Dk. Shein: Siitambui Kamati ya Maridhiano Zanzibar

Written by  //  08/06/2013  //  Habari  //  Maoni 26

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema haitambui kamati ya maridhiano inayotetea Zanzibar kuwa na mamlaka kamili kama taifa linalojitegemea na kuwa na kiti katika Umoja wa Mataifa.

Dk. Shein alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume baada ya kukamilisha ziara ya kikazi nchini China juzi.

Alisema kwamba haitambui kamati hiyo lakini alikiri kukutana nayo mara tatu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ilikwenda kumpongeza Ikulu baada ya kuibuka na ushindi, mara ya pili walifika kumpa mkono wa pole kufuatia ajali ya meli ya Spice Islanders kabla ya kukutana nao kwa mara ya mwisho.

Alisema shughuli zinazofanywa na kamati hiyo hazina baraka zake na wala hatambui mtu aliyeunda au kuteua kamati hiyo ambayo imekuwa ikifanya kampeni kubwa za Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili na kuwahusisha viongozi wastaafu akiwemo Rais wa Awamu ya Tano, Dk. Salmin Amour Juma ‘Komandoo’ na Rais wa Awamu ya Sita, Dk. Amani Abeid Karume.

“Waulizeni nani aliyeunda kamati hiyo na nani aliyeteua kama wakishindwa nitawaeleza mimi katika mkutano nitakaouitisha kuzungumza na waandishi wa habari, na walipokuja kwangu wanajua nini nilichowaeleza waseme,” alisema Dk. Shein.

Kamati hiyo ambayo ilikuwa ikitetea sera ya Muungano wa mkataba inaundwa na wanachama watatu kutoka CCM na watatu kutoka CUF, ikiongozwa na waziri wa kwanza wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hassan Nassor Moyo(CCM), Makamu Mwenyekiti Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Abubakar Khamis Bakari(CUF), Katibu wake ni Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu(CUF) na wajumbe ni pamoja na Waziri wa zamani wa SMZ na Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki, Mansour Yusuph Himid(CCM) na Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma Salim Bimani(CUF).

Hivi karibuni, kamati hiyo iliandaa mkutano wa hadhara na kutangaza mambo 10 yanayopaswa kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, ikiwa ni siku chache kabla ya Mwenyekiti wa tume ya katiba Jaji Joseph Warioba kuzindua rasimu ya katiba ya awali.

Kutokana na hali hiyo joto la kisiasa na vuguvugu la mabadiliko ya katiba mpya limechukua sura na mitizamo mbalimbali kutoka kwa wanasiasa, wanaharakati na wasomi ambao baadhi yao wamewanyooshea vidole wanasiasa wakiwataka kutoingilia mchakato wa katiba na kuipa nafasi tume ya mabadiliko ya katiba ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia jambo hilo kwa mujibu wa sheria.
CHANZO: NIPASHE

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 26 katika "Dk. Shein: Siitambui Kamati ya Maridhiano Zanzibar"

 1. nuramo 08/06/2013 kwa 12:49 um ·

  Hihihi huyu bwana,mi nataka waznz waandae maandamano kumshindikiza ajiuzulu hasa itakuwa raha sana

  • zinjibar.asli 08/06/2013 kwa 9:46 um ·

   Zanzibar haijawahi kupata raisi jahil na mpumbavu kama dude hili (Shein), huyu kavuka mipaka yote yaani toka alipoapishwa nchi yetu imeingia nuksi na mabalaa kila aina mpaka leo.

   Ati katoka China ziara ya kikazi bloody fool kazi gani labda kwenda kushangaa na kurudi mana hawakilishi nchi na hicho anachokigambia SMZ haitambuliki mahali, kinachojulikana ni Tanzania na yeye ni waziri mdogo tu miongoni mwa mawaziri wa Kikwete.

   Hili jamaa lina akili aina gani lakini???? Ah nlisahau kua matunda ya dhulma ni dhulma tu. Nlisahau kidogo kua jamaa si kiongozi wa wazanzibari bali ni kibaraka cha Dodomaaaaa kimeletwa kuja kutubughudhi and that’s exactly what he’s doing.

 2. Abdul 08/06/2013 kwa 1:18 um ·

  unajuwa maandamana yatapewa jina la chama pinzani ,mimi ninahisi katika kamati ya maridhiano

  amani karume asimame kiririni ahutubie kisha ndio yaandaliwe maandamano ikiwa kamati moyo na

  maalim tu ndio wasemaji juwa hakuna liwalo ilazogo jingi mwisho litasikika kutaka watake wasitake

 3. Abdul 08/06/2013 kwa 1:19 um ·

  ukiona habari ya mwinyi saadala ujuwe ni uzushi umesha pikwa

  • rayun 08/06/2013 kwa 1:23 um ·

   sio uzushi ni habari ya kweli bt muandishi ni kawaida yake kushupalia habari za kizombi zombi kama hizi

 4. rayun 08/06/2013 kwa 1:26 um ·

  mimi nataka kuuliza dr shein ameisikia rasimu ya katiba mpya? nataka kusikia maoni na kauli yake juu ya rasim hii. au ndo mpk waende dom wakapewe maoni ya kuongea mana hawa wenzetu wanakirihisha hawatumii mawazo yao ila yawe yamepata baraka za do….domo

 5. rayun 08/06/2013 kwa 1:28 um ·

  well! said mheshimiwa bt unajchanganya na kupngana na kauli yako, bac naomba nikurekebshe kua labda useme unaitambua lakini haina baraka za chama chako ambayo bado inanifanya niwe na miwe na maswali mengi miongani mwao ni kua kama hawana baraka za chama chako kwa nin msiwawajibishe kichama? kwa nin msiwaonye wakati wankitumia chama chako kinyume na utaratibu wenu.
  viongozi kama nyinyi mkiachiwa mtaendelea kuwachanganya wananchi wenu kwa majibu yenu ya mkato yasofahamika na yenye kukinzana. leo unatwambia kamati imekuja mara 3 ikulu kukupongeza na kukupa pole mara apo apo huitambui wapi tushike mheshimiwa? you are confusicus us!

 6. jimy 08/06/2013 kwa 2:04 um ·

  uwezekano wa kufanyika maandamano upo ambao wenzetu wanatumia kufikisha ujumbe kwa njia tofauti.Moja wapo ni kuchapisha flana(sare) zenye ujumbe na kuvaliwa na jamii ikiwa inaendelea na shuhuli za maisha bila ya mikusanyiko wala hotuba.Ni mfumo wa maandamano ambao hauhitaji kibali kwa mtu kuvaa nguo yake.naamini ikifanyika kwa siku tatu tu vyombo mbali mbali vya ndani na nje vitaujulisha ulimwengu.

 7. Wamtambwe 08/06/2013 kwa 2:19 um ·

  Hakuna haja ya ya maandamano wakauliwa watu bure, zichapishwe fulana zenye ujumbe mmoja na zifaliwe siku moja Zanziba mzimaa
  “Asieitambua kamati ya maridhiano na Maridhiano wenyewe, iko siku Wazanzibari hawatomtambua naye”

 8. MAWENI 08/06/2013 kwa 2:28 um ·

  Ndio wewe siume ekwa hapo kusimamia kugombanisha wa zanzibari? Hatuoni ajabu wewe kusema hivyo.
  WZANZIBARI WANA ANGALIA MBELE . WANPIGANYIYA HAKI YAO YA KIMSINGI. KUWA NA DOLA YAO ILO HURU YENYE MANLAKA KAMILI. UMA NDIO MS INGI WA UHLALI WA MAMLAKA YOYOTE KWENYE NCHI. UMEPWELEWA. SOMA ALAMA ZA WAKATI. UKIWA HUTAKI KUBADILIKA WAKATI UTAKUBADILISHA WEWE.

  MTU KWAO
  ZANZIBAR KWANZA!

 9. MAWENI 08/06/2013 kwa 2:38 um ·

  KUADHINI KWENYE VIBUYU SASA BASI ULIMWENGU LAZIMA SASA UJUWE WAZANZIBARI WANATAKA NCHI YAO. HAYO YA FULANA SAWA. MPAKA WAZANZIBARI WALIOKO NJE WAZIVAE.
  IKIWE WEZEKANA KUSIMAMA MBLE YA JENGO LA UN KUONESHA BANGO LA MADAI YETU. BARUWA ZEYE SIGNATURE ZA KUDAI UHURU WETU ZIPELEKWE KWENYE TAASIS ZOTE ZA KIMATAIFA. TUNATAKA NCHI YETU SASA TUME CHOKA.

  MTU KWAO SASA TUME CHOKA

  ZANZIBAR KWANZA!

 10. buhanan 08/06/2013 kwa 2:44 um ·

  Si kosa lake ,kosa ni la yule aliempa ushindi .Wazanzibari Sheni SI CHAGUO LETU TUNASEMA KWA MDOMO MPANA .Kwa hiyo tutegemee MADHILA Kutoka kwake na kama hatuamini TUTAONA.Nawasilisha.

 11. jazba ni udhaifu 08/06/2013 kwa 2:51 um ·

  kwa mtazamo wangu hizi ni shinikizo za kichama na kwa wakati huu kauli kama hizi ni kupambana nazo hadharani ikiwa ni hatari kwa umoja au vyoyote vile naviwe hatuwezi kuipeleka zanzibar kuwa mali ya tanganyika tena,
  inabidi tusimame kwa umoja viongozi wa ccm na wa cuf na wananchi wate kwa jumla walio na uchungu wa nchi yetu wakati wa kujitolea ndio huu ni kupingana nae hadharani bila ya woga ndio watakapo fahamu kuwa wazanzibari hawataki tena siasa wanataka nchi yao kwanza siasa baadae
  kwa upande wa ccm kama amani na mansour na viongozi na wanachama wengine walitakiwa watoke nje na kupambana na kauli hizi taim mbaya hii tukiwaacha wakitupeleka shule tena hawa ni miaka mia ijayo au machafuko ya nchi

 12. ex.sakua 08/06/2013 kwa 6:18 um ·

  @ waungwana
  Naona maoni yangu siyaoni kila nikituma kulikoni? Ama nshapigwa ban na mimi?

 13. Abdul 08/06/2013 kwa 6:21 um ·

  sheni fumanizi haiimarishi ndowa

 14. sale 08/06/2013 kwa 7:34 um ·

  Bwana shemegi @ex.sakua mbona hili swali lako linaonekana? unauhakika umetuma maoni?

 15. MKATABA 08/06/2013 kwa 7:51 um ·

  Ikiwa itakumbukwa siku ya mkutano wa K/Maiti tarehe 1/6/13, Mh:EDDY RIAMI,alitowa changa moto kwa wale wanao kataa Mamlaka kamili ya Zanzibar wajitokeze:
  Wamwanzo ni Vuai Ali Vuai na Wapili ni huyu Dr.Mohamed Ali Shein,kwa hivyo Wazanzibari wazalendo waliowengi wenye kuipenda Zanzibar yao yenye Mamlaka kamili walitambue hilo na wamtambue Dr.Mohamed Ali Shein na Vuai Ali Vuai si wenzetu na hawapo pamoja na Wazanzibari, na hayo maneno ya Dr.Mohamed Ali Shein na Vuai Ali Vuai ni salamu tosha kua wao hawako pamoja na Wazanzibari.
  Sasa uwamuzi wanao Wazanzibari wenyewe kwa watu wa aina hii ya akina Vuai na Dr.Shein.

 16. Alhabaad 08/06/2013 kwa 8:28 um ·

  Labda kapewa amri na Nape Nepi!!!

 17. ex.sakua 08/06/2013 kwa 8:52 um ·

  @ sale
  Mtani nadhan kutakua na technical problem, au kuna mtu anafanya hacking.

 18. kifuudume 08/06/2013 kwa 11:59 um ·

  well and good tumefamu ikiwa huo ndi uwamuzi Wake kama kiongozi mkuu wa nchi “haitambui kamati ya Marithiano leo wakati wao hao ndoi Waliojifungia Bwawani wa siku nzima siku ya kutangwaza Matokeo ya Rais.

  Swali langu Jee Unawambia vipi Raia wako Kuhusu rasimu ya katiba Mpya,Tupe Maoni yako! una
  hasa tayari unaonekana Uko na Muda wa kuongea na Vyombo vya Habari Tungependa Ukautumia Muda Huo kutupa Mtazamo wako na Hatma ya serekali yako.Nitashangaa sana ikiwa utatumia nguvu njingi Kujibizana na Kundi usilo litambua,Wakati huo Huo Mh Amani Karume Siku ya kikao cha Mwisho wa kuaga nafasi yake Umwenyekiti wa chama ZNZ alisema kwamba CCM Walishiri Zanzibar kuunda serekali ya pamoja,pengine wewe Muheshimiwa Rais hukuwemo ila lazima walikuwemo ccm.sasa ningeomba Msitumie nguvu nyingi Kuirejesha njuma serekali ila Tutumie nguvu Zaidi Kujuwa Ni vipi Zanzibar Tuitakayo itapita Katika KUjipatia Mamlaka yake katika Tafaraku huu wa Muungano Isiokishwa Kupigiwa kelele.

 19. kifuudume 09/06/2013 kwa 12:06 mu ·

  @ Sale nakumba katika comment yako moja ulisema kuwa “UKIONA CCM WAMEKAKIMYA BAISI HAKUNA JAMBO ” sasa wanume wamekuja juu kujibu una maoni gani,
  Au jambo lipo?

 20. makame silima 09/06/2013 kwa 6:49 mu ·

  Huyu jamaa si Mwanamme wakujipangia maneno yake kama Raisi, akielezacho chochote basi ujuwe kapangiwa hana ubavu kama alionao Jowe kutetea nchi yake,,Nyeye huyu ni Raisi zaidi Dodoma sio kwa Wananchi wa Zanzibar.

  Arubaini zao zinahisabika hawa tusubiri hio Serekali yao Watanganyika iundwe halafu tuone hio Serekali ya kinyaganyiro (Shirikicho) itawashirikicha Wazanzibar wangapi?.

  Mkataa kwao Mtumwa wale vidomo domo wate walio kimpizwa Bara na kuisaliti Zanzibar tutawaona watakavyo haha sasa.

  Hakuna nchi hato moja inayo simama kwa nguvu zake wenyewe bila kutegemea wananchi wake,jee Ccm/smz wananchi wa Zanzibar wako upande gani? hili ndio la umuhimu.

 21. Multiways 09/06/2013 kwa 8:29 mu ·

  dah,,hii kali,,ina mana,,ikiwa,,waliwah kufika kwako mheshimiwa,,walikuja kama nan,,tena ni mara tatu sasa,,leo hii ndio huwatumbuiii,,aaaaaahh,,jaman,,ama kweli,,mzoea punda hapand faras,,ipo siku utawatumbua dhahiri dhahiri subiri tuu,,,sooon,,co muda mrefu baba

 22. star 09/06/2013 kwa 1:07 um ·

  Maalim kasema anagombania tena lkn naona hataki kugombania ila anataka kumpa kipindi cha pili shein . Sasa sie wazanzibari mara hii rais tutomchagua sisi ndie atokuwa rais.

 23. ami-wa-ole 09/06/2013 kwa 9:19 um ·

  Mimi nashauri hivi. Ili Wazanzibari tuonyeshe kuwa twataka Muungano wa Nktaba basi wale Wanzanzibari waishio kule Tanganyika wote warudi zao Zanzibar kwanza. Halafu tuanze maandamano ya Nkataba.

Comments are now closed for this article.