CUF HAITOKUBALI KUSULUHISHWA NA KIKWETE ALIEWADHULUMU WAZANZIBARI

Written by  //  20/04/2017  //  Habari  //  Maoni 6

CUF HAITOKUBALI KUSULUHISHWA NA KIKWETE ALIEWADHULUMU WAZANZIBARI

MSULUHISHI WA KIMATAIFA PEKEE NDIO TUTAWEZA KUZUNGUMZA NA CCM
KUTATUA UHUNI WA CCM KUVURUGA DEMOKRASIA.

Na Ismail Jussa Ladhu; Nimesoma makala iliyoandikwa na Ndugu Deus Kibamba akimuomba Rais Dr. John Pombe Magufuli amteue mtangulizi wake, Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa msul uhishi wa mgogoro wa Zanzibar.
Wakati naunga mkono kuchukuliwa hatua madhubuti za kuumaliza mgogoro huo wa uchaguzi (ambao naamini suluhisho lake ni kuheshimu maamuzi halali ya Wazanzibari waliyoyafanya kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015), kabisa siungi mkono pendekezo la Ndugu Deus Kibamba kwamba eti JK ndiye apewe dhamana hiyo.

Kwa vipimo na vigezo vyote, Jakaya Mrisho Kikwete hana sifa, hana uadilifu, hana uthubutu, na hana uhalali wa kushughulikia mgogoro wa kufutwa matokeo halali ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

Kwa msingi upi ataweza kulishughulikia suala hili? Ingekuwa ni kusimamishwa kizimbani, yeye atakuwa wa kwanza. Ni yeye Jakaya Kikwete akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu ndiye aliyesimamia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu halali ambao ulikuwa umeshamalizika. Jeshi lisingeweza kupelekwa Hoteli ya Bwawani kulikokuwa kituo kikuu cha majumuisho ya matokeo ya uchaguzi wa Urais wa Zanzibar bila ya idhini ya Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa hakika, amejipotezea heshima kubwa ambayo angekuwa nayo kama angesimamia matakwa ya kidemokrasia ya wananchi wa Zanzibar. Badala yake akaamua kuyavuruga MARIDHIANO YA WAZANZIBARI kwa kuwakorogea uchaguzi wao uliopaswa kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoasisiwa na Dr. Amani Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad. Hiyo ndiyo LEGACY yake kwamba anakumbukwa kwa kuichafua Zanzibar na kuiingiza katika mgogoro mkubwa kuliko yote iliyowahi kuvikumba visiwa hivi.

Hata pale alipopigiwa simu kupitia namba yake binafsi na mshindi wa uchaguzi ule kwa nafasi ya Rais wa Zanzibar yaani Maalim Seif Sharif Hamad ambaye akimtafuta ili waonane kuzungumzia hatua ile ya kufuta matokeo ya uchaguzi akawa hapokei simu. Akaandikiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu. Akaandikiwa barua rasmi kuombwa wakutane hakujibu.

Yote alikuwa kayapanga vyema. Akamuita Maalim Seif siku moja kabla ya kuapishwa Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais. Na pamoja na hayo Maalim Seif hakuwa na kinyongo (kama kawaida yake) na akaitikia wito. Kumbe alimwita kwenda kumfanyia istihzai. Maana baada ya Maalim Seif kumueleza na kumpa ushahidi wa fomu halali za matokeo ya uchaguzi zikionesha kwamba yeye ndiye mshindi, jawabu la JK likawa kwamba amebakiza saa 24 tu kabla hajakabidhi madaraka na kwa hivyo asingeweza kufanya chochote.

Maalim Seif alimwambia humtendei haki mrithi wako, Rais Dr. John Pombe Magufuli, kumwachia mgogoro huu wakati ndiyo kwanza anapokea madaraka lakini hayo hayakumshughulisha JK. Yeye alitaka apige picha tu na Maalim Seif ili azitumie kuihadaa jumuiya ya kimataifa kwamba alijaribu kabla hajaondoka madarakani. Bahati nzuri, jumuiya ya kimataifa ilimshtukia! Haikuwa ajabu pale Taasisi ya Mo Ibrahim Foundation ilipomnyima tuzo ya Rais bora Afrika kwa kutoheshimu kwake misingi ya demokrasia na utawala bora.
Ndugu Deus Kibamba yuko sahihi kwamba mgogoro wa kufutwa matokeo halali ya uchaguzi halali wa Zanzibar unapaswa kutatuliwa, na mimi naamini utatatuliwa na kumalizika, lakini Jakaya Kikwete siye wa kumpa jukumu hilo wakati yeye ndiye mvurugaji wa yote.

WACHA HISTORIA IMHUKUMU.

fb

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 6 katika "CUF HAITOKUBALI KUSULUHISHWA NA KIKWETE ALIEWADHULUMU WAZANZIBARI"

 1. moyo 20/04/2017 kwa 7:17 mu ·

  Viongozi wa cuf kama sio waongo basi hawaeleweki, huyu jussa nae asema anakubali usuluhishi! Usuluhishi wa nini na kumebaki masaa tu kukabidhiwa haki yetu tulioporwa!

 2. shawnjr24 20/04/2017 kwa 11:06 mu ·

  Amani Abeid Karume tu ndie namkubali kwa kuleta suluhu lakini walobakia unafiki na BT umewajaa.

 3. Awami 20/04/2017 kwa 3:19 um ·

  Nitajikita moja kwa moja kutowa kuchangia maoni yangu, Deus Kibamba ametumika kama vile wazungu wanaposema ni platform kufikisha ujumbe ili waliomtuma waone jinsi gani wahisika watakavyo ingia katika hilo ,kwani waliomtuma wanajuwa fika raja kuwa nini walikifanya huko nyuma ,na huyu Deus Kibamba kuna uwezekanao amri aliyopewa hakuwa na uwezo wa kuikata kwani kama tujuwavyo Tz sasa inarudi kinyume nyume kwa maneno ya kizamani ni mithili ya kaa Dondo wa baharini anapokutana na taharuki akiwa mwendoni .vile vile inawezekana Deus Kibamba ametimiza magizo aliyotumwa kwa kuogopa kuja kuambiwa atatafutiwa kijij cha asili yake atokako kule mozambiki na kurudishwa ,.

 4. chatumpevu chatumpevu 20/04/2017 kwa 5:57 um ·

  Naunga mkono mawazo ya wote waliochangia hata mtani wangu moyo kwa staili yake ya uandishi wa kebehi na istihzai. Binafsi. Deus kibamba Ni Rafiki yangu wa karibu tokea kabla hajawa mratibu wa jukwaa la katiba. Anapenda Sana siasa za zanzibar na hapendi dhulma ktk ulingo wa siasa. Lkn kwa hili la yeye kumpendekeza kikwete kuwa msuluhishi wa mgogoro wa Znz siungi mkono mawazo ya Deus. Kama alivyosema jusa Kikwete ndo alosababisha sintofahamu hii na akamlazimisha baradhuli Jecha salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi na akajitiia kimaso maso cha kuwa eti hahusiki. Deus kibamba yte anayajua hayo tulishazungumza hapa na pale. Kwa mawazo yngu angetafutwa msuluhishi kutoka nchi ambazo zinafanya vzr ktk demokrasia kama vile Ghana au Senegal lkn sio huyu kikwete ambye akipewa role hiyo atakuwa kma mchezaji na wkt huo hip mi mwamuzi. Hafai kupewa jukumu hilo. Bora Malaya wa uwanja wa fisi angetenda haki lkn sio kikwete. Yafaa ifahamike kuwa hakuna mtanzania yoyote angetenda haki ktk kupatikana kwa suluhu ya mgogoro huu ambao ni wa makusudi. Pengine Mzee warioba ingawa na yy ni wa chama kilichoiba kura lkn unaweza ukafikiria kuwa anaweza kutenda haki.

 5. albany 21/04/2017 kwa 4:36 um ·

  Kama amekosekana msuluhishi wa mgogoro huu uliotengenezwa na hawa walaff wa madaraka(ingawa naamini wapo watu wazuri), basi ni heri ateuliwe rais mstaafu wa Gambia Yahya Jameh kuliko huyu Kikwete .KIKWETE HAFAI HAFAI HAFAI.

 6. Mzambarauni Takao 23/04/2017 kwa 4:47 mu ·

  Aliyoyafanya Kikwete ni kwa kukhofu Bara, Zanzibar itawaponyoka. Kwani angepewa uraisi Maalim Seif CCM Zanzibar wangeuliya na chuya. Wasingeshinda 2020,2025, …….Wasingeshinda chaguzi teeena. Na jinsi sasa mambo yanavoendeshwa kidikteta Tanzania Bara na Pombe ni uharo na kutu tupu.
  Kwa utabiri wangu sidhani huyu Pombe Chibuku atashinda 2020 hata kwa goli la mkono. Wabara keshawakwama kwenye vidaka tonge hawamudu hata kutiya rizki kinywani.
  2020 Raisi ni Mhe. Tundu Lissu Tanzania Bara na Zanzibar ni Maalim. Hapo kuna uwezekano wa mawili:

  1. Zanzibar kujitowa katika huu muungano wa kivamizi wa kidhulma wa kulazimishwa ukitaka usitake. Na hili CCM kwao ni mwiko. Ndio maana huyo ayyaari JK alipokwenda Maalim Seif kuonana naye alimwambiya, ” Maalim wanakuogopa usije ukavunja muungano” Hawo walokuwa wanamuogpa ni nani? Isipokuwa mnafik. Si angelisema direct tu, sikuachii uraisi Zanzibar kwa sababu najuwa utauvunja muungano period.
  2. Kupatikana Muungano wa Mkataba wa kifederalia between two sovereign countries kwa kila nchi na mambo yake ya nje na ndani bila kuingiliwa na na central Federal Gov’t. Na kuwepo vipengele katika Mkataba huu vya kuipa nchi shiriki uhuru wa kujitowa ( power of cessation)katika hiyo federalia.
  Naamini iko siku Zanzibar itakwamuka kutokana na makucha ya mwewe aitwaye Tanganyika. It’s just a matter of time. The time BOMB is ticking.

Comments are now closed for this article.