Dr Shein acha kuwadanganya Wazanzibar

Written by  //  10/01/2017  //  Habari  //  Maoni 7

Na Rushdy Ahmed

AIBU tena kubwa sana kwa msomi wa PhD kusema kuwa Zanzibar, haikupata uhuru. Mambo mengine ni unafiki na hulka za kishenzi hata kuyasema ni vichekesho na vioja.

Kiongozi kama huyu, ni hatari sana, akiambiwa na watu akina Kikwete na Magufuli kuwa atakuwa Rais wa Zanzibar kwa maisha yake yote (milele) lakini, akubali kuwa kafiri yaani aachane na uislamu, naamini yuko tayari.

Haiwezekani kuwa anajinasibu kuwa ni mzanzibari, tena msomi wa PhD na kwa umri wake naamini anafahamu vizuri tarehe ambayo Zanzibar, ilipopata uhuru wake, leo akaweza kuukana hadharani. Wote ni utamu wa madaraka jamani!!.mmh lazima tujiulize au kashakuwa chizi?.

Akiulizwa na akipewa picha ya Karume (Abeid Amani), Rais wa ‘Afro Shirazi Party’ akiwa katika mkutono wa London, (Lancaster House). Huu ulikuwa mkutano wa kuipa Zanzibar uhuru wake. Hivyo, Karume alikwenda ‘Lancaster House’ na timu yake kufanya nini?.

Hassan Nassor Moyo (Mzee Moyo),’ bado yuko hai na timamu wa akili’ maisha yake yote yuko katika Afro Shirazi na katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, aulizwe, atasema kwamba Zanzibar, ilipata uhuru au haikupata uhuru?.

Mbali na Mzee Moyo, na watu wengine wengi wapo hai bado, waulizwe, wanajuwa ukweli zaidi kuhusu hoja ya uhuru wa Zanzibar.

Asiachiwe huyu mnafiki (chambilicho watu: KINYAGO CHA MPAPURE), huyu rais gani anayepotosha watu kwa jambo ambalo lilitokea na Wazanzibari wanajuwa na dunia yote inajuwa.

Vitabu vya historia vipo na katika mitandao, nenda kwenye GOOGLE, ukipiga tu uhuru wa Zanzibar, umeelezwa A-Z. Google tabaan (mwiko) kuwa na taarifa za uongo.

Anatokea mnafiki anapotosha watu. Ati huyo ni kiongozi wa nchi. Kiongozi gani wa nchi anayefanya hivyo?. Kwa nini anapotosha watu au ni ile dhuluma ya uchaguzi wa Machi 20, inamtesa.

Hivyo, kweli yeye peke yake ndiyo hajui kuwa Zanzibar, ilipata uhuru…basi usomi wake umepigwa na laana na wala hafai hata kuwa rais wa kuongoza hata kuku, achilia mbali kuongoza watu.

Hakuna jambo baya kama dhuluma mwishowe unaangukia kupotosha watu na kuwapotosha watoto wadogo waliyoko maskulini katika masoma. Shein na Mapuri wote kapu moja kwa upotoshaji. Hatari sana watu wa aina hii.

NASHAURI: Watu waliyekaribu naye ‘huyu msomi mjinga’ (Shein) wampelekee kile kitabu cha Dr Harith Ghassany – ‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru.’ atajuwa kuwa Zanzibar, ilipata uhuru au la.

Nakumbuka miaka 1980s: Marehemu Aboud Jumbe (Rais wa Zanzibar awamu pili), katika mkutano mmoja wa ndani uliyofanyika katika ukumbi wa ‘Umoja ni Nguvu’, Mkoani alimwambia Bi Ashura Abeid Maftaha (Mwenyekiti wa UWT – Mkoa wa Kusini Pemba)

Nanukuu: “Kunyamaza kimya ni ustaraabu mkubwa…kuliko kusema kitu unachokijuwa ukapotosha watu kwa kukibadilisha ukweli wake, au kusema kitu ilhali hukijui, ukajifanya unakijuwa…wanaojuwa watakudharau na kukucheka na wasiyojuwa wataendelea kuwasimulia wenzao ujinga na hiyo ndiyo hatari.”

Mzee Aboud Jumbe, muda wote aliyokuwa kiongozi wa Zanzibar, sikuwahi kumsikia kukanusha kusema kuwa Zanzibar, haikupata uhuru.

Na sijui kama angesema Zanzibar, haikuwahi kupata uhuru, engeonekana vipi mbele ya macho ya Wazanzibari;
Hata waliyokuja baadaye akina Ali Hassan Mwinyi, Maalim Idriss, Dk Salmin (Komando) na Amani Karume (Junior), sikuwahi kuwasikia kusema kwamba Zanzibar, haikupata uhuru. Isipokuwa huyu ‘Kinyago cha Mpapure.’

Tunaweza tukasema japo walikuwa hawalitaji neno hilo la uhuru wa Zanzibar au hawakupenda kulitaja, lakini walijaribu kunyamaza kimya. Hawakuthubutu kusimama juu ya jukwaa la mkutano wa hadhara, wakaukana.

Lakini, Shein anawapotosha wanafunzi na wazee (ati jamaa zake wa kwao, Mkanyageni) “Zanzibar, haikuapata uhuru na uhuru wa Zanzibar ni mapinduzi ya Januari 12, 1964. Lugha ya kinafiki, iliyojaa ujinga na upotoshaji isiyo stahiki kusemwa kwa mtu aina ya Shein.

Wallahi naapa kwamba, iko siku Dunia itamsuta na kumuhukumu…atadhalilika kutokana na matamshi yake. Dunia uwanja wa fujo. Uhuru wa Zanzibar, Karume wa ASP, alishiriki kuudai, anakuja mtu anasema Zanzibar, haikupata uhuru wake!! ALLAHU AKBARU..

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 7 katika "Dr Shein acha kuwadanganya Wazanzibar"

 1. Ashakh (Kiongozi) 10/01/2017 kwa 8:26 mu ·

  Ingawa nilikuwa sijazaliwa laikin i sikatai kuwa Mapinduzi hayakufanyika. Na vilevile n akubali kuwa kulikuwa na uhuru ulitolewa.

  Iweje leo upande mwengine hautaki kukubali kuwa uhuru ilitolewa kisha ukapindua?

 2. Fahur 10/01/2017 kwa 10:40 mu ·

  Ni kichaa huyu Babu anaonekana anauza Taifa la Zanzibar kwa Tanganyika kwa bei ya Jumla , vilevile namtaka huyo Mwehu asiyejitambua aseme Mwaka huo wa 1964 ZNZ ilikuwa chini mkoloni gani?? Au ni ilikuwa koloni la nchi gani?nitamtukana huyo alaa!!! Sipendi unaaa?

 3. MAWENI 10/01/2017 kwa 10:23 um ·

  Hiyo ndio cardinal principle ya ccm kujidanganya wao wenyewe .
  Wamepitwa nawakati ulimwengu wa leo . Information yafikiwa kwa ncha za vidole.
  Ile nadhariya ya properganda oficer wa Hitler ( Paul Joseph Goebbels) ; ya kusisitiza kusema uwongo mpaka uwonekane kuwa ni kweli; si kwa ulimwegu huu wa leo. Sheni si mdogo kuwa hakusikiya au kuona hayo ya Uhuru wa Zanzibar 1963. Ajuwe tu kuwa uwongozi wa ASP ulikuwapo hapo Viwanja vya coopers (Golf course) sasa Maisara Serikali ya kikoloni ya kingereza ilipo kabidhi dola Ya Zazibar mamlaka yake kamili 10th dec. 1963. Uhuru ulotambuliwa na nchi zote za Afrika Mashariki ikiwamo Tanganyika. Nchi zote za Afrika na Ulimwegu mzima. Kilele cha hayo nipale Zanzibar ilpo kubaliwa kuwa mwana chama rasmi wa UN 13 dec. 1963.
  Pendera ya Dola huru ya Zanzibar lipandishwa kwenye viwanja vya UN. Kenya vilevile siku hiyohiyo walikubaliwa kwenye umoja huwo. Moja katika wajumbe walio towa khutba kuikaribisha Zanzibar alikuwa muakilishi wa Japan. Ziko picha za wakilishi wa Zanzibar kwenye ukumbi huwo wa UN, audio, na filamu kwenye kumbu kumbu ya Tokeo hilo.
  Mapinduzi ( uvamizi) wa Zanzibar 1964 ; ulosabibisha mauti ya halaiki. Na safishaji ya Wazanzibari wenye asili ambazo wavamizi hawakupenda. Unyangayajiwa mali za watu. Ndio msingi ya kuzaliwa huu ukoloni wa Tanganyika juu ya Zanzibar. Watawala wanaita muungano.
  Siku za kudangayana zime kwisha ulimwegu huu wa leo.
  ZANZIBAR KWANZA !

 4. mohamed 11/01/2017 kwa 12:23 mu ·

  Bangi nuksi kishenzi,hata kinyesi utasema wali kwa mandondo😀

 5. mohamed 11/01/2017 kwa 12:24 mu ·

  Bangi nuksi kishenzi,hata kinyesi utasema wali kwa mandondo. 😀

 6. sadimba 11/01/2017 kwa 11:02 mu ·

  Tusishangae ndio chama kushika hatamu, kwahiyo anavutwa kama ng’ombe kuelekea kule apapo atafurahisha mabwana zake. Na kwakweli ndio falsafa ya kirusi inavyomchemka na kwa upande mwengine anaonesha hama imani na zanzibar kwavile asili yake ni morogoro tutasikia na kuona vitimbi vingi tu. Mabwana wanachukuwa fungu mbaraka anasema sijasikia kama kimechukuliwa kwani ni kifaranga kwamba kikinyakuliwa na kunguru utasikia sauti.

  Sijui kesho atakuja na kejeli gani katika sherehe ya mauwaji wasio na hatia, unapofanya maovu na kujisifu ndio kibri chenyewe na mungu huwapuruzia watu waovu wakajiona wana nguvu kuwadhalilisha wanyonge.

 7. sadimba 11/01/2017 kwa 11:20 mu ·

  Kama huutambui uhuru wa zanzibar abudu mauwaji munayosherehekea.

  https://www.youtube.com/watch?v=NoRgEqtwAks

Comments are now closed for this article.