BREAKING NEWS ! Kibarua cha Balozi wa Tz Japan chaota nyasi Je ni utumbuaji au ni chuki binafsi??

Written by  //  25/01/2016  //  Habari, ZenjiLikiz  //  Maoni 16

batilda-2

MR. JOHN POMBE MAGUFULI aamuru balozi wa Tanzania nchini Japan ambae ni mke wa mwanasharia mkuu mstaafu wa Zanzibar Othman Masoud, Bi Batilda Burian kurudi zake nchini (Yaani kibarua kimeota mbawa)

………NI UTUMBUAJI MAJIPU AU NI CHUKI BINAFSI ???????

Kuhusu Mtunzi

BLOGGER/DEVELOPER/JOURNALIST/BROADCASTER

View all posts by

Maoni 16 katika "BREAKING NEWS ! Kibarua cha Balozi wa Tz Japan chaota nyasi Je ni utumbuaji au ni chuki binafsi??"

 1. mohamed 25/01/2016 kwa 9:53 um ·

  Atawekwa mtanganyika hapo, zanzibar muflis.

 2. Makengeza 26/01/2016 kwa 12:48 mu ·

  Huyu sio mzanzibari. Ni mtu wa Arusha.

 3. abuu7 26/01/2016 kwa 3:56 mu ·

  Pinda zenji sio nchi
  Lukuzi. Unataka wa zenji wajitawale wenyewe
  Ccm machotara kwao

  UTAWALA HUU LAZIMA KWA MWAKA HUU UYAYUKE. HATUWEZI KUWAACHIYA HAWA WATOTO WA KIHUNI WALOKOSA ADABU NA HESHIMA. KUFANYA MAMBO YA KIHUNI NI LAZIMA VIJANA WA CCM WOTE WAKASAFISHWE. UBONGO SABABU AKILI ZAO KIDOGO HAYAWANI. SABABU VIONGOZI WAO WAMEKOSA UTU.NA HAWAJUI NINI DUNIYA NI MPITO TU. Nm

 4. Bin Rajab 26/01/2016 kwa 4:09 mu ·

  WAZALENDO

  Msikileze Dr. Mgaganizi

  Tukubali matokeyo ya Uchaguzi

  Huyu hapa

  https://www.youtube.com/watch?v=FSNzjOMSAbs&feature=player_detailpage

 5. makunduchi 26/01/2016 kwa 6:36 mu ·

  duh haya video inaendelea sijui itamaliziaje sikamo mkurusheni naona unazidi kunenepa

 6. zamko 26/01/2016 kwa 7:25 mu ·

  @wazalendo
  Hhuyosie mke wa Alhabib wetu Othman Masoud. Mkewe Othman jina nalihifadhi, lakini mimi namjuwa kwasababu mama yake na sister wangu ni marafiki wakubwa. Ni mtoto wa Bi Salma Ngazi. Wengi tunamjuwa mwalimu bi Salma, alisomesha Hamamni na skuli nyingi Zanzibar.

  Huyu balozi ni mchaga wa Arusha

 7. AMIGO72 26/01/2016 kwa 9:25 mu ·

  JAMANI PUNGUZENI JAZBA SANA. MAANA YA UKOMAVU NI KUCHANGIA MADA KIISTAARABU BILA YA KUTUKANA MTU.

 8. khamisaj 26/01/2016 kwa 10:43 mu ·

  Iyo inaonesha wazi kuwa wapinga ccm watakutwa na matatizo mengi hapa nchini ila ALLAH atatusaidia INSHALLAH.

 9. mpetehalisi 26/01/2016 kwa 11:10 mu ·

  @Muandishi

  Hivi nikuulize swali, jee wewe umemuona huyo Batilda tu kuwa kaonewa kwa kuwa ni mke wa Othmani Masoud? Kwa taarifa yako ni mabalozi watatu wote wametakiwa kurudi nyumbani Tz haraka kuanzia jana, nao ni Balozi wa Italy, Uingereza na huyo wa Japan. Miongoni mwa sababu za kuwarudisha ni kuisha kwa mda wao au mikataba yao pamoja na mkuu hajaridhishwa na utandeji kwa baadhi yao. Jee wewe ulitaka awe balozi maisha? na jee unajuwa huyo Batilda kabla ya kuwa huko Japan alikuwa wapi? Usikurupuke tu kutoa dhana mgando na za kishabiki za siasa zisizo na tija, jaribu kwanza kuipa akili nafasi yake.

  @Zamko.

  Inabidi na wewe ufahamishwe kwamba huyo ni mke wa Othmani, huyo unaemjuwa wewe pia anaweza kuwa ni mkewe aidha wa kwanza au vyenginevyo, lakini na Batilda pia ni mke mwanasheria Othman, ni mke wake wa ndoa kama hujui na binafsi sijawahi kusikia kama walishaachana. Kama walishaachana hilo litakuwa ni jambo jengine lakini tunajuwa hao ni wanandoa.

  Mpetehalisi

 10. mpetehalisi 26/01/2016 kwa 11:16 mu ·

  Chuki binafsi na hao wenzake wengine vipi nao. Yumo wa Italy na Uingereza nao vipi wanahusiana na Othman Masoud? Kama hawahusiani basi nao mbona wameamriwa nao warudi mara moja Tz, muandishi unaandika kisiasa zaidi na nadhani wewe ndio mwenye chuki binafsi na Rais.

 11. MSHAMBA MFUPI 26/01/2016 kwa 12:45 um ·

  @ WAKITONGANI wee sasa majina yamekuwa kama shati asubuhi MPETEHALISI jioni WAKITONGANI

 12. fey 26/01/2016 kwa 2:21 um ·

  @ ZAMKO:
  Huyo unayesema mtoto wa Bi Salma angazi wameshaachana na Othman na yule bibi ameshaolewa na jamaa anaitwa Said.

 13. fey 26/01/2016 kwa 2:23 um ·

  Hebu tusubirini pengine atapangiwa nchi nyengine, maana mwaka na nusu alikuwa kenya.

 14. Alhabib 26/01/2016 kwa 2:24 um ·

  Ha babengwa Petehalisi kunrudi bila kutujuvya maana kunaondoka hapa kwavishindo na kuagansasanleo baa kunrudi bila Jodi vyerje baa kulikoni

 15. zamko 26/01/2016 kwa 11:31 um ·

  @fey
  ahsante kwa maelezo yako , ukweli mimi huwa sipendelei sana kutaja majina ya wake za watu au familia zao.. Hata hivo huyo unaesema kama alikuwa mke wa Othman halafu akamuacha akaolewa na kijana mmoja anaitwa Saidi ni kweli kabisa.

  lakini huyo mke aliemuacha sie mtoto wa bi Salma Ngazi, huyo alikuwa ni mke Ndugu na Othman.. babayake huyo Mke wa othman ni mtu wa Pandani na mama yake ni jamaa yetu wa Chambani.. Mimi huyo mke wa OTHMAN WA MWANZO NILISOMA NAE MZUMBE.. MIAKA YA 1991-94. alikuwa mke wa Othman wa Kwanza na wamekaa kiasi miaka inafika 7-10 lakini hakupata mtoto . Na OTHMAN NDIO AKAMUOWA HUYO MKE AMBAE NI MTOTO WA BI SALMA NGAZI NA ANAE MPAKA SASA NAANDIKA MAKALA HII.

  Hivo sipingi kama Othman anaweza kuwa na wake 2 na mmoja akawa huyu bibi aliekuwa balaozi..

 16. muwattin 27/01/2016 kwa 12:33 mu ·

  Wanamzalendo hebu tuwacheni kutoa details za watu kwani huenda mambo haya hayawafurahishi wehusika. Hii Huyu mke wa nani au sijui yule Mume wa nani sio ajenda zetu humu Mzalendo.Tusitoke kwenye malengo yetu yakuelimishana na kutetea HAKI YA VISIWA VYETU ADHIMU. Mtanisamehe kama nimewakwaza.

Comments are now closed for this article.