Dr Shein hakuna wa kumuondoa madarakani

Written by  //  19/03/2017  //  Habari  //  Maoni 8

5bf0Ali-Mohamed-Shein

Na Haji Mtumwa

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein ametua kisiwani Pemba na kuwataka wananchi kufanya kazi, huku akisisitiza hakuna atakayemuondoa madarakani.

Dk Shein amesema hayo ikiwa takriban siku 30 tangu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad afike na kuzungumza na wananchi akiwahakikishia kuwa, ‘haki yao wataipata hivi karibuni’.

Rais Shein ametoa kauli hiyo akiwa katika Sekondari ya Fidel Castro iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba alikokwenda kwa ajili ya kugawa vifaa vya michezo kwa maandalizi ya ligi ya mpira wa miguu kwa timu 18 za kisiwani humo.

Timu hizo zitashindana kusherehekea mwaka mmoja tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Zanzibar katika awamu ya pili na kusherehekea miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM.

Dk Shein amewataka wananchi kuepuka maneno ya kizushi kuwa kuna Serikali itakuja kuiondoa madarakani anayoiongoza.

Amesema katika siku za karibuni hakutakuwa na uchaguzi mwingine mpaka mwaka 2020 ambao pia chama anachokiongoza anaamini kitashinda na kuendelea kushika dola.

Katika ziara hiyo pia ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdalla Juma Abdalla ‘Mabodi’ aliyetumia fursa huyo kutoa shukrani kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo mjini Dodoma hivi karibuni

Mwananchi

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 8 katika "Dr Shein hakuna wa kumuondoa madarakani"

 1. Jino kwa Jino 19/03/2017 kwa 7:44 mu ·

  MwenyeziMungu (ALLAH subhanahu wataala ) Ndie atakaekutoa Madarakani kwa njia yyote aipendayo yeye ikiwa yy ndio aliekuweka basi yy ndie atakaekutowa .Hata Firauna alisema yy ni Mungu lkn ulipokuja ukweli alikuwa kama mavi tu kwa hivyo na weye jitaarishe na mtihani uliokuwa nao utapokutia mikononi kwa mwenye nguvu utajitambua .Wamepita wengi kama weye au mfano wako weyee na sasa hawapo tena na kama wapo basi wanauona ukweli wa mambo .sisi ni Waislamu tunaamini hayo juzi na jana hukuwa lolote si chochote kwa hivyo endelea tu lkn dhulma haidumuuuu.

 2. zamko 19/03/2017 kwa 8:43 mu ·

  @ CCM
  Kwanini Muwashirikishe Wanafunzi katika Sherehe za Serikali Haramu Au Ndio Munataka kutafuta Sanbabu kama zile za Salmini Amour Muwafukuze Wanafunzi hao Mashuleni?

  Hivo kama CCM inapendwa kweli kwanini inalazimisha mambo?

  Kuhusu Sherehe mimi ningewaomba Watu Wote wagome, Munawaibia Wananchi Haki yao .
  Munawafukuza Makazini na Kuwafelisha katika mfumo Mbovu wa Elimu.
  Munawanyima mishahara na haki ao za Kiraia.
  Ikesha munawaaambia Waje washerehekee Haramu kwa Nguvu na kama hawakuhudhuria Mutawafukuza Shule.

  kweli huu Ndio Msingi Mzima wa Kiongozi tena Muislamu tena (Ati) Al Hajj?

  @ Jino Kwa Jino.

  Naamini Dr Sheni huna nguvu za Kumshinda Allah SW. Na Hakika kama Uraisi Ni Haki Yako Bac Utakaa Maisha Hapo Na Uozee Hapo hapo.

  Laa Kama Uraisi sio HAKI yako Basi Naamini ALLAH NDIE Muondoaji Wa Hapo Alipokuweka Tena Hakuna Atakae sema kwii.

  Allahuma Kyaifa Anna -Sua, Alaa Zannjibar
  Bimaa-shitta -wakkaiffa Shitta , In-naka- Allah- Man-ntashau Qadir.

 3. zamko 19/03/2017 kwa 8:45 mu ·

  @ Tambaa Shuweni Tambaa,
  Hakika Aliekupa Wewe Kiti na Dola Ndie huyo huyo alietupa Sie Kumbi.

  Hakika Allah Hahafiliki na Duwa za Watu Wenye kudhulumiwa.
  Allah atakuondoa Hapo tena katika Idhara kubwa Inshallah
  Allahumma Amiin

 4. sadimba 19/03/2017 kwa 10:54 mu ·

  Hata uyo uliyesema anakutambuwa hana uwezo?

 5. abuu7 19/03/2017 kwa 12:01 um ·

  Mipira ya nini.wakati deni la umeme hamjalipa.wewe komba vishavu munatanuliya na kuendasha chama chenu cha kikafiri .kwa pesa za wananchi.
  Hutakiwi pemba hata kuonekana.nuksi wewe

 6. Calif 19/03/2017 kwa 12:56 um ·

  Tamba utambae mkuu pumzi tu najua zitaisha tena kwa huzuni na masikitiko na mbaya zaid utakua tayar mbele ya Allah (SW) na dhulma ya karibu watu milion moja na nusu (1,5000,000) ya wazanzibar watoto na watu wazima na CCM pia maana na wao wanadhulumiwa lkn hawajui au wanajipumbaza.

 7. Piga nikupige 19/03/2017 kwa 7:25 um ·

  Sheni usiwe na wasiwasi atakae kuondoa hapo ni Allah (S.W)

  Juzi nilicheka sana eti Vuai Ali Vuai anatowa Mawaidha wakati aki mkabidhi ofisi dhalimu mwenzake, aliwaomba msamaha CCM wenzake lakini sijui atawaomba msamaha Wazanzibari alio wadhulumu au ana uwezo wa kwenda kuwalipa kesho mbele ya haki? Mimi nijuavyo Vuai ameshiriki katika dhulma dhidi ya Wazanzibari kwa muda mrefu, basi sijui Bavuai utalichukuliaje hili jambo maana safari ni ndefu na wewe umebeba haki za watu na husamehewi abadani. Tambua una zigo umelibeba zigo ambalo huna salama ukataka usitake lazima urejeshe haki za watu vyenginevyo tutakutana Mkunazini.

 8. salali 20/03/2017 kwa 9:10 um ·

  Ukikubali ukikataa haki ya wenye kudhulumiwa M/Mungu hiilipa na sisi bado hatuja kata tamaa,wewe jitekenye na uwatekenye haini wenzako deni unalo hilo bakiroro.

Comments are now closed for this article.