DR. SHENI MUNGU ANAKUONA KAMA ZANZIBAR HAIKUPATA UHURU KARUME ALIKWENDA LANCASTER HOUSE LONDON NA UJUMBE WAKE KUFANYA NINI?

Written by  //  11/01/2017  //  Habari  //  Maoni 8

AIBU tena kubwa sana kwa msomi wa PhD kusema kuwa Zanzibar, haikupata uhuru. Mambo mengine ni unafiki na hulka za kishenzi hata kuyasema ni vichekesho na vioja.

Kiongozi kama huyu, ni hatari sana, akiambiwa na watu akina Kikwete na Magufuli kuwa atakuwa Rais wa Zanzibar kwa maisha yake yote (milele) lakini, akubali kuwa kafiri yaani aachane na uislamu, naamini yuko tayari.

Haiwezekani kuwa anajinasibu kuwa ni mzanzibari, tena msomi wa PhD na kwa umri wake naamini anafahamu vizuri tarehe ambayo Zanzibar, ilipopata uhuru wake, leo akaweza kuukana hadharani. Wote ni utamu wa madaraka jamani!!.mmh lazima tujiulize au kashakuwa chizi?.

Akiulizwa na akipewa picha ya Karume (Abeid Amani), Rais wa ‘Afro Shirazi Party’ akiwa katika mkutono wa London, (Lancaster House). Huu ulikuwa mkutano wa kuipa Zanzibar uhuru wake. Hivyo, Karume alikwenda ‘Lancaster House’ na timu yake kufanya nini?.

Hassan Nassor Moyo (Mzee Moyo),’ bado yuko hai na timamu wa akili’ maisha yake yote yuko katika Afro Shirazi na katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, aulizwe, atasema kwamba Zanzibar, ilipata uhuru au haikupata uhuru?.

Mbali na Mzee Moyo, na watu wengine wengi wapo hai bado, waulizwe, wanajuwa ukweli zaidi kuhusu hoja ya uhuru wa Zanzibar.

Asiachiwe huyu mnafiki (chambilicho watu: KINYAGO CHA MPAPURE), huyu rais gani anayepotosha watu kwa jambo ambalo lilitokea na Wazanzibari wanajuwa na dunia yote inajuwa.

Vitabu vya historia vipo na katika mitandao, nenda kwenye GOOGLE, ukipiga tu uhuru wa Zanzibar, umeelezwa A-Z. Google tabaan (mwiko) kuwa na taarifa za uongo.

Anatokea mnafiki anapotosha watu. Ati huyo ni kiongozi wa nchi. Kiongozi gani wa nchi anayefanya hivyo?. Kwa nini anapotosha watu au ni ile dhuluma ya uchaguzi wa Machi 20, inamtesa.

Hivyo, kweli yeye peke yake ndiyo hajui kuwa Zanzibar, ilipata uhuru…basi usomi wake umepigwa na laana na wala hafai hata kuwa rais wa kuongoza hata kuku, achilia mbali kuongoza watu.

Hakuna jambo baya kama dhuluma mwishowe unaangukia kupotosha watu na kuwapotosha watoto wadogo waliyoko maskulini katika masoma. Shein na Mapuri wote kapu moja kwa upotoshaji. Hatari sana watu wa aina hii.

NASHAURI: Watu waliyekaribu naye ‘huyu msomi mjinga’ (Shein) wampelekee kile kitabu cha Dr Harith Ghassany – ‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru.’ atajuwa kuwa Zanzibar, ilipata uhuru au la.

Nakumbuka miaka 1980s: Marehemu Aboud Jumbe (Rais wa Zanzibar awamu pili), katika mkutano mmoja wa ndani uliyofanyika katika ukumbi wa ‘Umoja ni Nguvu’, Mkoani alimwambia Bi Ashura Abeid Maftaha (Mwenyekiti wa UWT – Mkoa wa Kusini Pemba)

Nanukuu: “Kunyamaza kimya ni ustaraabu mkubwa…kuliko kusema kitu unachokijuwa ukapotosha watu kwa kukibadilisha ukweli wake, au kusema kitu ilhali hukijui, ukajifanya unakijuwa…wanaojuwa watakudharau na kukucheka na wasiyojuwa wataendelea kuwasimulia wenzao ujinga na hiyo ndiyo hatari.”

Mzee Aboud Jumbe, muda wote aliyokuwa kiongozi wa Zanzibar, sikuwahi kumsikia kukanusha kusema kuwa Zanzibar, haikupata uhuru.

Na sijui kama angesema Zanzibar, haikuwahi kupata uhuru, engeonekana vipi mbele ya macho ya Wazanzibari;
Hata waliyokuja baadaye akina Ali Hassan Mwinyi, Maalim Idriss, Dk Salmin (Komando) na Amani Karume (Junior), sikuwahi kuwasikia kusema kwamba Zanzibar, haikupata uhuru. Isipokuwa huyu ‘Kinyago cha Mpapure.’

Tunaweza tukasema japo walikuwa hawalitaji neno hilo la uhuru wa Zanzibar au hawakupenda kulitaja, lakini walijaribu kunyamaza kimya. Hawakuthubutu kusimama juu ya jukwaa la mkutano wa hadhara, wakaukana.

Lakini, Shein anawapotosha wanafunzi na wazee (ati jamaa zake wa kwao, Mkanyageni) “Zanzibar, haikuapata uhuru na uhuru wa Zanzibar ni mapinduzi ya Januari 12, 1964. Lugha ya kinafiki, iliyojaa ujinga na upotoshaji isiyo stahiki kusemwa kwa mtu aina ya Shein.

Wallahi naapa kwamba, iko siku Dunia itamsuta na kumuhukumu…atadhalilika kutokana na matamshi yake. Dunia uwanja wa fujo. Uhuru wa Zanzibar, Karume wa ASP, alishiriki kuudai, anakuja mtu anasema Zanzibar, haikupata uhuru wake!! ALLAHU AKBARU..

Chanzo : Rushdy Ahmed

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 8 katika "DR. SHENI MUNGU ANAKUONA KAMA ZANZIBAR HAIKUPATA UHURU KARUME ALIKWENDA LANCASTER HOUSE LONDON NA UJUMBE WAKE KUFANYA NINI?"

 1. salali 11/01/2017 kwa 10:43 um ·

  Walishasema hawana uchungu na dini ya kislam, wanauchungu na ccm hapo, hapo ndio mwenye akili wataujuwa kwamba ccm ni mahaini ndio sababu ya wawo kufurahiya mauwaji.

 2. sadimba 12/01/2017 kwa 11:45 mu ·

  Jamaa keshasema mungu anamtambua kwahiyo kumtajia mungu kwake ni sawa na kupiga konzi kinyago au kwenda kwenye mzimu wao wa kisiwa ndui na kummuliza karume marikiti iko wapi atakuonesha ya darajani lakini hana habari kuna nyengine za mwanakwerekwe na shimoni.

 3. Papax 12/01/2017 kwa 1:01 um ·

  Uhuru kamili ni mapinduzi matukufu ya64, ule uhuru bandia aliope muhamad shamte sisi waafrika tulio wengi visiwana hatutambui kwahio alichokisema shen uhakika na ndivyoilivyo

 4. mzeekondo 12/01/2017 kwa 5:25 um ·

  Tatizo kwani liko wapi? hata imekuwa lazima tukumbushane tarehe ovyo kama sote tuna msimamo mmoja,ni wazi tarehe ni mbili na hizo zote tulisomeshwa skuli katika lile somo la siasa.

  UHURU ulipatikana kwanza, decemba 10-1963 nafikiri kama si kosei na viongozi wake tunawajua wote,Karume hakuwemo katika hiyo serekali.

  MAPINDUZI yalifanywa january 12,1964 kuiondoa serekali iliyokuwepo baada ya kupewa uhuru huo, nilioutaja hapo juu,na kiongozi wa serekali hii akawa Karume, na aliye ongoza mapinduzi ni Okello,mganda wa kabila la acholi ambae baadae alifukuzwa Zanzibar na kurudi kwao.

  Sasa mnazozana nini?

  Kama desturi ya watu wenye akili timamu duniani hatuwezi sote kukubaliana serekali ipi inatufaa sote,wengine watakubali na kuona UHURU wa 1963, ndio mfumo sahihi wa serekali iliyopaswa kuongoza visiwa hivi.

  Wengine wataona na kukubali kuwa MAPINDUZI ya 1964,ndio matukufu na yanayo paswa kuendelea kutawala visiwa hivi kwa miaka mingine 100 ikibidi,huwezi kuwa lazimisha wananchi wote wa visiwa hivi kuwa na msimamo mmoja kuhusu mfumo upi unawafaa wote, na hakuna haja ya kuutaja uhuru au mapinduz,i kwa kuwa wewe,sisi au nyinyi, hamyatambui au kuukubali mfumo mmoja wapo kati ya hii miwili iliyoleta mageuzi ya kisiasa hapa visiwani kwetu.

  Hata hivi sasa katika mfumo huu tulio nao wa vyama vingi vya siasa,bado kuna watu wanaona bora turudi kwenye mfumo wa chama kimoja cha siasa,kwa sababu hawaoni faida ya vyama vingi, ikiwa sisi wenyewe bado tunatumia vifaa vyote vya mfumo wa chama kimoja, katika kutawala,kukandamiza na kuwahadaa watu bure,hivi vipigo na maafa ya wakati wa kila uchaguzi vya nini?

  Taifa lolote ulimwenguni lina historia yake,iwe mbaya, nzuri au imechanganyika, hiyo huwa ni historia huwezi kuzifuta tarehe muhimu za historia ya nchi yako, kwa kuwa wewe hukufaidika,huipendi au rangi yako haikuruhusu kuitambua historia hiyo,rangi, kabila au dini yako haikufanyi wewe uiandike upya historia ili ifanane na asili yako.

  Historia ina wajibu wa kutufundisha na kutuonyesha wapi tulikosea,na wapi tulikuwa juu ya mstari, na ni wajibu wetu kuitumia vema ili ituongoze kwenye maelewano, na sio mitafarakano isiyo kwisha, ya kulumbana tarehe peke yake kama majuha kalulu.

  Hajakatazwa mtu kuyasifu,kuyaabudu au kuyapigia debe Mapinduzi,hata kama hayajamsaidia kitu, hiyo ni haki yake, sisi kama nchi huru tunao uwezo, haki na uhuru wa kumpenda chongo tukamuita kengeza,vile vile msiwakataze watu kuusifu uhuru wa visiwa vyao uliopatikana kisheria, hata kama haukudumu hata miezi miwili,kwa maana hiyo hawakuwahi kujua faida au hasara ambayo ingelipatikana kama uhuru huo ungelidumu zaidi ya miaka hamsini kama yalivyodumu haya Mapinduzi.

  Sisi wananchi wa visiwa hivi inasemekana tuko huru,baada ya mapinduzi, sasa tunaogopa nini kusomesha jamii hasa kizazi kipya, historia yetu kama ilivyo, badala yake tunaanza kulazimishana uhalali wa Mapinduzi na uharamia wa Uhuru, kwa nini hatuwaachii wenyewe wahusika kutumia vichwa vyao kupima na kuamini wanachotaka?

  Udikteta uko wa aina tele,sio lazima uwe rais ndio uwe na uwezo au mawazo ya kaumu hii,sisi tunao lumbana hapa na kulazimishana kuamini unachoamini wewe, au ninacho kipenda mimi, hii ni moja wapo ya udikteta uliotuvaa bila kujijua,tuvifungue vichwa vyetu, viwe wazi na kuyakaribisha maoni tofauti ya watu bila hofu au miiko ya kisiasa.

  Mimi naaamini Uhuru ulipatikana na nakubali Mapinduzi yalifanyika, sasa nani mzuri kati ya hawa wawili, hilo peke yake ndio liko wazi kwa kujadiliwa”open for debate” sio kumkubali mmoja na kumtaa mwingine hawa ndugu hawatengenishwi kwa chuki wala faraja.

  Zanzibar kwanza,vyama na iwe basi.

  • Ghalib 13/01/2017 kwa 5:04 mu ·

   @mzee kondo

   Hapa hatuangalii ipi serikali yenye uhalali wakuongoza baina ya 63 na 64, kinacho angalia ni tukio la kihistoria katika uso wa kimataifa, tukio wa 63 ndio tukio sahihi ambalo la kupewa kipao mbele Zanzibar kama taifa linalo tambulika UN.

   Imagine Palestina hadi leo hawajapata kuwa full member wa un, Jee sisi hatuoni ufahari ¡ mapinduzi tuchukulie kama tukio la kisiasa kwa sababu chama kilichoko madarakani ndio kilicho pindua, hivyo kama vyama vyengine vitakuja kuongoza Zanzibar mapinduzi hakuna atakae sheherekea, lakini uhuru wa Zanzibar wa 63 ndio utakuwa wa kitaifa na mataifa, urasheherekewa tu.

 5. sadimba 13/01/2017 kwa 7:02 mu ·

  @Ghalib.

  mimi kama nimefahamu vizuri mzee kondo ni kwamba haina haja ya kulumbana kwani kwalazimisha akina Mtopea kukubali Zanzibar ni nchi kamlii iliyojipatia uhuru wake ni tabu ni sawa kumpigia mbuzi gita sidhani kama atayawacha majani ni kucheza muziki. Hakuna asiyejua matukia haya mawili na athari zake.

  Uhuru wa Zanzibar kama unavyosema kumbukumbu zipo kimataifa na hazipingiki, ila hakuna jambo baya duniani kama kufadhiliwa na anakufadhili ni bwana wako. Kwahiyo wanaoukana uhuru wa Zanzibar ni kumfurahisha bwana aliyemuweka kwa mtutu wa bunduki japo wanajidai wamechaguliwa demokrasia. Na kwahakika wazanzibar wanajua thamani ya nchi ila wale ambao waliokuja kwa mwenge na soksi wakavuliwa hapa leo ndio wamekuwa wanaukana uzanzibar na uhuru wake kwa nguvu zote.

  Mapinduzi yalifanyika na haya yalifanywa na bara chini ya nyerere na mpaka leo wameendelea zanzibar kuitawala kimabavu na kuuwa wazanzibar ili wawaweke vibaraka wao, mapinduzi ni kuwauwa wazanzibar na kupeleka madaraka ya zanzibar kwa Tanganyika. Na wanaosema himaya ya wazanzibar asilimia kubwa ni wakustaarabishwa na kujifanya ndio wenyewe. Mapinduzi kama ni kupata serikali kwanini wanaendelea mpaka leo. Tumrejee Lukuvi na samweli sita bin Saba pamoja na baba yao nyerere utapata picha kuwa mapinduzi ni mauwaji kwa wazanzibar. Mauwaji ya halaiki yaliyoratibiwa na nyerere ndio leo tunasherehekea kwa mungu weshajikubalisha anawatambua. Miezi mitatu tu wakajidai kufanya muungano na ndio leo ndio kisingizio chao cha kufanya wanayofanya.

  Hao wanaoikandamiza zanzibar wanajua fika wenyewe hawataki, lakini tukikaribia kuigeuza zanzibar kuwa Dubai. Ila wengi hawakufahamu Dubai ya zama zipi kama ni za zamani tutafika muda si mrefu, Darajani, kijagwani na jumba la treni linatuonesha mafanikio ya safari yetu, sikwambii kusaka ng’ombe wa wanyonge.

 6. MAWENI 13/01/2017 kwa 11:30 mu ·

  Hayo ” mapinduzi” ( mavamizi) .Ndio ilofanya Zanzibar miaka 53 kuendelea kuwa koloni la Tannganika kwa wisayay nchi za kibeberu. Walio zoweya kuwa nchini nidhamu za kikoloni ndio hao wanaona hayo mavamizi ndio uhuru. Kusalimisha mamlaka ya nchi yao yote kwa kikundi cha watu wa nchi nyengine.
  Kwa maneno ya mwana Sheriya- Othman Masoud. ( Znzibar imekuwa kama Mwana mume alie tolewa udume wake) Ati huwo ndio Uhuru. Hata chama cha mpira ulimwenguni hamruhusiwi kungiya na bwana wa tawala wa koloni wa Tanganyika.

 7. Papax 14/01/2017 kwa 2:04 um ·

  @Maweni
  Usikufuru bali ushukuru mapinduzi matukufu ndio yalio wakomboa wengi hata hawa hizibu mavi, wamepata maeneo mingi hapa unguja wanaishi bila ya kulipa kodi kutka kwa mabwana zao mimanga

Comments are now closed for this article.