CUF watueleze umuhimu wa wao kuwa Sehemu ya Serkali
Written by Bablee // 31/12/2012 // Habari // 21 Comments
Wazanzibar walipoamuwa kupiga kura ya ndio ili kukubali uwepo wa serkali ya umoja wa kitaifa (SUK) walikuwa na matumaini ya kuona wazanzibar wanakuwa na amani na umoja katika kupeleka mbele maendeleo ya Zanzibar, lakini pia kuwa pamoja katika kudai na kutetea haki Zanzibar. Lakini, pamoja na uwepo wa amani, wazanzibar waliowengi walitegemea kwamba uwepo wa CUF kwenye serkali hiyo kutapunguza kama sio kutaondosha kabisha unyanyasi na uvunjwaji wa haki za binaadamu, walitumaini kutaondosha ubabaishaji katika kuendesha serakli, kutapunguza rushwa na badala yake kutaleta afuweni katika maisha ya wazanzibar ambao wengi wao ni maskini. Zaidi ya hili la kuwa na amani (ambayo kifupi si amani ni utulivu tu), CUF wanalipi jengine lakutwambia?
Chama cha CUF chenye “slogan” ya HAKI SAWA KWA WATOTE, ilitegemewa uwepo wake kwenye serkali, haki za wazanzibar zitalindwa, badala yake tumeendelea kuona haki za msingi kabisa za binaadam (wazazibar hawa) zikikanyagwa na kukandamizwa! Kuanzia wakati wakuandikishwa sensa watu kuvamiwa wakipigwa ovyo majumbani mwao, na hata hili sakata la kukamatwa baadhi ya masheikh kisha kunyolewa ndevu, kutengwa na wafungwa wengine, kunyimwa dhamana, kuzuiliwa kuonana na wanasheria na ndugu zao n.k. Ubaya ni kwamba waziri wa katiba na sheria ni kutoka CUF! Hata kama mahakama haingiliwi, lakini kuna mengine hayahusiani na mahakama ni ukiukaji wa sheria unaofanywa na askari kule mahabusu! Na hayo yaliopo mahakamani, kama kiongozi unaona mahakama unazozisimamia hazitendi haki inakupasa kuwajibika ili uendelee kulinda heshima na sera za chama chako. Lakini leo itawezekana vipi kuilaumu serkali (magereza na mkugerenzi wa mashtaka) kwamba inawakandamiza na kuvunja haki za masheikh wetu bila kuihusisha CUF? Itawezekana vipi kulaumu polisi waliovamia makazi ya raia na kujeruhi (mfano kijiji cha Kendwa) bila kuihusisha CUF, wakati waziri wa katiba na sheria na makamo wa kwanza wa rais ni CUF?
Tumesoma kwamba shirika la ndege la Precision Air tangu lilipoanza kuleta ndege zake Zanzibar haliwajawahi kulipa kodi kwa ZRB! ZRB wameamuwa kuzuia ndege za shirika hilo, lakini kwa ambri ya mkubwa/wakubwa wa ikulu. Wakubwa hao wamepiga simu eti ndege za shirika hilo ziachwe zitue zikiruka kama kawaida tu…hivi CUF wapo wapi katika kukemea kama sio kuzuia utumbo huu? Jee tutaweza vipi kutenganisha CUF na utumbo huu ikiwa CUF pia ni sehemu ya ikulu?
Kama haitoshi, tumesoma kwamba kampuni ya kikristo ya AGAPE imepewa tenda ya kuuza ving’amuzi Zanzibar, lakini hakuna kumbu kumbu ya lini na wapi tenda ilitangazwa! Waziri wa biashara na viwanda ni CUF! Jee CUF watatuambia nini katika hilo? Tutathubutu vipi kuilaumu serkali bila kuihusisha na CUF!
Kuna umuhimu gani wakuwepo kwenye serkali hii ikiwa kama viongozi hao wa CUF (mawaziri na makamo wa rais) hawana nguvu hata yakumpa ambri mfagiaji wa ofisi! Kuna haja gani yakuwa sehemu ya uvundo ukiwa huwezi kuondoa au angalau kuupunguza uvundo huo? Kuna lipi wanalolifanya viongozi hawa wa CUF lenye kuonesha utofauti kiutandaji zaidi ya kusain mabuku ya “attendence” na kupokea mishahara yao mwisho wa mwezi! Kuna mabadiliko gani ya kiutendaji na kiufanisi katika wizara za SMZ baada ya kuwemo CUF kwenye serkali? CUF wangekubali tu kumkubali Amani Karume kisha wakaamuwa kuwa wapinzani kama mwanzo tu, basi kwa amani hii (mie naita utulivu) tungeipata!
CUF watueleze walikosea wapi mpaka wakapewa madaraka yasiyo na maana zaidi ya kujaza matumbo yao (kwa kupokea mishahara), watueleze walikosea wapi mpaka wakawa viongozi makoti bila vitendo? Waje watueleze ilikuaje wakakubali kuwa wa ving’ora bila kuwa na ambri? CUF watueleze kuna umuhimu gani wa wao kuwa sehemu ya serkali?



21 Comments on "CUF watueleze umuhimu wa wao kuwa Sehemu ya Serkali"
@Bablee
Hayo yote ni madogo kubwa zaidi na hofu ya Wananchi wa Zanzibar hivi sasa kwa Serekali yetu ya Smz ni Kanisa na Muungano.
Naziki zote hizo na manyanyaso yote hayo yanayofanywa na vyombo vya Dola chini ya Amiri Jesh Mkuu kikwete na Shein, Kubwa wanaloliogopa Wazanzibar hivi sasa ni chokochoko za Kanisa zidi ya ulimwengu huu wenye kuwawinga Waislamu kwa jina la Ugaidi.
Hivi sasa Viongozi wa Kanisa Zanzibar ambao wengi wao ni wahamizi tu kutoka Upande wapili wa Muungano ,wameanza harakati na Mchaka mchaka wa kufanya kila mbinu na hila ili kuipaka Matope Zanzibar na watu wake kwa kudunia tecnic ya udini zidi ya Waislamu wa Zanzibar ambao wengi wao ni wenye dini hio yenye kulengwa na makafiri.
Hii imekuja kwa kasi hivi sasa Baada ya kuona Kanisa kuwa Serekali waitegemea ya Smz imepoteza mvuto kwa wananchi wa Zanzibar na kutokuwa na sauti zidi ya kuzidiwa na jumuia ya kislamu na mihadhara ya kidini uamsho kuwa ndio sauti ya Wananchi wa Zanzibar hivi sasa.
Kanisa lina hofu baada ya kuona huenda Chaka wajifichalo la Muungano na Srekali ya Smz huenda likafyekwa baada ya Wazanzibar kuja juu na kuukana hazarani Muungano.
Jee Muungano huu ni Laana au rehma kwa Zanzibar?
Uhakika Wazanzibar tufumbue macho tusiwe wanafiki mbele ya Allah , Muungano huu ni laana kumbuka Uislamu wetu na Mila zetu Wazanzibar zilivyo chafuka na kuto kujitambuwa kwa kuletewa kila laana na uchafu katika visiwa vyetu hivi?.
Kumbuka Makanisa yanavyo miminwa Zanzibar kila Chochoro na penu za nyumba?
Kumbuka Zanzibar hivi sasa Makanisa yanavyopata watu na kujaa ?
Kumbuka Madanguro na ndugu zetu kukopi utamatuni usio endana na wakizanzibar ambao ni uislamu?
Ndugu zangu yako mengi lakini sito yecha , hii yote imekuja kwa kufungua Mlango wa kuingia tiko kwa kisingizio cha kuwa Tanzania ni moja na haina dini na unaweza kuichi popote.
Jee nikweli Tanzania haina dini?
tukumbuke kuwa dini ya Tanzania ni Kanisa katoliki na ndio linaloweza kutowa kauli na Serekali ya SMT na viongozi wake wakafata na kunyeyekea Maskofu katika amri zao wazitowazo kwenye ma Hekalu yao .
Kwa upande wa Zanzibar hivi sasa Kanisa linaanza kuonyecha makucha yake Baada tu yakuona Serekali ya Umoja wa Kitaifa SUK sio ya ccm pekeyao na Baada yakugunduwa kuwa Jumuia za kislamu zimecha izidi nguvu ya Serekali kusikilizwa zaidi Tayari kanisa linaanza fitna na kutafuta mwega juu ya nchi za Mangaribi.
Wazanzibar viongozi wetu wa Smz hawaupendi Muungano kwa kuwa eti tumeingiliana watu wake no, Ni kuwa viongozi wana Intrest zao binafsi ndio ukaona hoja za viongozi wetu wa smz hazitafautiani hoja Zao.
Mulimsikia Mh Spika Kificho na wenzake katika ukusanyaji maoni ya katiba ,eti anasema kuwa tumejenga Tanganyika sisi wengine na kuwekeza , hii ndio faifda kubwa ya viongozi wetu?.
Jee Wazanzibar tuze Dini yetu na nchi yetu ilio vamiwa na Kanisa na chokochoko zake za kutaka kuihujumu na kuiponza kwa maduwi wa uislamu kwa hoja ya Kificho na wenzake?.
Hawa hata dini hawana wao ni tamaa ya mali tu na madaraka kwa kukiuza kizazi cha Zanzibar mbele ya maduwi wa uislamu.
Muandishi wa habari hii sijui wewe unaishi katika dunia gani hata ikawa hujui kwamba zanzibar imetawaliwa na inaendeshwa kwa rimoti kutoka Tangayika?
Kwa fikira zako unadhani raisi tulie nae hivi sasa ni chaguo la wazanzibari au unajitia hamnazo tu?
Tokea Zanzibar ilipoungana na Tanganyika ilipoteza maamuzi yake mpaka leo akitakacho tanganyika ndicho kinachofanywa na viongozi mamluki wanaoiongoza zanzibar, na wewe kama kweli unaishi zanzibar na angalau umeshafikia umri wa miaka 20 ulitakiwa usiulize masuala haya kwani hata watoto wa sekondari wanajua majibu yake.
Kama ulimsikiliza rais wa zanzibar alisema yeye ndie rais na ndie mwenye maamuzi ya mwisho, sefu 1 na sefu 2 ni washauri tu na wanapomshauri anahiari yake kukubali au kukataa.
Kama huelewi maadui wa zanzibar wanafanya kila aina ya vitimbi ili cuf akiwemo maalim seif wahamaki na watoke katika serikali ili wapate nafasi ya kufanya ubalaa ambao wewe hata katika akili yako huwezi kufikiria.
Mtu hata kama adui yako vipi hawezi kukutilia sumu katika juisi au katika maji wakati wewe mwenyewe umemsimamia (unamtazama) kwani anajua hakika hutoinywa.
Ndugu yangu au kaka yangu ingekua bora hayo masuala yako ukayaelekeza kwa rais kwamba huu ndio utawala wa sheria na haki za binadamu? au ukawauliza ccm kwamba haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania?
Mfumo kristo ambao umejengwa kwa takriban miaka 50 huwezi kuuondoa kwa siku moja, cha msingi wazanzibari sote tusikate tamaa na tuendelee kuitetea nchi yetu kwa pamoja badala ya kukaa na kumlaumu mtu mmoja. Nguvu zetu kwa pamoja ndio silaha na ushindi wetu pamoja na kumtegemea ALLAH JALLA JALALUH.
WABILLAHI TAWFIQ.
Mwandishi fuatilia zaidi ili upate kuandika makala yenye info za uhakika.
umesema
“Kama haitoshi, tumesoma kwamba kampuni ya kikristo ya AGAPE imepewa tenda ya kuuza ving’amuzi Zanzibar, lakini hakuna kumbu kumbu ya lini na wapi tenda ilitangazwa! Waziri wa biashara na viwanda ni CUF! Jee CUF watatuambia nini katika hilo?”
hii haihusiki na Wizara ya Biashara na Viwnda, hii ni masiliano kwahiyo hii inaenda aidha wizara ya miundo mbinu au wizara ya habari.
fuatilia zaidi ili uandike info za uhakika.
@Mwanafunzi, sasa kama serkali SMZ yaendeshwa kwa remote kutoka Tanganyika au Shein ndo kila kitu, kuna umuhimu gani CUF kuwemo kwenye serkali hiyo wakati hawana la maana wawezalo kufanya? Au ilimradi tu nasie tuwemo!
@Salem, ahsante kwa marekebisho….lakini kwani ikiwa inayohusika ni iwizara ya miundo mbinu au habari, mawaziri wa wizara hizo wanatoka chama gani? Sio CUF?!
Zanzibar siku atopatikana rais alochaguliwa na watu basi hapo mtasema ayo maneno yenu lkn mnajua vzr km mpaka sasa tunastahamiliana tu na uvumilivu lkn sasa tumefikia ukingoni kwani tulotegemea sio tuloyapata kua , angalau haki za binaadaam zitalindwa basi badili yake imekua hasara zaidi watu kufungwa bila hatia
Sina haja kusoma habari yote ni ndefu ila yangu ni kuhusu Leseni za Biashara na viwanda,hivi hamjui kama LESENI ZA BIASHARA NA VIWANDA NI ZA MUUNGANO au mmesahau hiyo ni moja kati ya kero? au pia mlisahau kesi ya Zantel?
Pili naungana na mwandishi ni kweli kabisa labda kama atatokea mtu atueleze hivi Mawaziri kazi zao ni nini hasa na wabunge mbona lawama zinaenda kwa mkuu wa mkoa na wilaya inaonesha mawaziri wao hawashuhuliki na lolote ila ni cheo tu.
Pia kama tutapata mchangiaji atutajie faida za kuwa na serikali ya kitaifa kwa wananchi ukiachana na mambo ya kudai Nchi nakusudia manufaa gani wananchi wa Zanzibar wamepata?
kwa kuwa nyota njema huonekana alfajiri wasi wasi wangu ni ule ule hata kama tutapata Zanzibar yetu still uchu wa madaraka na uroho wa fedha utaturudisha nyuma.
Kwa hakika CUF WAMO KWENYE MTIHANI MKUBWA. LAKINI KISIASA IMEPATIKANA FAIDA. ANGALAU BAADHI YA WANA CCM WMEFUNUA MACHO.
DHULMA INA MWISHO WAKE HATA WAKIJILINDA VIPI. MUHIMU WAZANZIBARI WAJITAHIDI KUDAI NCHI YAO NA WAMTEGEMEE ALLAH TU.
KANISA LINA TAPA TAPA KWA KAZI NZURI ILOFANWA NA MUUAMSHO.
IKO SIKU ZANZIBAR ITAKUWA HURU. NA HATUTOKUWA NA VIONGOZI WANAO CHAGULIWA BARA NA KUWA NA KUENDESHWA KWA REMOTE CONTROL.
@ Bablee
Kama wewe upo zanzibar unatakiwa uwe unazijua siasa za zanzibar zinaendeshwa na nani (rais anachaguliwa wapi, maamuzi makubwa yanatoka wapi, rais wa zanzibar ana wadhifa gani ktk tz, amiri jeshi mkuu ni nani, ikitokea tatizo dogo tu si anakuja waziri nchimbi kusuluhisha, na mengineyo mengi)
Kuhusu cuf kuwemo ktk GNU ni wananchi ndio walioamua kupitia kura ya maoni. Maadui wa znz wanaomba muungu muibadilishe ili ibakie ccm pekee ktk smz mukione cha moto zaidi kuliko hivyo unavyolalamika.
Kwa mawazo yangu mimi ni afadhali kuibana serikali ukiwemo ndani ya serikali kuliko ukiwa nje ya serikali.
Huu mfumo kristo umeimarishwa kwa miaka takriban 50, usidhani utauondoa kwa siku moja, na ndio maana tunatakiwa tuwe na subira, tumtegemee ALLAH, tuendelee kudai haki yetu kwa pamoja bila ya kuchoka.
@Bablee,,,,,,swali hilo ulilololiandika hapa jibu lake hata sijui litapatikana wapi kwani hata mimi huwa najiuliza hivo hivyo……kati ya moja nililokuwa nalitumainia kuwa sisi CUF viongozi wetu watakaposhiriki katika hii serikali itawabana hawa madhalimu wasijifanyie mambo kama vile Zanzibar haina wenyewe,,,lakini wapi, hali ndio imekuwa yakukatisha tamaa mara 10 zaidi,,ukiachia mambo ya uchumi imefika wakati CUF yangu inashindwa kuizungumzia haki na sheria,, niliyatanabahi haya pale walipokamatwa wanaharakati walienda nje ya baraza la wakilishi kutaka iitishwe kura ya maoni, kuvamiwa na kuharibiwa misikiti kule mahonda, kuuliwa mtoto kule Bububu,kutofanyiwa haki viongozi wa dini walioshikiliwa,tukio la mufti nk, Viongozi waliokwemo ndani ya hiyo serikali kimya, baadae hujitia hamnazo kwenda kuyazungumza mengine pale kibanda maiti, wakati kuna sehemu zake wanazijua pakuyazungumza lakini wanaogopa…..
@Bablee
Mimi nitakubaliana nawe kwamba CUF imo.
Lakini kama ni mchambuzi ,wenye upeo kuna mambo kadhaa uyazingatie.
- Sera zinazotumika ni za Chama Kilichoshinda. Haya ni makubaliano ya msingi kuundwa GNU.
- Chama kilichoshinda ni CCM, sera zake ndio zinazotumika
- Rais ni Dr Shein, Makamo wa Kwanza ni mshauri wake tu, ana khiari ya kukubaliana au kukataa usahuri.
Hata hivyo ndugu yangu BABLEE, kuna mengi huyajuwi yaliyoko Zanzibar. Na laiti ungeyajuwa ungesema mimi basi na UZANZIBAR. Hiyi nchi watu walikwisha gawana. Kuirudisha huko unakotaka kunahitaji Nguvu za malaika wema. Sikuvunji moyo lakini nataka tujuwe hali halisi ili tujipange kwenye ukombozi huu.
Nikupe mafanikio yaliyopatikana:
- Angalau kusikia wawakilishi japo kidogo kutetea maslahi ya wananchi.
- Kamati nne za Baraza la Wawakilishi zimeundwa kuchunguza dhulma zinazofanyika; kamati ya jumla (mawasiliano), kamati ya kuchunguza Manispaa, kamati kuchunguza Shirika la Umeme (ZECO), na kamati kuchunguza Ardhi.
Tumeshuhudia kamati ya kwanza taarifa yake manyago yaliyofanyika; angalau yule katibu mkuu, naibu wake, na wengineo wameondoshwa kwa manyago yao waliyoyafanya.
Kwenye ripoti ya manispaa tumeshuhudia manyago yaliyopelekea Mkurugenzi wake mwenyewe kukimbia Idara.
Tunasubiri ripoti mbili za ZECO na ARDHI, hapo hadi SHAMHUNA tumkate makende tukiendeleza lilelile la Bahari kuu. Haya ni baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa CUF kuwemo kwenye serikali ya GNU.
Mengine:
- Katika ziara za Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif, anazofanya zimepelekea wafanyakazi wengi kumfunga paka kengele kwa kueleza bayana udhaifu ulioko huko maofisini.
- Mawaziri wa CUF wametishia kujiuzulu ili kulazimisha kupatiwa fedha, na mwisho hupatiwa.
- Kuna bajeti nyingi wawakilishi walizizuwia hadi walipoingiziwa fedha kwa yale maoneo waliyodai.
- Kuna taarifa moja, Wizara ya Biashara ilituma maofisa wake kutafuta soko la karafuu. Walipofika waliamua kuziuza bei ya chini bila ya makubaliano na wazi wao. Waziri wa Biashara aliamuru maghala yafungwe, pesa zirudishe, na mwisho karipoti kwa Rais, aidha yeye abaki katibu aende, au yeye aende katibu abaki.
- Kwenye hilo sakata la AGAPE, hapo ni nguvu ya Waziri. Kwa taarifa yenu ilikuwa project hii ishachukuliwa mkopo wa 28 milioni dolas. Wakati kuna kampuni nyingi zingefanya chini ya 5 milioni dolas.
@BABLEE
Yako mengi ya kuyasema, sitaki niwachoshe. Tatizo ni lilelile kuna gap kubwa ya kupashana taarifa. Hatuna vyombo vya habari, hatuna waandishi, hatuna watoaji taarifa. Kwanza tujikomboe kwa hili. Tukifanikiwa hapa na kwengineko hakutakuwa na kipingamizi.
Binafsi sikuunuga mkono juhudi zile za UAMSHO, kwani tokea mwanzo nilisema faida ilikuwa ndogo kuliko hasara. Sasa hivi kanisa limeshapata power kubwa sana ndani ya Zanzibar. Umeshindwa kuizungumza hoja ya kuja makachera wa tanganyika kwenye mkasa huu.
Kanisa sasa hivi limeongeza nguvu yake kubwa hapa Zanzibar. Hata vipi UAMSHO kwa mbinu zile haifui dafu mbele yao. Na hili ndio walilokuwa wakitafuta.
Ndugu yangu Bablee sitaki uwe na akili ndogo ya samaki ambayo haimsaidii hata kutambua tofauti baina ya chambo na chakula. Ivi kweli wewe huelewi faida iliyopo kwa CUF kuwemo ndani ya GNU? Au ndio miongoni mwa wenye tender ya kuchochea watoke? Kwa tathmini yangu hawa hawatoki Ng’o. Toka nje ya sanduku na angalie na usilikize umma wa Zanzibar unasemaje na ulimwengu unasemaje kuhusu Zanzibar; Wanazungumzia Zanzibar kwanza ukitaka usitake!! Na kwa hili, nataka uelewe kuwa mambo haya sio ‘fixing nuts and bolts’, ni process inayohitaji fikra, mikakati, mass na uongozi bora. Nyenzo hizi zipo, na zaidi sasa ni wakati! Safari wameinza na hakuna ishara ya kurudi nyuma; na kama wewe humo ndani ya msafara utakuja kufahamu kesho na keshokutwa pale Zanzibar itapokuwa huru na yenye mamlaka yake kamili.
CUF wanaelewa fika kuwa mfumo uliopo wa Muungano ambao ndio unaathiri uwekaji na utendaji wa Serikali, nchi hii haitofika mbali kimaendeleo; na kuendelea kuchangia utendaji juu ya misingi mibovu ni kupoteza muda. Sasa elewa kwamba mapinduzi ya ajenda yaliyofanyika yatawafikisha huko kwa muda mfupi zaidi. Na hili halina mjadala InshaAllah. Subiri uone kama wewe si mshiriki. Nadhani akili imefunguka kidogo.
Wabillah taufik.
@Ashakh,
Suali la msingi kuna umuhimu gani wa CUF kushiriki katika serekali, ikiwa walijuwa tokea makubaliano ya awali kuwa chama kitachoshinda (kawaida ni CCM) ndio kitachoongoza serekali.Kwa maana CUF walijua kama executive hatokuwa makamo wa kwanza, bali ni makamu wa pili {imeandikwa wazi kuwa waziri kiongozi ataitwa makamu wa pili na kumfanya makamu wa kwanza awe ceremonial/asie na amri yoyote kama inavyoonekana}.
Mie nadhani tuache kujibabaisha huku na kule kwa ushabiki wa kisiasa, Bablee ana kila haki ya kuhoji na kuchakachua anachokiuliza.Kama nimemfahamu vizuri amevunjika moyo na matokeo au hizo faida zilizopatikana.Alitarajia angalau Amani na utulivu, leo tunashuhudia masheikh na wanyonge wakitwanga na kupea kichapo zaidi kuliko hata kabla ya GNU/SUK!…..Nadhani na CUF pamoja na wawakilishi ikijimazia kimya (sina uhakika na hili la ukimya wao)!
Kuna kila sababu ya kuvunjika moyo, ikiwa hata hii faida basic ya kuweza kukaa nyumbani kwa amani ukala mihogo na chai pia imekosekana ?
Mwisho nimalizie kwa kusema hao wawakilishi hadi leo wananchi tunajiuliza mswada wa kura ya maoni kujadili muungano uko wapi ? Nadhani ni majuzi kulikuwa na mzalendo ameleta makala kuhoji suala hili, ambalo hata nami sina majibu……nimebaki kunani ??? Inawezekana ikawa wawakilishi wamejitahid, lakini nina wasi wasi haitoshelezi!Tumeanza kujiuliza maswali ya msingi kama kweli wawakilishi wanafanya kazi zao kwa uadilifu au wabinafsi ?
@Mrfroasty
Leo kidogo nataka nikuvunjie heshma.
Najuwa kuna kitu kimekuchoma kwa ule msimamo wangu. Nimetowa hoja, ziko wazi, leo nashangaa kusema najibabaisha kwa ushabiki wa kisiasa.
Jee hizo hoja zangu nazo hazina mashiko?
Nashangaa pamoja na upeo wako bado unaomba “kura ya maoni”. Tukitaka kuididimisha Zanzibar na uwe mwisho wake ni kuleta hiyo kura ya maoni kwa mazingira tuliyonayo sasa.
Nasema wazi nitamshangaa Mzanzibar au mzalendo yoyote yule atakayediriki kulazimisha kupigwa kura ya maoni ndani ya mazingira haya. Huyo si mkombozi bali ni mzikaji wa Zanzibar.
@Mrfroasty,,,,,heywalaaaa, kisha sio Bablee peke yake, tuko wengi tulokata tamaa lakini Mwenyezi Mungu akatuletea Uamsho kidogo hawa madhalim wanajua kipi wazanzibari hatukitaki japo kua haitosaidia kitu lakini na sisi tutawakera tu,,zile ajenda zao za siri zote watazitoa hadharani mfano kama hii inayodhihirika sasa padri anathamani kubwa kuliko mashehe na mamuft,,(Allahuwakbar),,Cuf yangu imepoteza fursa ya hii miaka 10 na laiti wangeacha haya mambo ya sijui ya tume ya nini, sijui tume ya ardhi, badalayake angejikita kwa pamoja kupigania sheria na haki, basi hawa madhalim tungewazika 2015 ,, lakini wapi,,,ALFOLA,ALFOLA (ALFOLA BANDARI SALAMA) ALFOLA IMEKUFA,,,(IMEBAKIA MAFUPA)
Kuna mazingira gani ya kuogopa kura ya maoni wakati huu? Na kulikuwa na mazingira gani kuwepo kura ya maoni wakati ule?
@Sale
Hayo maswali yako yakumbuke, kwa leo mimi sitoyajibu, lakini kuna mtu atatokezea kuyajibu hivyo yakumbuke tu.
Jengine nakupa homework ikiwa upo Zanzibar yapime hayo mazingira yaliyopo. Laa ikiwa uko nje ulizia kwa wenye kujuwa.
@Ashakh,
Hoja gani unazitafuta mkuu na ukweli uko wazi tokea asubuhi (usaliti umezidi kupindukia), tulipiga kura ya maoni kutaka hio GNU na mazingira haya haya tuliyonayo wazalendo wakajikita na kampeni.Sioni kilichobadilika ndani ya miaka hio michache kuwa sasa tuwe defensive kusema kura ya maoni itakuwa kaburi!
Nadhani kura ya maoni kukana muungano itakuwa na support kubwa zaidi kuliko uanzishwaji wa GNU.Naamini fika kama Zanzibar iliingia ndani ya muungano kwa hiari lazima pia iweze kutoka kwa hiari.Angalau hicho ndio ninachokiamini au ninachotaka niamini.
Tujaribu kwanza….halafu ndio tujizonge kama haiweezekani.Bila ya kujaribu maisha tutabakia kupiga kelele za mlangoni.
@Ashakh labda ongezeko kubwa la watanganyika na watu kutoka nchi nyengine na wote hao wana lengo la kuinga mkono sera ya ccm,,(fikiria baada ya miaka mitano mengine)
Kwa ufupi jitihada za mtu hazihitaji kutafutwa Zanzibar tuna wabunge mabubu wamekaa tuu kule bungeni.Unamsikia Zitto Kabwe anatetea Zanzibar, tena wabunge wetu hata kupiga kofi kuunga mkono wanashindwa.Humo wamo CUF kila mtu anajichukulia mishahara anarudi kwake kula na wanawe.
Si lengo langu kujadili siasa kiasi chote hicho hicho maana hio sio proffesion yangu.Lakini nikiwa kama mwananchi wa kawaida utanidanganya sio mara zote.Ukweli utabakia pale pale jitihada za CUF na wanasiasa wote wa Zanzibar hazitoshelezi.
Nikisema hazitoshelezi nakusudia kwenye kutetea maslahi ya umma.Hapo ndipo linapokuja suala zima la muungano ambao kiukweli umebana maslahi ya wazanzibari (mara nyingi wanyonge).Wao ndio wanaolipa kodi mara dufu, wao ndio wanaokosa misaada yoyote ile hata ya kutoka nje.
Kiukweli ukimuuliza Pandu Kificho au Hamad Rashid, Balozi Seif, Samia Suluhu n.k hao wanazijua fika faida za muungano.Wanaweza kutajia orodha ndefu ambazo mtu mwenye akili yake zote zinamaanisha kitu kimoja tuu “FAIDA BINAFSI”.
Sasa ukweli tukubali kuwa CUF tokea kuingia madarakani imekuwa kama vile imemwagiwa maji.Imeacha haswa mwenendo wake wa kukemea maovu na madhila ya wanyonge.Huo ndio ujumbe unaobebwa na malalamiko haya.Kama watu wamejisahau wanahitajika kuamka na kuanza kupiga kazi waliotumwa na watu wende wakaifanye huko kwenye vyombo vya sheria.
Ndugu Yangu @ Bablee
swala la jibu lako ni hili kuwa Zanzibar noyo hivi sasa inaongozwa na mfumo Kristo viongoziwatendaji kwenda kuangukia Kanisa na kupata maelekezo ya Kanisa ndio ukaona Kanisa na Smz ila machirikiano makubwa.
Hii imekuja kwa nini?
Nikwakuwa Maskofu wakubwa wa Kanisa Katoliki ni watu kutoka Tanganyika na wamekuja hapa kwa ajili ya kueneza dini yao Zanzibar ambayo kipindi kirefu ilikuwa haijapata mwanya wa kukuwa Zanzibar kutokana na Pasenteg ya waumini na wenyeji wa zanzibar ni waislamu .
Sasa kanisa chini ya mwevuli wa ccm kuwa tanzania ni moja na haina dini ndio wamejipanga na kupata sindikizo la nguvu za nje ili kuja kuichafua Zanzibar kwa vile ina waislamu wengi.
Hofu ya kanisa hivi sasa ni nini mpaka ikawa wanakuja juu.
Hofu ya Kanisa ni Baada ya kuona mfumo wa serekali ya zanzibar sio ule wa serekali ya Tanzania Bara , Zanzibar haiongozi na mfumo kristo pekee (ccm) na cuf tayari wamechatia mguu wao .
Kwa hio Kanisa limeshushwa na kuona kuwa cuf tayari wamo ndani na hili hawakulipendelea wacha Kanisa tu Katoliki hata Watnzania Bara na viongozi wao walichukia lakini ndio ilikuwa no way kwa vile Wazanzibar walitumia silaha yao ya kujioganazi na kutowa mamuzi yao bila kuangalia itikadi za chama cuf/ccm.
Hapa Wazanzibar tulifanikiwa ingawaje lilikuwepo kundi ndani ya Zanzibar kutaka kuchafua hali hii lakini lilichindwa na nguvu ikawa kubwa.
Sasa kanisa ndio likanza choko choko za kuingiza chuki za udini na kuchukuwa kila kitendo cha hujumu na kuwaruchia waislamu wa Zanzibar ambayo ndio wananchi wa Zanzibar kwa %99 ya wakazi wake.
Na hili kwa kuto kutumia akili viongozi wetu wa ccm/smz wanachirikiana na Kanisa na kuwa Bega kwa Bega kukubali kuwa Zanzibar kuna chuki za udini na dini yenyewe hata watu wake ni wageni waliokaribishwa na wenyeji wa dini yenye kujengwa na waislamu %99.
Leo serekali hii yetu ambayo viongozi wake wote wa ngazi za juu mpaa rais ni waislamu wa Babu na Bibi na hajawahi kuwa Rais zanzibar mkristo lakini wamejiengemeza kwenye %0 na kuacha jamii ya Kizanzibar yenye % 99.
hii ndio Laana ya unafiki wa viongozi wetu , hivi sasa Kanisa lenye viongozi kutoka Tanganyika linakumbadiwa na Kunyeyekewa na huku Mashekhe wetu wakila mkumudo na kusekwa ndani kwa kisingizio tu cha kiudini kwa maelekezo ya chokochoko za Kanisa .
Kilicho wasibu Ma-Sheikh wetu sio chochote sio udini au kubaguwa ukristo kama sumu waipakayo ndani na nje ya nchi, kilichowasimu Mashekhe wetu ni Kutowa kauli za kudai haki ya zanzibar na kusema Muungano haufai.
Hii ndio iliowashtua kanisa na kuona sauti ya Mashekhe imepokelewa vidhuri na wananchi wa Zanzibar na kufanyiwa kazi sasa hapa ndipo walipo anza heka heka Kanisa na viongozi wake wa Tanganyika kuona huenda Kanisa likavunjika Zanzibar.
Maana hakuna asojuwa kuwa Muungano ni Kanisa na Kanisa ni Muungano, ukitaja Kanisa kwa Zanzibar inamana umetaja Muungano nikitu kimoja,
Sasa Maskofu na wao huona wenye kutaka kuvunja Muungano Zanzibar ni Waislamu maana wanachindwa kusema kuwa Wazanzibar hii haito sound vizuri kwao lakini wakisema waislamu basi itakuwa na nguvu na kwa vile wakaazi wa Zanzibar % 99 ni waislamu na uislamu unachukiza nchi nyingi za kubeberu basi ndio kanisa ika tumia mwanya huu ili kuipaka matope Zanzibar na watu wake.
Ndio matokeo yake hata viongozi wa ccm/smz wameingia katika dimbi hili bila kujuwa lengo la Badae la Kanisa Katoliki ni nini? %99 zote za wakazi wa Zanzibar zimekuwa (work done 0 ) wamekuja Mapadri kuja kuifundicha Smz vipi ifate kuwazibiti waislamu wa Zanzibar.
ikiwa Zanzibar inalengwa kwa udini hivi sasa Jee hao dini nyengine ina passentegi ngapi? hivi zote ni choko choko na Sumu za Maskofu na Wachukga wa Kanisa ambao sio Wazaliwa wa Zanzibar kuona kuwa Muungano ndio uliowaleta na uko hatarini.
Huundio ukweli wenyewe wanajuwa kusema kuwa waislamu wa Zanzibar wanadai haki zao au kusema matatizo ya Zanzibar ni yasiku nyingi kisiasa hili halinanguvu tena kwao.
Sasa wanaingiza udini kwa kisingizio cha Uamsho na hili limepokelewa na smz bila kujuwa mtego gani walioutega kanisa? Kanisa hivi sasa linalihujumu jina la Zanzibar na watu wake kwa njia ya tecnic za udini ili Zanzibar ipoteze sifa yake na ingizwe katika nchi zenye ugaidi watu wake.
Na kama Serekali yetu haikuchuka na kuwapa mwanya hawa basi amri itakuwa haitoki tena Tanganyika itatolewa vatikani na nchi za kibeberu na Wazanzibar tutachindwa kujijua ni watu gani sisi?.
Bada ya % 99 tutaonekana duni na kumezwa na %0 ya Wakazi wa Tanganyika na Maskofu wenye kumiliki makanisa ya Zanzibar kuyaongoza.
Tujuwe tu kuwa Zanzibar ikichafuka na kulengwa kwa jina Baya la kuwa kuna ugaidi wa kidini basi hawato pata hujuma wananchi wa Zanzibar pekeyao tu na hata viongozi hao wa Smz patawachinda Zanzibar kukaa na kustarehe na rasilimali zao walizo jikumbizia.
wasome kutokana na nchi zilizokoseswa utulivu kwa jina la ugaidi na kufunga magaidi, wawawashe Maskofu waipake matope Zanzibar kwa agenda yao ya kukosa nguvu ya kuwazibiti wazanzibar halafu tuangalie matokeo yake?
Huyu Seif Iddi ni hatari kwa jamii tuwaulize hawa hawa ccm/Smz wana nini gani hasa ? ikiwa wanakumbatia Kanisa na kuwatesa ndugu zao kusota Gerezani na kuwapa hilaki ,jee wao ni waumini wa dini gani?
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/377691-zanzibar-sasa-hali-ni-tete.html#post5355505
@Ashakh (Kiongozi)
Kamanda kwanza ni kushkuru sana kwa majibu yako mazuri! Ndo maana nkaleta swali hili ili na sisi wengine tujuwe! Lakini nimeona tatizo jengine; Kuna kasoro katika upatikanaji wa taarifa za mafanikio na utendaji wa viongozi wetu! Katika zama hizi za utandawazi sitegemei madudu kama hayo yaliyofanywa na katibu wa wizara ya Biashara kubakia kuwa siri ya serkali. CUF au SUK imeendelea kufanya mambo kwa kujificha/sirini. Huo sio aina ya uongozi wa karne hii!
Wananchi wa kawaida hawawezi kupima uwajibikaji wa CUF kwenye SUK kwa kuangalia tume zilizoundwa kuchunguza kashafa za ubadhirifu ilhali wanaona askari wakiendeleza ubabe wakuwatesa na kuwapiga wananchi bila sababu, wanaendelea kuona dhulma watu wakikamatwa na kuteswa magerezani huku wakinyimwa haki zao za msingi kama binaadam wakawaida! Ni lazima CUF wasimame na kujipambanuwa na aina zote za dhulma zifanywazo na CCM kwenye kivuli cha SUK ! Hata kama sera zinazofuatwa ni za CCM, bado CUF wanaowajibu wakupinga dhulma au utendaji mbovu usiokuwa na uzalendo kwa nchi yetu, hakuna sera ya chama hata kimoja unayotetea hayo!
Ama kuhusu nguvu za viongozi wa CUF akiwemo makamo wa kwanza wa rais, hapa nililiona tatizo la msingi katika uundwaji wa SUK! Makosa yaliyofanywa na Karume na wenziewe kwenye kuungana na Tangyika, ndio yaliyorudiwa na CUF (maalim seif na wenzake) kwenye kuunda SUK!
Pamoja na umuhimu wa kuepo SUK, lakini kitendo cha kukubali mgawanyo wa mdaraka uishie kwenye ngazi ya uwaziri tu na makamo wa rais awe ni mshauri tu (hana nguvu yoyote kiutendaji) hili ni kosa ambalo CUF linaigharimu sasa! Lakini kosa jengine ni kutoainisha ndani ya katiba kikomo au muda wakurudi tena kwa wananchi kuwauliza kama wanataka iendelee kuepo SUK au la!
Kwani kwa aina hii ya SUK, ndugu yangu Ashakh, si kipindi kirefu wananchi wengi wasionaguvu kwenye serkali hii wataanza kulalamika, hili nalo litageuka kuwa kero la wazanzibar! SUK ipo kikatiba hivyo nakuitoa kwake itakuwa ngumu (kunahitaji mchakato mkubwa na kwa matakwa ya wenye dola) kama ulivyo muungano!
Lishalovunjika ni gae, kwa hivi sasa viongozi wa CUF walio serkalini watumie mikutano na vyombo vya habari kuileza jamii kinaga ubaga nini wanafanya, mafanikio, na challenges wanazokutana nazo katika utendaji! Hili litafufanya sisi wengine tusiojuwa hayo ya sirini (kama uliyoyaandika hapa Ashakh) tuweze kuwa “evaluate” na kuona umuhimu wa kuwepo SUK! Kwa sababu kipimo pekee cha raia wakawaida juu ya utendaji wa serkali yake ni kuona hali yake ya maisha inatengemaa (improve), anapata haki zake za kisheria, anaheshimiwa badala ya kunyanyaswa na pia anasikilizwa! Hayo bado hatujayaona sisi raia wakawaida, hivyo CUF inapaswa watujuze hayo mengine yanayohitaji uwe sehemu ya wenye siri, uchambuzi na utaalam!