Dk Salmin: Msikubali Mapinduzi kufutwa Zanzibar

Written by  //  03/07/2013  //  Habari  //  Maoni 13

Dk Salmin: Msikubali Mapinduzi kufutwa Zanzibar
NA MWINYI SADALLAH
3rd July 2013

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar walipo mtembelea nyumbani kwake Migombani na kusisitiza umuhimu wa kulinda misingi ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour Juma, amewataka vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kusimama imara katika kulinda uhuru na mapinduzi matukufu ya Zanzibar, ili kupinga nadharia aliyosema ya kinyang’au inayokumbatia ukoloni.

Dk. Salmin alitoa kauli hiyo nyumbani kwake Migombani, Zanzibar jana, mara baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka, kumaliza ziara yake ya siku sita katika mikoa mitatu ya Unguja.

Rais huyo mstaafu alisema, uhuru wa watu hupatikana mara moja hivyo vijana ambao ni kizazi kipya wana jiukumu la kuulinda uhuru ulioletwa na TANU pamoja na kuyatetea Mapinduzi ya ASP.

“Ingawaje kazi ya jumuiya yenu ni kuimarisha chama, kazi muhimu ya bidii ni kupambana na manyang’ au wanaotaka kupora uhuru wenu au kuyatekeketeza Mapinduzi ya Zanzibar” alisema Dk. Salmin maarufu kwa jina la Kamandoo.

Alisema nchi za Kiafrika, Marekani na Ulaya zilikataa kutawaliwa baada ya vijana wao kujitolea kupingana na ukoloni hadi pale uhuru kamili dhuluma na udanganyifu viliipoondoshwa na watu kuanza kujitawaliwa na kujiamlia mambo yao wenyewe

“Kina Mahatima Gandhi, Martin Luther King Jr, Lenin, Karl Max na wengine, walikikataa kutawaliwa katika nchi zao hadi walipopata tunu ya uhuru, hebu inukeni, simameni pia lindeni uhuru wenu, ukipotea hamtaupata milele” aliwaasa vijana.

Akizuingumzia mabadiliko ya mfumo wa kisiasa nchini, alisema ni vyema vijana wakatambua kuwa huko nyuma kulikuwa na mfumo wa chama kimoja ambao ulitoa nafasi ya wananchi na viongzi wao kuwa na misimamo ya pamoja kuliko ilivyo sasa.

“Sasa kuna vyama vingi, hilo ni jambo jema, indhari yangu kwenu mfumo huo usitoe mwanya na ruksa ya kuwaachia wenye mawazo ya kukumbatia wakoloni wakapenya na kutimiza malengo yao, msikubali kuitupa nchi yenu” alisisitiza Dk. Salmin.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 13 katika "Dk Salmin: Msikubali Mapinduzi kufutwa Zanzibar"

 1. abdulwaheed 03/07/2013 kwa 7:25 mu ·

  maneno aliyoongea hapo yana maana mwisho anasema msikubali kuitupa nchi yenu samaki mnaambiwa bc hata akili hamna
  zanzabar kwanzaaaaaa

 2. Multiways 03/07/2013 kwa 6:51 um ·

  ukiangalia,,,yana mantiki sana,,,haya maneno,,lkn vip feedback ya huyu mtu,,,alikua na mongez kama haya apo kabla,,,i mean alipokua ni mzima,,,ama,,,leo tu ndio ameshawishika na wale wanaodai mamlaka kamili,,muhimu ni kufikia malengo lkn,,siku zote,,,ukweli ndio silaha pekee itayotufikisha tunakokwenda,,,

 3. AK-47 03/07/2013 kwa 6:55 um ·

  Well done komando wa udongo kwa kweli ukisoma hayo maelezo utaona uzito wake kwa wenye akili sio hao samaki. Angalia alivosema
  1.pamoja na uvi wa ccm kazi yao ni ya chama lkn wasikubali kuporwa uhuru wao na manyang’au nani hao kama si watanganyika?

  2.anasema nchi za afrika mpaka ulaya zilikataa kutawaliwa na vijana wapiganie mpaka dhulma na udanganyifu uondoke na uhuru kamili upatikane na kujiamulia mambo yao wenyewe .sasa nani wadhulumiwa na kudanganywa kama sio znz?

  3.anawambia kina mahtma gandi luther king walikataa kutawaliwa ktk nchi zao na wao vijana walinde uhuru wao kwani ukijakupotea hawatoupata milele upi huo kama sio zanzibar na hii katiba mpya?

  4.mwisho anawambia waache mawazo ya kukumbatia wakoloni ili wasje wakaweza kutimiza malengo yao nani hao kama sio watanganyika?

  5.kwa msisitizo wasikubali kuitupa NCHI YAO ipi hyo kama sio ZANZIBAR?

  Chakungaza hyu mwinyi sangara ndio ktk hao samaki yy ameona kaeka heading nzuri lkn kasahau kuwa ameweka quote za komando ndani yake na ndioo zenye maana.

  HONGERA COMANDO lkn ndio hivo hao ni SAMAKI!!!

 4. fey 03/07/2013 kwa 8:04 um ·

  Huyu hapo mwanzo hakuwa na kauli Kama hizi maana alikuwa na kibri na kuwafurahisha waliomuweka, Kama ailvyo Shein hivi sasa. Hata Kama alikuwa anaona yanayofanywa sio lakini alikuwa anachunga unga wake, hata last moment alipotaka kuitetea Zanzibar ndio walipompa sumu kwa kujua itamuathiri baada ya kumaliza muda wake. Na sasa ndio anathubutu kusema kuwa vijana wailinde nchi yao, alipokuwa na sauti alikuwa kisasi wa Pemba na kutia sumu wa unguja na Wa Pemba “mshenzi hatumsamehe maisha”

 5. serelly 03/07/2013 kwa 8:08 um ·

  Mwinyi Sadala yamekushinda maneno ya Komandoo kuyaCCMisha, nikifumba macho nina hisi kama ninasoma maneno ya Barua ya Shkh. Msellem Bin Ally kwa Umma wa Kizanzibari. Lakini Masikini kaandika Sadala {SAMAKI}! Ama kweli atakalo Allah huwa.

 6. buhanan 04/07/2013 kwa 4:00 mu ·

  Mmeniona, nimependeza ,mama salma huyo,kamando wa udongo mfa maji haachi kutapatatapa ,tuombe husnul khatima kamando pale ulipokuwa na nguvu ndio usime maneno hayo sio leo tena huwashi huzimi ,ulighurika na ulimwengu na ukajisahau hili ndio tatizo letu la viongozi wetu wanajisahau halafu ndio inakuwa shida sana .KAMA TUDINU TUDANA.Nawasilisha.

 7. Wamtambwe 04/07/2013 kwa 8:04 mu ·

  Huyu mtu Mnafiki sana, Bado CCm anataka na Mamlaka kamili anayataka. Mimi siono haja ya mpaka leo kumung’unya maneno. Sema wazi msimamo wako ueleweke. Hapa pana mbivu na mbichi tu, mambo ya mafumbo inaonyesha ya kwamba mpaka leo huko huru kusema maoni yako hadharani. Kama alivyose mchangiaji mmoja kuhusu Mh. Bomani. Dr. Salmini bado unaonekana ni Mtwana, yaani bado huna uhuru wa mawazo. Unaigopa ccm wasikunyanganye Vijihekta ulivyojimilikisha? Hutoingia navyo kaburini hivyo Baba.

 8. MAWENI 04/07/2013 kwa 8:32 mu ·

  Mapinduzi + Muungano = Ukoloni wa Tanganyika juu ya Zanzibar.

  The motto : MAPINDUZI DAIMA.
  Sasa siwakati wa kutafuna maneno , waabieni vijana kweli.
  Mapinduzi ya kweli ni kuwa na Zanzibar yenye Mamlaka Yake Kamili Naje na ndani.

  ZANZIBAR KWANZA SHENGESHA BAADAE .

 9. makame silima 04/07/2013 kwa 8:54 mu ·

  Hapa mimi kanipa shida kidogo Mh Kamandoo ,katika kutowa nasaha na karibio la kuhatarishwa Zanzibar kurudi tena kwenye ukoloni, Sasa lakumuliza hao WAKOLONI aliokusudia Mh Kamandoo ni wapi wanao taka ku kolonazi Zanzibar?.

  Au kakusudia Sultan Muarabu? Maana akisema kuwapiga vijembe Cuf basi Cuf ni Wazanzibar halisi , na hata huyo Sultani jemshid ni Mzanzibar ,kazaliwa Zanzibar kasoma Zanzibar, kwa hio ana haki ya uzawa sawa na Ali Hassan Mwinyi na Jumbe Wamezaliwa Tanganyika wamesoma Zanzibar?.

  Sasa tumulize Kamandoo nani anae hatarisha Mapinduzi ya 64 na Muungano tulionao? mimi nahisi huyu rabda nimefahamu vibaya lakini nahisi kakusudia Mizengwe Pinda aliposema Zanzibar sio nchi?.

  Ikiwa ni Warabu Sultaani basi wao ndio hujipendekeza kwenda kuomba misada na sizani kuwa warabu wa Omani watarudi tena Zanzanzibar hizo ni chuki tu za kibaguzi labda watakao rudu ni wazanzibar wenye asili ya kiarabu.

 10. fey 04/07/2013 kwa 3:24 um ·

  @Buhanan:
  Kwani hayo tu, Kuna siku alijisifu na kusema hivi “: Wenzangu hapa patamu hapa” huku akitingisha matako, Juu ya yote hayo alizidi jeuri, na kibri kwa kusema tangu lini mbwa akaingia msikitini,

  Alipouuwa Micheweni na kumuacha kijana wa miaka 23 (wakati huo ) kuwa mlemavu wa uume (kapigwa risasi ya tako na kutokea utupu wa mbele) siku iliyotangazwa CUF kupata usajili, kwa kosa la kupachika Pendera

  Maalim alipomlaumu akasimama na kusema kuuwa wa Pemba 1, 2 mpaka …….. (Nimesahau) si tatizo na jengine alipokuja akasimama akasema mwendaazimu mmoja wa UNguja ni bora kuliko wa Pemba 10 kwa kuongoza.

  Jee anayakumbuka haya? Kama yeye amesahau basi sisi tutakwenda nayo kaburini. Na yule kijana alitamka juu ya jukwaa kuwa hatomsamehe Salmini, na alisema ” ameniweka pabaya Salmini, ndio nimesalimika lakini nipo tu”

 11. mzaliwa 04/07/2013 kwa 6:54 um ·

  kama anamazungumzo ya kweli si ache kuongea tunduni toka kaa jukwaani utamke au unaona haya kwani nawe ndio ulio toboa jahazi?
  Unajificha na ukiona zanzibar imepatikana ndio unajitoa tunduni,
  We bado kikulacho tu.
  Zanzibar huru.

 12. Abdul 05/07/2013 kwa 7:16 um ·

  hakuna mkamilifu hivyo hatupaswi kunanga wala kumuumbuwa komandoo kawaelimisha samaki ila hao ni samaki mikizi na mwinyi sadala habari ameishindwa na uchambuzi

  habari ipo kimuamsho zaid sasa wewe ulikuwa u i ccm

Comments are now closed for this article.