Damu ya wazanzibar ikimwagika basi na hawa ni miongoni mwao

Written by  //  14/03/2017  //  Habari  //  Maoni 14

IMG_7502

Ndugu zangu wanaukumbi na wazanzibar wezangu wandani na wanje ya nchi, tumeshuhudia unafiki na uchochezi wa kundi hili la Lipumba kupalilia mafa na damu ya wananchi wa Zanzibar imwagige ili tu hawa wanafiki wajaze matumbo yao.

Lakini sisi wananchi wa Zanzibar tunajua tafauti ya nyekundu na nyeupe tusichaguliee rangi si majuha wakuto kujua yupi ndie na yupi sie.

Sisi tunasema yakitokea mafaa hapa Zanzibar hatuto wanyoshea vidole Lipumba na Saif iddi tu.

Mujuwe na nyiyi wafuasi wa Firauna hatuto wasamehe kwa njaa zenu kama munaona biashara ta tumbo ni ufitna zakutaka kuwakandamiza Wananchi wa Zanzibar ?.

Basi yakitokea roho na damu za wazanzibar zitawaganda milele.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 14 katika "Damu ya wazanzibar ikimwagika basi na hawa ni miongoni mwao"

 1. alwattan 14/03/2017 kwa 5:38 um ·

  Hata khalifa aliekuwa mbunge kwa miaka 20 kama sikosei wa jimbo la gando , leo anakosa fadhila la wapiga kura wa gando, anawasaliti wapigania haki?

  • jazba 14/03/2017 kwa 6:38 um ·

   na huyu jamaa wala hajielewi kuwa hasira zake na chuki juu ya kukosa ubunge ndio zinamfanya atumiliwe tu kwa maslahi ya watu wengine

 2. Jino kwa Jino 14/03/2017 kwa 6:37 um ·

  BREAKING NEWS
  TAARIFA KWA UMMA

  TAWI LA JUNGUNI LAMVUA UANACHAMA KHALIFA

  Leo ilikua ni zamu ya Tawi la Junguni kufanya maamuzi ya kumfukuza uanachama wa CUF Mhe. Khalifa Sleiman Khalifa ambaye alikua ni mwanachama wa CUF katika Tawi hili uamuzi huu umekuja ikiwa ni siku ambayo chama cha wananchi CUF kinaendelea kuwang’oa wale wote mamluki na wanafiki waliokua wanaunga mkono kundi haramu la wanaojiita Mungiki.
  Ikiwa nisiku ya pili tu mara baada ya Lipumba kufanya uteuzi kwa wale anaowaita Wakurugenzi ambaye Khalifa Sleiman Khalifa akiwa miongoni mwao.

  Tawi la Junguni lipo na wanachama hai 98 na waliohudhuria ni 64 wanaume wakiwa 27 na wanawake wakiwa 37 na wote kwa sauti moja wakiridhia kumfukuza uanachama mdhandiki na mnafiki huyu na huku wakitoa onyo kali kwa mwanachama yoyote atakayefahamika akiunga mkono Kundi la mungiki basi hatua za kinidhamu zitachukuliwa.
  Mwisho mwenyekiti alitoa tamko la kuwataka wanachama wote washikamane kukilinda chama chao ambacho ni chama cha wananchi CUF.

 3. Jino kwa Jino 14/03/2017 kwa 6:40 um ·

  THE CIVIC UNITED FRONT
  (CUF-Chama Cha Wananchi)
  Tawi La Kangani (Jimbo La Mtambile)
  Wilaya Ya Mkoani (PEMBA)
  14/3/2017

  TARIFA KWA UMMA
  Mkutano mkuu tawi la Kangani ume mfukuza rasmi uwanachama. Nd: NASSOR SEIF AMOR mkutano mkuu ulidhia kumfukuza, nd: Nassor kwa kukiuaka katibaba ya chama (IBARA YA 11) kifungu kidogo cha (1) na cha (2) na ( IBARA Ya 12) kifungu kidogo cha (2) cha (6) cha (7) cha (8) na cha (16)
  Wajumbe hakali wa mkutano mkuu (TAWI) ni (437) akidi ni wajumbe (219) wajumbe walio hudhuria ni (226) walio Kuala kufukuzwa uwana chama Nd: (Nassor Seif Amor) ni (226) sawa na asilimia 100% ya kura halali
  Asnteni sana
  CUF NI TASISI IMARA ISIO YUMBA
  HAKI SAWA KWA WOTE
  Kaimu Katibu wa tawi Kangani
  0778-702878

 4. Piga nikupige 14/03/2017 kwa 8:33 um ·

  Dawa yao ni kunadiwa mwizi tu popote watakapo onekana kwenye mitaa au Masokoni, hasa huyu Khalifa ndio kazidi. Aibu imemtoka kaweka nyuma fadhila za miaka 20 aliyo fadhiliwa na watu wa Gando, lakini labda hakuwahi kupigiwa kura na watu wa Gando, alikuwa akipigiwa kura na Lipumba ndio akawa mbunge.

  Tunaomba wasaliti wote zisambazwe picha zao na majina yao kwa ukamilifu watu wawajue vizuri ili wajipange kulipiza kisasi cha maandamano yaliyo pita na kupelekea kuuwawa watu wasio kuwa na hatia. Nashauri washughulikiwe haraka iwezekanavyo endapo kutatokea dalili tu za umwagikaji wa damu.

 5. Mkandaa 15/03/2017 kwa 4:54 mu ·

  Siko kwenye mada ya kuvuana uanachama ama kugombani uongozi ila nataka nichangie hii tabia ya Wanasiasa kutokuridhika na kujiandaa na maisha nje ya nyadhifa zao kisiasa.

  Ukiangalia kwa umakini utabaini kuwa wanasiasa wengi huingia kwenye siasa kwa ajili ya maslahi yao binafsi na kwa bahati mbaya hata pale wanapopata fursa hushindwa kuzitumia kujiendeleza, mwisho wa siku huishia kudhalilika, kutukanwa na kuhama vyama kama watu waliokosa rehema za Muumba.

  1. Pato la Mbunge.
  Ukifuatilia mishahara na maposho ya Wabunge utabaini kwamba Mbunge anaweza kumiliki hata milioni 50 kwa mwaka ukitoa matumizi yake na makato mbalimbali, wakati huo huo Mbunge huyo anahudumia watu wasiozidi laki 1 katika jimbo lake. Mfanyabiashara mdogo huanza na mtaji wa milioni 5 na akaweza kuuendeleza hadi kuwa mfanyabiashara wa kutegemewa wa bidhaa za jumla. Sasa tujiulize Waheshimiwa hawa huwa wanakosea wapi hata washindwe kujiendeleza na kusaidia maendeleo ya Wengine?

  2. Eneo la Jimbo na huduma zake
  Kiukweli eneo la Jimbo moja la huku kwetu Bara unaweza kutoa majimbo matano ya huko Zanzibar, tukiangalia waheshimiwa Wabunge wetu huwa wanajitahidi kujua kero za Wananchi na ama kuzisemea Bungeni au hata kuzitatua kwa njia zao kwa kuwa hayo ndio majukumu makuu ya Wabunge. Wabunge wote wanapata kipato sawa bila ya kujali ukubwa wa jimbo au wingi wa wapiga kura, inasikitisha kuona Mbunge anakosa mikakati ya kuendeleza Jimbo au hata kuishi kama vile yeye ni mtu wa dunia nyengine hadi ufike wakati wa uchaguzi. Imefika wakati sasa kwa wananchi kujitathmini mahusiano yao na Wabunge.

  Hapa tujiulize iwapo Mbunge ataamua kuanzisha kamati za maendeleo ya Jimbo na kushirikisha watu wa vyama vyote, akaanzisha mfuko wa Jimbo, akaamua kuekeza katika miradi ya maendeleo yenye tija kwa wananchi na kuchangia mfuko wa Jimbo, atakuwa amesaidia maendeleo ya wananchi. Mradi gani Jimbo lianzishe hilo litaamuliwa na kamati za maendeleo za Jimbo kwa kuzingatia vipaumbele vyao.
  Hapa nitolee mfano wa jambo moja na namna linavyoweza kuakisi maendeleo. Tuchukurie Mbunge ameanzisha mfuko wa SACCOS wa Jimbo kwa milioni 30 na kuanza kutoa huduma zake kama SACCOS nyengine, baada ya miaka 10 itakuwa tunazungumzia mili 500, na itaendelea hivyo hivyo hadi kufikia bilioni ama uwezo wa kuibadili SACCOS na kuwa Benki ya Jimbo husika.
  Tatizo la Wabunge wetu ni kudhania kwamba kila kitu lazima kifanywe na Serikali na wao jukumu lao ni kusema na kugonga meza tu.

  3. Upatikanaji wa Wabunge.
  Vyama havina budi kuanglia Utaratibu unaotumika kuwapata Wagombea wa nafasi mbali mbali, kuna umuhimu kuwashirikisha wananchi kwa hatua zote na kuheshimu maamuzi yao, vyama vinatakiwa kusimamia rushwa ya aina yoyote wakati wa mchakato wa kupata wagombea, na ikibidi katiba za vyama zitoe msimamo juu ya hukumu kwa washukiwa wa rushwa wakati wa chaguzi za vyama. Hii itaondosha uwezekano wa watu kurubuni wapiga kura wakati wa michakato hiyo na hivyo kujifanya wabunge wa kudumu ilhali wananchi wanadhalilika.

  • Ghalib 15/03/2017 kwa 12:47 um ·

   @mkandaa

   Wabunge wa Zanzibar ndio wenye uwezo huo wa kufanya maendeleo zaidi kuliko hata bara kwa sababu kama unaangalia jimbo la mbunge basi idadi ya wananchi wa jimbo hawafiki hata 40, 000 wakati tanganyika jimbo linaweza kuwa na watu milioni 1.
   Nakiomba chama kifanye tathmini ya wabunge walio kaa katika nafasi hizo kwa muda mrefu kama utekelezaji wa ahadi pamoja na ilani ya chama haudhishi kwa wananchi pamoja na chama waondolewe katika uchaguzi Ujao, na wale ambao ni wasaliti vile vile bila ya kuoneana huruma.

   Ndugu wazanzibari tuongeze dua kwa Lipumba ambaye anataka kuvuruga haki yetu isipatikane, Allah ampe analo stahili kulipwa na nia yake mbaya isifanikiwe pamoja na walio kuwa nyuma yake Amin

 6. sadimba 15/03/2017 kwa 1:04 um ·

  @Ghalib

  Mimi naungam mkono maone yako ila napenda kuongezea tu mchawi hakutesi kama jamaa yako hayumo, na udhaifu wa binadamu utauona kwenye kitu. Kama wazanzibar waliokuwa wabunge kwa miaka ishirini kwa vilewananchi wamewaona hawatekelezi ahadi zao wamewahukumu imekuwa nongwa. Hawa jamaa zetu wanaofikiri kwa kutuia matumbo ndio wanaotegemewa katika move hii ambao dolla ina mkono wake. Na mimi napata mashaka walikuwa wakitumiliwa kukihujumu chama na wananchi kwa jumla.

  Watu hawa naona ng’ombe ana afadhali kuliko binadamu aliyrthamini utu wake.

 7. chatumpevu chatumpevu 15/03/2017 kwa 1:32 um ·

  Wazalendo wote
  Naheshimu mawazo ya wachangiaji wote. ukisoma pace ya uharibifu wa Lipumba kwa CUF utaona anafanikiwa na anatanua scope ya uharibifu kila kukicha. Ukiona kuwa ameweza kuwashawishi wabunge wa cuf kumuunga mkono ujue kuwa hali ni tete kwa ustawi wa chama. hatujajua hata wale wafuasi wa hamad Rashid na wao wanamsaidia / allies ktk uharibifu huu. Lililo dhahiri ni kuwa rupia inatembezwa na rupia hii inatoka SMT via ofisi ya msajili.

  Kinachofuata ni wafuasi hawa kufanya fujo znz na si ajabu iko siku tuataamka tukiona kuwa ofisi za cuf zimedhibitiwa na mazombi na polisi ili kuwaruhusu wasaliti hawa akina Nassor seif na Khalifa et al kufanya kazi ndani za ofisi za Mtendeni.

  Tujue kuwa chama kinapitia kipindi kigumu ( storming stage) na kikivuka ktk dharuba hii yenye jina la “lipumbavu hurricane” basi itakuwa ni vizri ingawa sitarajii kwani wahuni waliochaguliwa na lipumba hivi krbuni wanaungwa mkono na dola kule znz. Mkuu wa kaya wa SMT ameapa kupitia msajili wa vyama kuiondoa cuf ili mwka 2020 aingie ktk uchaguzi kukiwa na UKAWA iliyo dhaifu.

  Ni wakati muafaka kwa viongozi wa cuf kufanya tafakuri ya kina ya jinsi ya kuwabaini wasaliti na hao ni wengi na jinsi ya kukabiliana nao. Ujenzi wa chama cha siasa si kitu rahc na tukumbuke kuna wenzetu zaidi ya 45 walishapotezewa roho zao kwa kukilinda chama.

  Nini kifanyike?
  1. viongozi wawatayarishe wananchi na hasa wagombea kisakilologia kuwa ktk kugeombea nafac za ubunge/ uwakilishi/ diwani ni kuweka mbele maslahi ya chama sio ya binafsi.
  2. Kuweka mwongozo maalum kwa watakaochaguliwa wa kuleta maendeleo na viongozi wapimwe performance yao ( performance appraisal ) ktk kuleta manedeleo majimboni mwao( refer mawazo ya mkandaa ) .
  3. Kuwe ni vipind maalum ( isizidi miaka 10) ya mbunge/ mwakilishi/ diwani / rais kushika nafac aliyogombea
  .

 8. kisisina 15/03/2017 kwa 2:05 um ·

  Nimeiona, picha ya Musa haji, na nasoro,sef, hawa weto mimi nawajuahibu, ntakupeni wasifu wao nkipata nafasi

 9. abuu7 15/03/2017 kwa 2:52 um ·

  Tumbo likikosa chakula .basi mishipa ya ubongo huwa inashindwa kufanya kazi.
  mimi naona kitawaka mapema. CCM inataka kuwasha vibatari.hii ni moja ya kupitisha wahalifu kutoka bara kuja kuvamiya ofisi za CUF .ndio ukasikiya wanataka kukata umeme.

  walijaribu kupitiya njia ya uchaguzi wa marejeo ili wazanzibar wachokozeke. Matokeyo yake wakaona watu wako baardi kama kawaida.sasa CCM inakuja na njia ya mnyamwezi ( mnyamwizi) lipumba.Malim Seif alikwisha kuwambieni kuwa Amani ya Visiwani imezuiliwa na yeye na wala sio CCM.au Sheni.
  KAZI KWENU NAONA MTAIYUWA CCM KWA KUMTUMILIYA LIPUMBA.
  MAALIM NI WA WAZANZIBAR.HATA MFANYE NINI

 10. Mkandaa 15/03/2017 kwa 4:07 um ·

  CUF haiku imara katika kukabiliana na matatizo mazito na yenye taswira ya mgogoro wa mara hii, migogoro yote iliyopita ilikuwa inahusisha Chama na haikuwa na wadau wa nje ya Chama. Kama wenyewao wanavyosema kwamba wanapambana na kambi nyingi sana. Katiba ya Chama ina mianya mingi inayotoa nafasi kwa taasisi nyengine kukidhoofisha. CUF kama taasisi imekosa wanamtandao na wanamkakati wa kukabiliana na matatizo, chama kinaendeshwa kiimani Zaidi.

  Utaratibu uliotumika kukabiliana na kadhia Prof. Lipumba ni ushahidi toja juu ya hilo; Kwa kufahamu kikatiba Lipumba alipaswa kuwa Mwenyekiti hadi 2019 utakapofanyika uchaguzi mwengine na kwa kuzingatia matakwa ya Kikatiba ya kuziba nafasi yake, kuziba nafasi ya Lipumba kulipaswa kuwa sehemu ya agenda wakati wa mkutano wa kutathmini kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

  wana CUF wa sasa (??? baadae) wanatakiwa kujiandaa kikamilifu na kuwa na mbinu mbadala. kwa vile suala la uchaguzi wa Zanzibar ni mpaka 2020 na hakutegemewi mabadiliko yoyote ya Uongozi, mgogoro huu utaendelea kuwepo ili kukidhoofisha chama na utapamba moto ifikapo mwaka 2019 kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 na si shaka ukakiyumbisha chama kushiriki uchaguzi huo na Chama kupoteza muelekeo Zaidi ya uchaguzi wa marudio wa 2016. CUF ni chama kilichopo kiimani, wafuasi wake wanaunganishwa na Imani yao kwa Viongozi na sera za Chama, ni wakati muafaka Viongozi kufanya Uamuzi wa Busara utakaopelekea Imani na sera kusimama imara 2020 na kuwaacha wasaliti mdomo wazi na kuingia katika historia mpya ya ushindi mkakati.

 11. hamad salum 15/03/2017 kwa 6:09 um ·

  Cannibalism.

 12. Abdul Zakinthos 15/03/2017 kwa 8:25 um ·

  @Mkandaa
  nikukumbushe tu CUF ni Taasisi na ipo imara, na haindeshwi na imani kama unavofikiria ila watu wamefikia hatua ya kukata tamaa na serikali ilokuwepo

  Kuhusu suala la Lipumba ni obvious halitaki hata dictionary , walikuwepo wengi na waanzilishi hasa sasa ivi wako wapi?/

  Watakwendaa watasaidiwa na kila mtu lakini wataishia kunawa tutawasahau kabisa.

Comments are now closed for this article.