Deni la umeme laanza kulipwa

Written by  //  19/03/2017  //  Habari  //  Maoni 6

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) imeanza kulipa deni lake inalodaiwa na Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco).

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa Profesa Muhongo amesema SMZ imelipa kiasi cha Sh10 bilioni na itaendelea kulipa deni hilo hadi litakapomalizika.

MCTL

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 6 katika "Deni la umeme laanza kulipwa"

 1. abuu7 19/03/2017 kwa 11:43 mu ·

  Kateni nyinyi wanafik. Sheni hawezi kulipa .pesa za wavuja jasho wanazolipa wananchi.tunataka ziwembele kwa mbeke.wakati sheni wakisema washaanza kulipa.itabidi kuna mambo muhimu ambayo.yatekelezwe itabidi ya simame kwanza .kwa ajili yakulipa umeme.

  wazanzibar hatutambui hilo deni. Kama miaka yote hiyo mlikuwa mkitanuwa
  na kujenga minara na marejeo ya uchaguzi wa balozi mwizi (seif mweusi)

  Tunasema hatulipi taxi ili na nyinyi msiweze kulipa deni.
  CCM inafanya kufuru na ndiomaana mitumbo mikubwa.hawawezi hata kufunga nyuzi za viatu.

 2. moyo 19/03/2017 kwa 12:19 um ·

  Tulisema zamani humu kuwa hawawezi kuukata, na sasa wanajidai kuwa Zanzibar imeanza kulipa deni lake. Waongo wakubwa serikali ya Zanzibar haina uwezo hata wa kulipa mishahara ya wafanyakazi itaweza kutoa bilioni 10 !

  Si mseme tu kuwa rais wa malaika aliporoja siku ilie.

 3. mzeekondo 19/03/2017 kwa 2:58 um ·

  Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Rais wa jamhuri ya Tanganyika,mtawala halisi na amiri”emir” jeshi wa majeshi ya ulinzi na uvamizi, yanayo vikalia kwa nguvu visiwa vya Zanzibar, chini ya kivuli cha chama cha mapinduzi, kinachoamini na kuhubiri utawala bora,sheria, katiba na uongozi safi, tafadhali usikubali usanii huu wa Tanesco, Zanzibar sio kama hatuwezi, hatutaki na kamwe hatutolilipa deni hili la umeme unalotudai, kwa sababu sisi “your loyal subjects” ni koloni lako,ni wajibu na jukumu lako kuhakikisha hatukai gizani maisha yetu yote.

  Nafikiri utakubaliana na mimi kuwa hatutaki kumaliza kulilipa deni hili kwa senti hizi billioni 10 tulizotowa kwa sasa,wakati matumizi yetu kwa siku unayajua yanavyoongezeka, pia deni lenyewe hizi billioni 180 na ushee “and counting” tutafika siku ya kiama basi bado wewe tajiri yetu itakuwa bado unatudai,ulipaji huu ni sawa sawa na mtu anakudai kontena moja la karafuu kavu/karanga,na wewe umeamua kumlipa kifuniko kimoja cha soda ya coca cola kwa mwezi kwa hapa kwetu, au cha bia”pombe” kwa huko Tanganyika,sasa usijifanye hujui hesabu au hujasoma, tafadhali nijibu lini utalipwa kontena lako la karafuu kavu au karanga kwa huko kwenu.

  Sisi Wazanzibari mtatuonea kwa mengi,wizi wa kura,wizi wa fedha zetu za kigeni na hizi zenu za madafu,ardhi,bahari na kila mnachoona inafaa mchukue nyie kwa kisingizio chenu kitukufu cha Muungano na nchi yenu adhimu ya Tanzania,sisi wanyonge wa mungu hatuna,sauti/kauli, nguvu za mikononi wala vifaru,lakini kwa hili la umeme hapa mtaimba sana,hili TUMEKUWEZENI.

  Deni hili lipo kabla hujabalehe mheshimiwa,na utaliacha hapa hapa, mpaka hivi sasa unakurubia kama hujavuka ‘menopause’ hili deni linaongezeka,tafadhali jiulize mheshimiwa kwanini tukulipe au tukutunze kwa kukulipeni, wakati nyie ndio mnaojilazimisha kututawala sisi kwa nguvu?umepata kuona wapi mtu anaeku’uwa kabla hujakata roho, ukaamua kumlipa deni lake lote, huku ukijua kuwa ukimlipa usimlipe roho anaitoa tu.

  Sisi tuna matatizo mengi hapa visiwani kwetu, na hatuelewani kabisa, ndio maana imekuwa rahisi kwako au kwenu kututawala miaka yote hii,lakini kwa hili la umeme tunaelawana, ndio maana kila kibaraka mnaemuweka hapa atutawale kwa niaba, umeme Halipi,tuko radhi wajenge majumba yao ya kifahari na kuongeza mahawara kwa fedha hizo lakini Tanganyika deni liongezeke.

  Mimi nilisema na wenzangu wengi hapa maskani walisema kuwa hamuwezi kukata umeme,na hili suala la umeme kwa hapa sio makamo yako mheshimiwa,sisi bado tunaomba duwa ile amri yako uliyotowa bila kutumia maarifa Tanesco waitekeleze,kwa sababu ‘NYIE MKIKATA UMEME, NA SISI TUNAKATA MUUNGANO” sas tumbua hili jipu kama kweli mheshimiwa wewe hujaribiwi,sisi tumeshakujaribu ndio maana Rais wako wa hapa Dr Sheni alikwambia KATA na yeye atawasha KIBATARI IKULU. sasa unasubiri au unataka majaribu gani tena mheshimiwa zaidi ya haya inaonyesha huyu muungwana hakuogopi tena.

  Komandoo Salmin Amour aliwahi kumwambia babu wa taifa mwalimu nyerere,kuwa asitikishe kibiriti,sasa na wewe baba wa Tanganyika unaambiwa na Daktari Kata au zima,pia alituhutubia kwa kujiamini,kuwa anavyojua yeye umeme hauzimwi/haukatwi,na sisi tunamuamini kwa hili sio mengine, sasa nani mkubwa kati yenu wawili?mkoloni mwenyewe rasmi au muwakilishi mwenyewe,mimi leo sikuja kuleta uchochezi, nimekuja kupalilia makaa tu, huu moto mmeuwasha wenyewe bila kusaidiwa na mtu, kwa kauli/amri zenu za kila siku zisizokwisha, hata jua nalo huvuta shuka na kwenda lala au kupumzika wakti ukifika, lakini sio AMRI ZENU waheshimiwa.

  KATENI UMEME NA SISI TUPATE SABABU.

 4. Abdul Zakinthos 19/03/2017 kwa 9:45 um ·

  kwa hisabu za haraka haraka ni 5.5% ya deni limelipwa sasa hebu tuambiwe Mapato ya Serikali Ya Zanzibar kwa mwaka ni kiasi gani?
  Kisha mishahara ni kiasi gani na tujue tutamaliza lini hili deni?

  Na je lilifikaje hili deni kama ni miaka 20 wanavosema kwa hiyo kila mwaka tunadaiwa Bilioni 9 je mapato yetu yanafika?

 5. Abdul Zakinthos 19/03/2017 kwa 9:46 um ·

  Sasa Waziri Wa nishati imekuwaje ajue pesa zimelipwa kwani yeye ni tanesco?? au anasimamia mapato ya tanesco?

 6. moyo 20/03/2017 kwa 8:21 mu ·

  Kwani ni hilo tu la waziri muongo, taarifa pia imetolewa na msemaji wa ikulu! Sijui afisi ya tanesco imehamia ikulu.

Comments are now closed for this article.