk nchi .SMZ mmeshindwa kuwapatia wananchi kazi kwa roho zenu mbaya mmeshindwa kuona mbali kazi ni kazi tu lazima ziwe za serikali mashamba yamejaa tele na duniani inahitajia vitu vingi pamoja na mboga mboga ambazo ni organic .Muusimu wa maembe watu wanaytupa muusimu wa tungule zinatupwa kila muusimu wa neema yyote vitu havina soko serkali hamsadii kitu mkulima watu wanajiajiri wenyewe lkn mapato zero sasa vipi nchi itakwenda vipi watu watanufaika na kilimo serikali imebana kila kitu halafu unasema serikali haina kazi .Munatakiwa kuweka roho zenu mbovu pembeni na kuweka maslahi ya mwana nchi bila kujali chama ,gani anatoka munatakiwa muweke soko la Kimataifa watu watakuja ulimwengu mzima kuja kununua mazao yenu.Kuweni na akili.

Comments are now closed for this article.