Dr Shein – Tumezipokea Salam za Mwaka Mpya, Jee vipi Wafanyakazi wako

Written by  //  01/01/2013  //  Habari  //  4 Comments

Kheri ya Mwaka Mpya.

 Kama ilivyokawaida ifikapo tarehe kama hii ya leo, viongozi kadhaa dunia hutoa salamu na wengine hufikia kujitathmini kile walichofanya kwa muda wa siku 365.

Nasi Zanzibar, kama nchi, Rais wetu naye ametowa salam zake za mwaka mpya. Salam zake zimejiegesha zaidi kwa wananchi kuwaasa na kuwanasihi kuenzi sheria za nchi. Ni nasaha nzuri kwani bila ya sheria nchi itakuwa mkorogo.

Nilichojiuliza kuenzi sheria ni kwa wananchi tu, vipi wafanyakazi wa serikali, watendaji wake na yeye mwenye Mh Rais ataenzi sheria hizi.

Pasopo shaka watendaji wake, viongozi wake, na yeye mwenyewe amekuwa mkengeukaji wa sheria. Uteuzi wake wa watendaji wasiokuwa na maadili huku ndivyo Mh Rais anavyokengeuka sheria. Kumteuwa kiongozi au mtendaji mwenye shutuma na ushahidi wa wizi au ubadhirifu wa mali ya umma, huko ni kuvunja sheria. Vipi Dr Shein umlinde na umtetee mtu aliyethibitishwa kwamba kaiba mamilioni ya fedha za umma, uepukike na hukumu ya uvunjaji sheria.

Mh Rais, mwana hufuata kisogo cha mleziwe. Ili wananchi wako wawe watiifu juu sheria, hakuna budi na nyinyi wazee kuonyesha mfano. Hapo ndio utakuwa na nguvu za kuwakanya, kinyume chake watakujibu ufedhulu uone umevunjiwa heshma. Tunatarajia mwaka 2013, Mh Rais, hutowalinda wale wote watakaotajwa kwenye ubadhirifu wa mali ya umma, sio wananchi peke yao.

Mh Rais, kuhusu suala la kulinda miundo mbinu ni sawa kuwaasa wananchi wailinde. Mh Rais ubaya umeanza kwenu wakubwa kushindwa kuilinda miundo mbinu hii. Kwanza mamilioni ya fedha watendaji wako wamezila, pili, huo uwekaji wake ni wa “kufyatua”. Unajuwa fika barabara ya Chake-Wete imo kwenye mpango wa kutanuliwa, vipi unauweka fibre mita mbili kutoka kwenye barabara. Ndio niliposema Mh Rais mungeanza nyinyi kuonyesha mfano wa kulinda rasilimali zetu.

Mh Rais, kumbuka kauli yako kwamba Mgao wa umeme utamalizika mwezi wa December 2012. Leo ni January 1 2013 bado tunaendelea kupata mgao wa umeme. Jee tukikwita “muungo” utajisikia vipi, umevunjiwa heshma. Tunataka kauli zifuate vitendo. Usemacho kiwe ndicho, ikiwa kuna mtu anakudanganya mseme hadharani kisha muondoshe. Vipi uweke watu wanaokupotosha?

Mh Rais, nasikia kuna uzinduzi wa e-governance, jee huo umradi umekamilika? Mh Rais unadanganywa mchana kama vile unayeuziwa paka pakachani. Nakupa mwaka mzima tuone e-governance tuone kama itafanya kazi.

About the Author

View all posts by

4 Comments on "Dr Shein – Tumezipokea Salam za Mwaka Mpya, Jee vipi Wafanyakazi wako"

  1. mwanafunzi 01/01/2013 at 7:22 mu ·

    Heko mtoa mada naona umemaliza kila kitu. Iwapo viongozi watakuwa mfano wananchi hatuna matatizo lakini wao viongozi ndio wanaoanzisha migogoro kwa maslahi yao wenyewe halafu wakawatafuta watu fulani wakawabambikizia kesi za uongo.

    Nawatizame uongozi wa kiongozi wa kiislamu Omar bin Khatwaab jinsi alivyokuwa akisimamia utawala wa sheria.

    Sio muda mrefu atachagua tume ya uchaguzi tusubiri tuone hao watu tutakaoletewa tunaweza tukapatwa na mshangao sote.

  2. Makame Ame 01/01/2013 at 8:28 mu ·

    Nafikiri Raisi ilikuwa kwake ni kututaka tuzidi tuwe wastahmilivu kwa vyombo vyake vya Dola vinavyotuonea kama vile walivyofanya ndugu zetu wa Kendwa.

    Kwa kweli salamu zake tuzisome kinyumenyume na hivyo tutafahamu nini anakusudia. hawa watu wenye ‘doctorate’ wana mambo saa nyengine, wanatuona sooote sisi wengine mazuzu, mabwege na mbumbumbu hatujui kitu mzungu wa reli na hatufahamu wanayoyakusudia.

    Salamu zimefika Mh Rais.

  3. buhanan 01/01/2013 at 10:28 mu ·

    Happy new year Wazalendo nyote pamoja na Uongozi Mzima wa MZALENDO ,Mtoa mada na muandishi nakupeni pongezi .Dr Shein tumezipokeya na ww pokeya zetu kwanza tunakuomba utupie jicho lako ktk humu mzalendo ndio utajuwa what is going on na utajuwa Wazanzibari wanataka nini na wanasema nini sasa salamu ni kuwa jana tulikuwa 2012 leo ni 2013 kama siku zinavyokwenda na ndio hivo hivo Uraisi wako ndivyo unavyokwenda weye pamoja na kundi lako ,Salamu zetu ni kuwa Hatutaki Muungano wa aina yyote na tunakuomba Uwaachiye viongozi wa Uamsho mara moja ,hayo mengine yatafuatia baadaye kama tutakua hai .

  4. makame silima 01/01/2013 at 12:22 um ·

    Salamu za Shein ni hizi za kuligumbatia Kanisa Katoliki na Kuwaweka ndani Ma-Sheikhe wetu kwa choko choko za Kanisa kuona tu kuwa Sauti ya Mashekhe zidi ya Kanisa na Serekali ime imekuwa haina nguvu.

    Wamesahau kuwa Zanzibar wakazi wake ni mojority waislamu na ni %99 lakini Nguvu ya Kanisa %0 ndio viongozi wako nayo sambaba.

    Kusema Kanisa na Smz eti Zanzibar kuna udini, Hii nibabaisha Bwege ya Kutaka kutufunika Kanisa na wingi wetu tulionao na kutaka kujifanya wao wapo lakini wanatengwa.

    Kwa hali ya milango ilivyo wazi ya ingia toka na mfumo Kristo unavyo ingizwa Zanzibar kecho na kechokutwa tutambiwa Wakristo na Waislamu Zanzibar ni nusu kwa nusu kwa hio na wao watengewe sehemu maalum katika Baraza la wawakilishi.

    http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/377691-zanzibar-sasa-hali-ni-tete.html#post5355505

Comments are now closed for this article.