BREAKING NEWS: Mswada wa Umiliki wa Mafuta/GAS Wapelekwa Bungeni Kinyemela.

Written by  //  04/04/2017  //  Habari  //  Maoni 9

Asalamu Aleikhum ndugu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa vyetu adhimu. Na Habari zenu Nduguzetu (Majirani zetu) Watanganyika na wasomaji wote wa Mtandao huu.

Nduguzangu wa ZANZIBAR na TANGANYIKA, hii ni habari nyeti Kuhusiana na Umilikaji wa Rasilimali Yetu ya Mafuta na Gas kama Wananchi halali wa Tanzania. Tuna haki yakujuwa Suali la Umilikiji wa Rasilimali ya Mafuta na Gas ya Zanzibar na ya Tanganyika. Hata hivo suali hili sasa linafikia pabaya sana kwa pande zote mbili za Muungano- hasa baada ya Serikali ya CCM- MAGUFULI kulitaka Bunge kupitisha Sheria hio ya Umilikaji wa Mafuta na Gas haraka sana. Na wamefika mbali zaidi pale walipotoa siku mbili tu na kutoruhusu Wabunge hao kuijadili kwa undani Sheria hio inayosemekana kwamba ina Vifungu zaidi ya 30 na vitoto vyake zaidi ya 200. Inasemekana na Wataalamu wa Sheria kwamba, Zanzibar na Wazanzibari wameachwa SOLEMBA.

Jambo la muhimu, tunapaswa tujuwe kwamba makala hii inamuhusu kila Mtanzania aliekuwa Mkubwa na Mdogo, Muislamu, Mkristo au hata asiekuwa na Dini. Mtanganyika na Mzanzibari yoyote basi anafaa ajuwe sheria inayomiliki rasilimali ya Nchi yake; itawafaidisha wananchi hao na si vyenginevo. Ndiomaana nikasema hapo juu kwamba makala hii ni muhimu kuisoma na kuifahamu ili tupate kusimamia lile ambalo Wabunge Wa Upinzani wameliona kuwa sio halali. Pia tunatakiwa kuwaunga mkono wa hali na mali Wabunge wote wa UKAWA au hata wa CCM kama wataamua kuungana na Wabunge wenzao wa Upinzani; na kuitetea haki. Hivo Wito wetu kwa Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar, ni wajibu wetu sisi RAIA, kuwabana Wabunge wetu wasikubali udhalimu na mazoea ya CCM wa kutaka kupora rasilimali za Wananchi. Tunatakiwa tuwe tayari hata kuandamana Nchi Nzima ikiwa Sheria hiyo itapitishwa kinyemela bila yakuzingatia matakwa ya Wananchi wa pande zote mbili zilizounda Muungano huu.

Bila yakutafuna Maneno ninaona bora nianze na mada niliokusudia baada yakurushiwa Video ambayo Mh. Tundu Lissu na Wabunge Wenzake wa Upinzani Wametoka Nje ya Bunge (As I Speak) Kukataa Kutoukubali Muswada wa Rasilimali ya GAS na MAFUTA ambao umepenyezwa Bungeni leo tarehe 04. April 2017. Lengo nikuukubali Muswada huu kuwa Sheria rasmi ya “Umilikaji wa Mafuta na GAS”.

Tunaweza kujiuliza, kwanini Sheria hii Imepenyezwa haraka haraka hivi?

1. Wabunge Wapewa siku 2 tuu (Ati) wapitishe Sheria ya Umilikaji wa Mapato ya Mafuta na GAS.

2. Sheria haina Uwazi, Uwajibikaji, na haki.

3. Zanziba hawana hakki ya kumiliki rasilimali zao.

1. Wabunge Wapewa siku 2 tuu (Ati) wapitishe Sheria ya umilikaji wa Mapato ya Mafuta na GAS.Sheria ina vifungu 30 na vitoto 200.
Sheria Nyeti zinazohusu Mapato au Rasilimali ya Taifa, hazitaki kufanyiwa haraka kama bunge lilivo agiza. Lakini haya yote yamepangwa hivi kiu-janja ujanja makusudi, ili CCm Tanganyika na CCm SMz wamaliziane makubaliano yao yakuuza Zanzibar na Wazanzibari. kwa upande wetu Wazanzibari hatushangai kuona muswada huu unapitishwa kinyemela au haraka haraka hivi. Huo ni uendeleaji wa uporaji wa mamlaka na rasilimali za Wazanzibari kwakutumia Bunge na Sheria. Na hata kama Wabunge watapewa Mwezi mmoja kuipitisha sheria hii. Wazanzibari tunaamini Wabunge wa CCM-SMZ hawana uwezo wakufahamu Sheria, kutokana na ukosefu wao wa elimu na ukereketwa wao wakubakia madarakani hadi kifo kiwashukie.

Sio hivo tu, sheria nyingi zilizoandikwa na Serikali ya Tanganyika hazikuandikwa kwa ufanisi au haziko (comprehensible).Tumeweza kuwasikia wanasheria wetu walio bobea, wakifafanua vifungu vya Rasimu ya Katiba na kuna siku walimfahamisha Mh. Hamza (Muwakilishi wa Kwamtipura) kuhusina na sheria ya Mafuta na GAS, na kumwambia ( Hamza) kwamba CCm hawakuifahamu vizuri sheria hii ya Umiliki wa mafuta na Gas, isipokuwa wanaichukulia so sipmle. lakini kama ilivo kawaida ya wawakilishi na Wabunge wa CCM – SMZ. Wazanzibari tunajuwa wapo hapo kwa ajili ya Matumbo yao na familia zao – na kuwafurahisha mabwana zao ambao wamewaweka na kuwalinda katika madaraka haramu.

Pili tunawaomba Wabunge wa CCM na CUF kutoka Zanzibar, waache tofauti zao na wasimamie maslahi ya Nchi yao na rasilimali zake. Hivo wasikubali kupitisha sheria yoyote ile iliokuwa imekiuka matakwa ya Wazanzibari au iliotoka nje na ile Rasimu ya Katiba ya Warioba.Kwasababu Rasimu ile ilishaweka wazi kuhusu Utafutaji, uchimbaji na umilikaji wa suali la Mafuta na Gus; kuwa kila Nchi itamiliki rasilimali zake. kwanini CCm wafanye dhulma hii? mpaka lini dhulma hii itafanywa na kuongeza matatizo ya Muungano? Kama Serikali ya CCm Tanganyika ni waungwana kweli, basi Tanganyika wamiliki rasilimali zao na Zanzibar hivo hivo.Dhulma na udanganyifdu mulioufanya 1964 unatosha.

Nataka wazalendo muelewe kwamba hakuna la ajabu kwa Nchi zilizoungana kumiliki au kusimamia rasilimali zake wenyewe kwa ajili ya manufaa ya wananchi wake.Tunaweza kuangalia mifano mizuri ya Miungano ya wenzetu, kama vile muungano wa UK, EU na Scandanevia. Nchi hizi zina miuungano mzuri sana ambayo umedumu kwa miaka 50 na upuuzi. Lakini kila nchi inamiliki rasilimali zake. Hata passport kila mtu ana yake na sio kila kitu kutiwa katika KAPU la Muungano, kama wanavofanya hawa ndugu zetu wa damu.
Leo Vyama vya upinzani wameshutukia uharamia huu, lakini sisi tunaamini sheria hii inaweza kupitishwa tena kinyemela bungeni na kutakiwa wabunge wa CCm watupu waipigie kura. Tayari tumeona ile Rasimu ya Warioba ilivotiwa kapuni na kuletwa Rasimu ya CCM-CHENGE 2014. tuliweza kuona uharamia na unyama wa CCm walivo pitisha vifungu vya Rasimu hio na kuwapigia kura hata maiti na Mahujaji waliokuwa hawakuwa na access au hawakuhudhuria Bungeni. Samuel Sitta (laaghana tullah) aliwapa kura za bandia na kutuzomea Wazanzibari, naamini dhulma zake alizozifanya sasa anapata malipo yake huko kaburini aliko.

2.Sheria haina Uwazi, uwajibikaji na haki.
Hata kama CCM wanasema Sheria ina Uwazi na Uwajibikaji ktk “UMILIKAJI wa Mafuta na GAS”. Sisi Wazanzibari tunaamini kwamba Serikali ya CCM Tanganyika haiwezi kufanya Haki kwa Zanzibar wala wazanzibari, (let alone) rasilimali za Zanzibar. Mipango hii ilipikwa tokea zamani na kufanya juu chini ili CCM- Zanzibar ibakie madarakani hata kama hawakushinda uchaguzi. Kwasababu tayari kuna kundi la CCm ndani ya SMZ wameahidiwa nafasi kubwa kubwa za vyeo, na ndio maana wakafuta matokeo ya uchaguzi halali wa 25.oct.2015. Jengine liliowafanya Wabunge wa Ukawa wawe invigilant ni kuogopa kufanya
makosa ambayo yalishawahi kutokea hapo nyuma. Kwa mfano:-

Serikali ya CCM- Tanganyika mwaka 1997, ilipitisha mikataba ya Sheria ya umilikaji wa Madini ya Tanganyika. Na sheria hizo zilipitishwa haraka haraka kama inavotaka kupitishwa sheria hii ya Mafuta na Gas. Mwaka 1997, CCM ilipitisha Sheria ya Uwekezaji haraka haraka yakutaka Bunge kufuta Kodi kwa Wawekezaji wanaoingia Tanzania/ Tanganyika. Hizo ni akili kweli? mbona waafrica wanaoekeza Ulaya au nchi nyengine za jirani hawasamehewi kodi? Hivo kupelekea kuiona Tanzania tajiri kwa Madini na rasilimali nyengine- lakini wanaofaidika ni wawekezaji wa Nje na viongozi wa CCM na familia zao tu.

Mh. Tundu Lissu anasema walipiga kelele sana na kulitaka Bunge hilo na Serikali ya CCm wawaletee Sheria hizo za 1997/1998, Lakini Chakusikitisha Serikali hii hii ya CCM na Bunge hilo hilo lilikataa kufikisha Sheria hizo Mbele ya Bunge na kujadiliwa upya. Tundu Lissu anasema wameamua Sheria hii ilioletwa jana ya Mafuta na Gas, hawataipitisha haraka bila ya kuijadili. Hivo itakuwa wanarudia Makosa kama yaliofanywa 1997 na 1998.Sasa ikiwa serikali ya CCM na Viongozi wa Tanganyika wameweza kuwadhulumu Wananchi wao wa Tanganyika mamilioni ya fedha au mapato ya rasilimali zao; watashindwa kutufanyia sisi Wazanzibari wanao tutatawala kijeshi na wanaotuchukia?

Wazanzibari wanaamini sheria hizo zote za umilikaji na ufutaji wa kodi, haukufanywa kwa bahati mbaya. Kama tunavojuwa Viongozi wa CCM ambao walikuwa madarakani wakati huo walifanya hayo kwa kuangalia maslahi yao Binafsi na sio maslahi ya Wananchi au Taifa lao.Tunaweza kusema,Serikali au kiongozi yoyote yule anae saini mikataba mibovu, basi ujuwe na yeye anafaidika katika mikataba hiyo.

3. Zanzibar Hawana Haki yakumiliki Rasilimali zao.
Dr Sheni na Genge lake wamewadanganya Wazanzibari pale alipojidai (Ati) Wanaanza mchakato wakutafuta Mafuta na GAS. Kwa mujibu wa Wanasheria wa Zanzibar, Sheria ya Mafuta na Gus inaonyesha kwamba bado ni Mali ya Muungano. Ndio Sheria hio sasa inatakiwa kupitishwa haraka haraka au (Kinyemela) kwa muda wa siku 2. CCM Tanganyika Wanajuwa hakika Wabunge wa CCM-SMZ waliotoka katika Serikali haramu, hawana Elimu wala uwezo wakufahamu sheria zilizofungwa fungwa na vifungu 30 na vitoto 200.

Wanachokitaka nikuwatumilia wazanzibari hao kuimaliza Zanzibar na bahashishi zao ni kubakia madarakani tu. Hivo hata wakiambiwa wapitishe Sheria yakuvunjwa Misikiti na shule wanazo soma Wazanzibari, wabunge hao wa CCM watazipitisha kwa kura za Ndio. Hivo tunawaomba wazanzibari wote wa CCM na CUF wawashinikize Wabunge wao na waache mara moja kutuuzia Rasilimali zetu. Na Ikiwa watalazimishwa kufanya hivo ni bora watoke Bungeni na Wawaache Watanganyika peke yao.

Wabilahi Toufiq.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 9 katika "BREAKING NEWS: Mswada wa Umiliki wa Mafuta/GAS Wapelekwa Bungeni Kinyemela."

 1. Jino kwa Jino 04/04/2017 kwa 9:35 mu ·

  Nchi ya dhulma huendeshwa kidhulma dhulma tu ni mwisho wake inakuwa ni vita .Waongo ni wengi sana lkn uwongo hauji juu kabisa na mwenye kusema uongo anajidanganya nafsi yake .Mafuta ni ya wazanzibari tone moja halitakwenda bara tumeona mifano mingi duniani kuhusu mafuta leo Walibya wanayatia mafuta yao wenyewe moto kwa ajili ya roho mbaya zao (Allah habadilishi kaumu mpaka wao wenyewe wabadilkee)Serikali ya uongo inafanya mchezo sana na hii amani iliopo lkn mifano tunaiona Iraq.Syria. Somali na Libya .Imani au neema yyote ikija ni kwa sote vile vile likija balaa au vita havitachagua ni kwa sote ,wanao chezea maisha ya watu watakuja kuja pale litakapolia (PAAA).Binadamu yyote anakikomo chake cha kusubiri akija akisema basi hapo atakuwa mchafu kaogeee.Wazanzibari Umoja ni nguvu Utengano ni Udhaifuu kwa hili tuache tafauti zetu tuwe kitu kimoja tupiganie haki zetu wakati umefika duniani hivi sasa kuna vita vya UCHUMI tu.

 2. stonetown 04/04/2017 kwa 1:29 um ·

  GUS ama Gas?

 3. Piga nikupige 04/04/2017 kwa 1:31 um ·

  Haya hodari Salama Aboud usemae humuogopi Sheni wala Seif Ali Iddi wala hushughulishwi na maneno yao maagizo yao wala kitu chochote seuze kutii maombi au maagizo ya vitaasisi vidogo vidogo vya kiserikali hasa wanao jiita wanasheria, na kwamba utasema utakavyo na utafanya utakavyo katika wizara yako na usicho kitaka utakiwacha hata kama kina maslahi kwa serikali au utakiipuuza mpaka muda unao taka mwenyewe ikiwa kitaharibika potelea mbali, na ndio maana tasisi nyingi tu serikalini hazikupendi kwa mdomo wako na vitendo vya hovyo na dharau.Wanakuomba mambo kibao uyafanye huna unacho kifanya, watu wa sheria ndio usiseme. Sheni fatilia hilo utaligundua anajifanya ana kutii tu huyo, ila anakudharau kama wewe unavyo wadharau wananchi.

  Kama wewe ni mbabe kweli usiishie kutaka kupora viwanja vya watu tu walivyo pewa na serikali na kudhulumu wanyonge wasio kuwa na hatia kwa kisingizio cha uwaziri.

  Tuna kuomba toka hadharani uwajibu watanganyika kuwa suala la mafuta na gesi haliwahusu na wala hawana mamlaka ya kuyataja seuze kuchukua mapato yake. Usiishie kudharau na kuwadhulumu watu kwa visingizio visivyo kuwa na maana. Mambo ya kudharau taasisi zenu za serikali hayatuhusu mtajuwana wenyewe ila mafuta yana tuhusu kwani si urathi wa CCM.

 4. mkitope 04/04/2017 kwa 5:57 um ·

  Sio kweli acheni kupotosha watu hakuna mswaada ulioenda kinyemela,wala hakuna mswaada Wa mafuta uliotambulishwa hivi karibuni

 5. Wamtambwe 05/04/2017 kwa 7:36 mu ·

  @Mkitope
  Hujawaona wabunge wa Upinzani waliotoka Bungeni kuupinga?
  Wewe uko huko bungeni au vipi ndio maana ukasema sio kweli?

 6. zamko 05/04/2017 kwa 9:06 mu ·

  @ stonetown

  Ni Gas, hayo ni makosa ya uandishi ambayo yamejirudia kwasababu ya kandika makala haraka haraka bila ya kuwa na Standard nzuri ya uwandishi. Ahsante kwa kuliona hilo.

  @ mkitope.
  Nafikiri hili suali likitaka kupitishwa halitonadiwa hasa kwavile ni suali la Dhulma. na kwavile Srikali zote 2 hazina nia njema kwa wananchi hasa Wazanzibari. sidhani kama siku muswada huo utakapopitishwa utakuja kunongonezwa.

  @wazalendo.

  Mimi siogopi Uchimbaji wa Mafuta Zanzibar, waache wanaotaka kuchimba wayachimbe, na wafaidike wao huku wakiwaavha wananchi wakila Vumbi kama walivo ahidi katika kampeni zao. Ninachohofia ni uharibifu wa Mazingira ambao utasababishwa na Taka taka hizo za Mafuta..

  Uchimbaji wa Mafuta sio Kitu rahisi kama Sheni na Salama Abudu anavosema. Uchimbaji wa Mafuta unataka preparation nyingi sana na kwa muda wa miaka mingi sana.

  kwa Upande wa Tanganyika, tayari wameshajitayarisha Kielimu na kiutaalamu, hivo hata hayo mafuta ya Wazanzibari yakija yakichimbwa basi atakae pata kazi ya Maana atakuwa ni Mtanganyika. ambae ana elimu.

  kwa wazanzibari wataambulia Kumwagiwa Tope za GAS na kuchafuliwa Bahari zao angalau zinazowapatia Dagaa .

  pili mmilikiji mkubwa wa Rasilimali hiyo ukiacha ajira itakuwa ni Muwekezaji, akigawana faina na Local company za Ndani yaani Mashirika madogo ya ndani.

 7. MAWENI 05/04/2017 kwa 8:16 um ·

  Serikali ya ccm pamoja na makapuni yatayo chimba mfuta na hiyo gesi Tangsnyika na Zanzibar wote wana maslahi makubwa kuhusu shughuli hiyo. Wote wana haraka ya kuila hiyo keki.
  CCM haijali maslahi ya wanachi. Hapa maslahi ya chama tu ( wakubwa)
  Kila njiya zina fanyawa na wakoloni wa Tanganyika kuwa nyima Wazanzibari uwezo wowote ule wa kujinyanyuwa kiuchumi. Ili wasiwe na ushupavu wakujitowa kwenye ukoloni.
  Viongozi hasa wapinzani wawache kuwapa tamaa wananchi isio na uhakika , na kuwapiga shindano ya ganzii wasipiganiye nchi yao kwa njiya ambayo umma unaona ndio muwafaka.
  Ikiwa wame shindwa wasiwapotezee umma mustakbali wa nchi yao.
  ZANZIBAR KWANZA YENYE MAMLAKA KAMILI !

 8. salali 05/04/2017 kwa 8:59 um ·

  Wanaogopa kukatiwa umeme hao ndio sababu (chuma) aliweka mkwara ili sasa mafuta na gesi yakianza kuchimbwa wawe ndio wasimamizi wa rasilimali za wananchi wa Zanzibar Babu Ali Shein kaufyata kama m’bwa koko.

 9. Abdul Zakinthos 06/04/2017 kwa 9:49 um ·

  watajijua waacche wafanye wanavotaka

Comments are now closed for this article.