Dola yashika mpini kuihujumu CUF

Written by  //  10/01/2017  //  Habari  //  Maoni 2

Kila siku ipitayo Mwenyezi-Mungu anadhihirisha njama za dola za kutaka kukivuruga Chama cha Wananchi (CUF) kwa kumuunga mkono kwa njia chafu Bwana yule na genge lake!

Sasa hivi tumegundua hujuma ya ruzuku ya Chama, ambayo Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alizuia kutolewa kwa uongozi wa halali wa CUF, ikiwa imedokolewa, kwa fedha kutoka Hazina ya Serikali Kuu na kuhamishiwa katika Account ya Chama cha CUF, Wilaya ya Temeke. Katibu Mkuu wa CUF hana taarifa, Bodi ya Wadhamini haina taarifa!

Baya zaidi watia saini katika hio accounti ya wilaya ya Temeke walibadilishwa kinyemela, bila bKamati ya Utendaji ya Wilaya kupitisha azimio la kubadili watia saini. Watia saini wapya ni Mhe. Magdalena Sakaya, Bw. Thomas Malima na dada mmoja ambaye bado jina lake halijapatikana. Fedha zilizotolewa Hazina na kuhamishiwa katika accounti ya CUF, Wilaya ya Temeke ni TShs. 369,378,502.64/-.
Uhaulishaji huo ulifanywa tarehe 05/01/2016. Siku ya pili yake, yaani tarehe 06/01/2017, Watia saini hao walitoa Tshs. 69,000,000/- kutoka accounti hio. Siku hio hio TShs. 300,000,000/- ziliondolewa kwenye accounti hio ya CUF, Wilaya ya Temeke na kuhamishiwa kwenye accounti ya mtu binafsi aitwaye Mhina Masoud Omary iliyoka katika Benki ya NMB iliyofunguliwa katika Tawi lake la Handeni, iliyofunguliwa tarehe 22/01/2008.

Tarehe 09/01/2017 Bw. Mhina Masoud Omary alitoa TShs 149,000,000/, Kutoka Tawi la NMB, Kariakoo, Jijini Dar es Salaam!Na baadaye tarehe hio hio, Bw. Mhina Masoud Omary ametoa Tshs. 150,000,000/- kutoka Tawi la NMB, Magomeni, Jijini Dar es Salaam.
Tunajiuliza jee katika kashifa hii Msajili wa Vyama vya Siasa alishirikishwa au la? Ikiwa alishirikishwa naye akakubali ni kwa kiasi gani? Maana sheria iko wazi. Fedha za ruzuku za Vyama vya Siasa zinaingizwa katika accounti maalum ya Ofisi ya Msajili, nayo Ofisi ya Msajili ndio huidhinisha fedha za kila chama zipelekwe katika accounti ya chama husika. Jee, maofisa wa Hazina waliikwepa hatua hii?

Ikiwa waliukwepa utaratibu huo, basi hivyo ndivyo baadhi ya watu wenye dhamana ndivyo wanavyoendesha mambo kwa utashi wao bila kujali sheria, kanuni wala taratibu!

Katika hali kama hio, bado Rais Magufuli anayo kazi kubwa ya kutekeleza kile anachokiita ; “…kuinyoosha nchi…” Kumbe bado yapo majipu mengi yanahitaji kutumbuliwa!

Pamoja na yote hayo,sisi katika CUF tunajua kuwa fedha zetu ambazo Msajili wa Vyama vya Siasa ametuzuilia, bado ziko kamilifu katika Mfuko wa Hazina. Mazonge yetu yakimalizika, Hazina itatafuta pahala pa kuzijalizia ili sisi tupate fedha zetu zote.

Papo hapo huu ni ushahidi mwengine unaothibitisha, bila ya kuwa na chembe ya shaka, kuwa wako maofisa wakubwa katika Serikali wanaomsaidia Bwana Yule kukivuruga Chama chetu. Na ilivyokuwa hio ndio nia yao, kamwe Bwana Yule na wanaomsukuma na kushirikiana naye kwa hali na mali, hawatafanikiwa. Mwenyezi-Mungu yuko nasi!

Fb

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 2 katika "Dola yashika mpini kuihujumu CUF"

 1. Mkandaa 10/01/2017 kwa 2:24 um ·

  Ni taarifa nziru katika wakati muafaka.
  ni busara chama kikaangalia kitakavyoweza kuwawajibisha wahusika wa uharamia huo na kujiweka katika mazingira ya kufahamu hatma yao ya baadae. Washauri na wataalamu mbalimbali ndani ya chama wanapaswa kuchukua hatua muafaka kwa wakati, wasisubiri hadi wakati wa ukaguzi ndio wakategemea watasema hawana taarifa na hizo pesa, itakuwa ni kuhalalisha chama kuchukuliwa hatua yoyote wasioitarajia.
  Ni wakati wa kulijadili hilo suala na kumuandikia wazi Msajili wa Vyama vya siasa na kila ngazi inayohusika na kusimamia sharia zao kwamba chama hakitambui muamala huo.

  Sakata la kujiuzulu kwa Prof. Lipumba na hatua ya kuwavua uanachama kina Sakaya kunadhihirisha wazi kwamba chama hakifanyi maamuzi ya msingi kwa wakati na kuyasimamia. Viongozi wanatakiwa kujifunza na kubadilika wakijua kwamba adui yao ni mkubwa Zaidi ya wanavyofikiria.

 2. Papax 12/01/2017 kwa 1:07 um ·

  Hii ni shitupa tu zidi ya serekali tukufu, ukweli hamuuseme kwanini? maali kaikimbia ofisi buguruni aliko mwenyekiti pr lipumba , anajitenga kufanya kuwa cuf, ni mali yake kwahio marahii mtaisoma namba, mkitaka lipumba ni mwenyekiti wenu mpaka uchaguzi ndani ya chama chenu ufanyike , na sisi tunajua hakuna mgogoro ndani ya cuf, ndio maana serekali inampa ushirikiano

Comments are now closed for this article.