CCM: Tupo tayari kukaa meza moja na CUF

Written by  //  14/04/2017  //  Habari  //  Maoni 9

CCM: Tupo tayari kukaa meza moja na CUF

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdalla Juma Abdalla

CHAMA Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimesema kipo tayari kukaa katika meza moja na Chama cha Wananchi (CUF) kwa ajili ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho na sera zake kwa mwaka 2015-2020, lakini sio kujadili suala la uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 ambao ulifutwa na Tume ya Uchaguzi (ZEC) kwa mujibu wa sheria.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdalla Juma Abdalla maarufu Mabodi, alisema hayo wakati akizungumza na ujumbe kutoka Marekani ukiongozwa na Ofisa wa kusimamia masuala ya sera za kijamii na kisiasa Ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Gregory Simpkims, katika Ofisi Kuu Kisiwandui mjini Unguja.

Dk Abdalla alisema Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 ulifutwa na ZEC baada ya kujitokeza kwa kasoro mbalimbali na ndipo ulipoitishwa uchaguzi wa marudio Machi 20, 2016.

Naibu Mkuu wa CCM Zanzibar alisema maamuzi yaliyochukuliwa na Tume ya uchaguzi kufuta Uchaguzi Mkuu yalikuwa halali kwa sababu ndiyo chombo kilichopewa mamlaka hayo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

“Msimamo wa Chama Cha Mapinduzi upo wazi ni kwamba ipo tayari kushirikiana na Chama cha Wananchi kwa ajili ya kutekeleza Ilani ya CCM pamoja na sera zake kwa maslahi ya wananchi, lakini sio kukaa pamoja kujadili Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 ambao ulifutwa,” alieleza Dk Abdalla.

Alisema ujumbe huo kwamba Serikali ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein inaendelea na majukumu yake ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi na ustawi wake kwa ujumla.

Alisema mambo makubwa yamefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja tu kipindi cha pili cha uongozi wa Dk Shein ikiwemo kuanzisha pensheni kwa wananchi waliofikisha umri wa miaka 70 huku uchumi na ukusanyaji wa mapato ukiimarika kwa kiwango cha kuridhisha.

Naye Ofisa kutoka Marekani, Simpkims alisema wameridhishwa na kasi ya maendeleo iliyofikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kusema nchi hiyo ipo karibu zaidi kusaidia miradi ya maendeleo.

Alisema mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na ukomavu wa CCM katika kuongoza na uzoefu wake kwa kuwa na viongozi wenye busara na hekima kubwa.

“Marekani imeridhishwa na juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza ahadi zake kwa wananchi zinazotokana na kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 wa kampeni kwa wapiga kura na ndiyo maana sisi tupo tayari kushirikiana na Zanzibar,” alisema.

Ujumbe huo miongoni mwa masuala uliotaka kupata ufafanuzi wa kina ni kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mazungumzo ya kuleta muafaka wa kisiasa kati ya CCM na CUF ambao ulitokana na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 ambao ulifutwa.

FB

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 9 katika "CCM: Tupo tayari kukaa meza moja na CUF"

 1. Calif 14/04/2017 kwa 12:47 um ·

  Kumbe mnajua kuwa BWANA ni BWANA tu ata akikulisha mwaka mzima bado ni BWANA wako tu.
  Shwain nyi nyi em nyi

 2. Calif 14/04/2017 kwa 12:53 um ·

  Ajenda na mjadala ni uchaguzi na wizi mlioufanya kwaio sisi tutashiriki kujadili hilo wala sio sera za ccm

 3. shawnjr24 14/04/2017 kwa 4:15 um ·

  Sasahivi ndio wanataka kukaa meza moja na cuf na kuongea.
  Sasa kuongea nini? Cuf wao wanataka kuongea kudhulumiwa kwa haki yao. Au mnataka kuongea na cuf ya Lipumba na kuwaridhisha marekani?
  Kama mimi kiongozi wa chama cha cuf basi kwanza ningeomba aletwe Jecha na kuelezea sababu na hitilafu zilizofanya hata uchaguzi aufute. Ingawa mimi naamini tanganyika ndio walioamuru majeshi kumzuwia na kuufuta uchaguzi.

  Swali nje ya hii mada:-
  Kwanini cuf hawapendi kufungua kesi mahakamani wakati chadema kutwa wanafungua kesi, pindipo wakiona wame dhulumiwa? Au hii ndio moja ya sera yao?

 4. Wamtambwe 14/04/2017 kwa 4:49 um ·

  @shawnjr24
  Katiba inasema Uchaguzi wa Raisi hauwezi kujadiliwa Mahakamani. Mbona hao chadema hawakufungua kesi kwa matokeo ya Uraisi?

  • shawnjr24 14/04/2017 kwa 8:35 um ·

   @wamtambwe
   Sawa kuhusu matokeo ya rais. Lakini vipi kuhusu Jecha kuufuta uchaguzi? Kwanini hawakufungua kesi ya kuzuwia kurejea kwa uchaguzi mpaka aweke ushahidi wa kuufuta.

   • Wamtambwe 15/04/2017 kwa 10:20 mu ·

    @Shawnjr24
    Unataka kunambia Zanzibar kuna Mahakama au Jaji anayeweza kuisimamia kesi kama hii?

    Usilinganishe Tannanyika na Zanzibar, Hapa Zamani Zanzibar ndio ilikuwa ni kitovu cha Elimu, Ustaarabu na Uadilifu.
    Wale tuliokuwa tukiwatuma Zamani kulimia mikarafuu, sisi wametutia Umaskini, Ujinga, na Unafiki na hivi sasa wameshatuzidi kwa Kila kitu

 5. salali 14/04/2017 kwa 5:50 um ·

  Habari za ujio wa ujumbe wa Marekani Babu Ali kaufyata sababu ccm na CUF walisha kaa vikao visiopungua kumi sasa leo tena mnataka kutuzidisha kwenye vikao yanini wakati uchumi wenu unakua. Mmuache Maalim Seif Sharif Hamad na diplomasia yake hakuna tena manusra kama nyinyi ni nguruwe mloinajisi politik mtazidi kujitekenya wenyewe.

 6. abuu7 14/04/2017 kwa 7:45 um ·

  tushakaa mpaka matako yamekufa ganzi. ccm mnaomba toba kiujanja wakati mnaona mwezi mtukufu wa Ramadan unakaribiya. wazanzibar washakutoweni kwenye imani.mnanuka zambi

 7. Mfalme 16/04/2017 kwa 6:52 mu ·

  It is enough that the people know there was an election. The people who cast the votes decide nothing. The people who count the votes decide everything .”Joseph Stalin”

Comments are now closed for this article.