Breaking News! Taarifa nilizozipata hivi sasa kutoka visiwani Zanzibar

Written by  //  25/01/2016  //  Habari, ZenjiLikiz  //  Maoni 9

Malisa Godlisten

Taarifa nilizozipata hivi sasa kutoka visiwani Zanzibar ni kuwa Hoteli ya kitalii ya nyota 5, Konokono Beach Resort imeungua moto.

Mmoja wa wamiliki wa Hoteli hiyo ni Bi.Fatma Karume, Mwanasheria mashuhuri na mtoto wa Rais Amani Karume. Bado haijajulikana chanzo cha moto huo, lakini kuna kila dalili ni hujuma za kisiasa kutokana na misimamo ya Fatma kuhusiana na hali ya kisiasa visiwani humo. Ikimbukwe jana TLS walifanya kongamano kupinga Shein kuendelea kubaki madarakani na Fatma aliwasilisha mada.

Hali ya Zbar imekua tete na ya kusikitisha. Ni siasa za hovyo na za kijinga kuharibu mali kwa sababu mwenzio amekupinga kisiasa. Unachoma moto hoteli kubwa kama hii bila kujali watu wangapi watakosa ajira, serikali itapoteza mapato kiasi gani? Watalii waliokuwepo hotelini watasemaje huko kwao? Je hii haiwezi kuathiri sekta ya utalii nchini? Nalaani vikali wote waliohusika na tukio hili..

Kuhusu Mtunzi

BLOGGER/DEVELOPER/JOURNALIST/BROADCASTER

View all posts by

Maoni 9 katika "Breaking News! Taarifa nilizozipata hivi sasa kutoka visiwani Zanzibar"

 1. Suleiman Alrumhy 25/01/2016 kwa 5:36 um ·

  سبحان الله
  Pole kwa kila alieguswa, ikiwa pole inastahiki.
  Na ole wake kila aliehusika ikiwa haikustahiki kufanya alichokifanya.

  Mbona picha za tukio halisi hazijawekwa?
  Au ni kukhofia kuitwa mchochezi?

  UHALIFU HAUKUBALIKI…!
  ————————–

 2. Kidekide 25/01/2016 kwa 5:45 um ·

  Hii hoteli iko beach gani au katika kijiji cha wapi?

 3. Kidekide 25/01/2016 kwa 5:54 um ·

  Oh sorry, nineiona. Iko Michamvi kusini Unguja. But hizi sasa sio siasa tena. Huu ni uhasama kama ule wa kumpokonya Maalim ushindi wake.

  Yanayofanyika sasa hapa visiwani mwetu ni mambo yakusikitisha sana. Chama cha Marehemu kimekosa manahodha mahiri. Shein na Vwai Vwai wanakipeleka mrama chombo chao.

  Sasa nchi imekuwa rasmi haina sheria wala kanuni, imekuwa jungle!

 4. abuu7 25/01/2016 kwa 5:56 um ·

  Lazima tuwangoweni hawa mbwa ccm. Mara hiii kitaeleaweka tuuu baba

 5. Mwarubaini 25/01/2016 kwa 6:19 um ·

  Hao walofanya hivyo hapana shaka ni vikosi vya SMZ kama kawaida yao, wameweza kuchoma moto studio za matangazo ya Redio watashindwa hoteli, Wametumwa na Baalozi Seif Ali Iddi na Haji Omari Shari kwa niaba ya Sheni, Kweli inauma, Fatma Karume kawazidi kwa hoja uchungu wao wanachoma hoteli yake. Na hao jeshi la Polisi hawana mpango wowote utakujakusikia tunawatafuta wahuni waliochoma hiyo hoteli na ndiyo imetoka hakamatwi mtu, wanajuana wote njama zao wanashirikiana, Hiyo haisaiidi, watu wakianza kujibu mapigo mtaipata fesh

 6. mas-albimany 25/01/2016 kwa 6:21 um ·

  Picha za tukio bado hatujazipata, zilizopo ni muonekano wa Hoteli ilivyo katika mazingira ya kawaida

 7. Bin Rajab 26/01/2016 kwa 4:16 mu ·

  WAZALENDO

  DR. MGAGANIZI KAPATA KURA 17,OOO PEMBA NZIMA
  HIZO KURA 30,000 HAZI KUPIGWA PEMBA
  NI AJABU SANA. BABU IDDI KAPANDIKIZA
  HIZI KURA

  https://www.youtube.com/watch?v=FSNzjOMSAbs&feature=player_detailpage

  SIKILIZA VIDEO YA MGAGANIZI ANASEMA TUKUBALI
  MATOKEO YA UCHAGUZI.

  SHUKRAN

 8. mpetehalisi 26/01/2016 kwa 11:27 mu ·

  Ngoja tuone kama ni vikosi vya SMZ au vinasingiziwa. Mzigo mzito mpe mnyamwezi hilo linajulikana na hasa kipindi hichi. Hoteli hii inaulinzi wa kutosha kabisa, kwahiyo kama ni vikosi vya SMZ basi itakuwa kulikuwa na mapambano na walinzi wa hoteli, na ndipo wakafanikiwa kuwazidi na hatimae wachome moto, ni akili ndogo ndio itaamini upotoshaji huu.

  Swali la kujiuliza jee hivi kuungua moto mahoteli ni jambo jipya zanzibar au kosa tu au upya unakuja eti tu kwakuwa hoteli iloungua ni ya Fatma Karume(mpiga debe wa upinzani kwa sasa)?
  Hoteli ngapi zishaungua moto, majengo na nyumba za kifahari ngapi zishaungua moto hapa znz? Tuwe wakweli, tutafute chanzo chake then ndio tutoe majumuisho na sio kukurupuka tu kishabiki.

  Kama ingeungua ya Vuai A. Vuai tungewasingizia kina nani? Does it sound okey?

  Mpetehalisi.

 9. mapango 27/01/2016 kwa 9:03 mu ·

  Nakubaliana na wewe bwana/bibi mpetehalisi, unaonaje juu ya kadhia ya kuchomwa moto kwa kituo cha redio? unadhani ni akina nani wanahusika? unaonaje kadhia ya wananchi wanaopigwa na watu wasiojulikana na wala hawawezi kujulikanwa hata tukitumia jeshi letu tukutu la polisi, unadhani nani anahusika? lazima tukiri kuwa kuna tatizo katika watawala wetu na tusipochukua hatua litatuumiza sote, kwani usisahau, No one is free, as long as others are not!

Comments are now closed for this article.