Bhaa amchana mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi

Written by  //  19/05/2017  //  Habari  //  Maoni 3

Mwakilishi wa jimbo la Mtoni, Huseein Ibrahim Makungu (Bhaa) amemtaka mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi kuunda tume maalum kwa ajili ya kumchunguza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud ili kuona anafanya kazi kwa maslahi ya Zanzibar au yake binafsi.

Bhaa ametoa kauli hiyo hayo leo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar wakati akichangia hutba ya makadirio ya mapato ya fedha ya Wizara ya nchi Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ kwa mwaka 2017-2018.

Amesema kuwa utendaji wa Mkuu wa Mkoa huyo bado una mashaka, hivyo yuko tayari kutoa maposho kwa wajumbe wote wa tume hiyo teule ili kufanya uchunguzi huo ambao amesema utasaidia kuona uhalisia wa madaraka ya kiongozi huyo.

Aidha ameongeza kuwa Mkuu huyo amekuwa akifanya kazi kwa kuingilia madaraka yasiomuhusu kwa kupiga marufuku ya kazi kwa baadhi ya wananchi hasa wanaotafuta maisha yao kwa kujiari na kuwaacha wengine wakifanya wanavyotaka.

Bhaa ametoa mfano kwa kusema kuwa Mkuu huyo amepiga marufuku kwa baadhi ya wasanii kufanya shughuli zao hizo, kwa madai kuwa wanasababisha mmong’onyoko wa maadili, huku wengine akiwapa kibali cha kufanya kazi hizo bila ya kuwa na muhali.

Akizungumzia suala la dawa za kulevya Bhaa alisema kuwa pamoja na jitihada zinazofanya na Mkuu huyo katika kupambana na wasika na dawa hizo lakini bado uwazi juu ya suala hilo bado ni kikwazo kikubwa.

Bhaa ambaye pia ni Mbunge anayewakilisha Baraza la Wawalishi amesema kuwa mara nyingi amekuwa anazitaka taarifa za dawa za kulevya ili kumuwezesha kutoa taarifa sahihi katika mkutano wa Bunge lakini Mkuu huyo anashindwa kumpatia ila humjibu zipo tu.

Zanzibardaima

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 3 katika "Bhaa amchana mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi"

 1. Abdul Zakinthos 20/05/2017 kwa 10:42 mu ·

  we Bhaa ndio muuza unga mkubwa asiekujua nani

 2. Papax 20/05/2017 kwa 1:57 um ·

  @Abdul Zakinto
  Achakumbabaisha, kijana wetu bhaa, yeye, anawajibika kuwatetea wananchi, sio, nyie cuf, mlikuweme kwenyebaraza, na kwenye suki, hamkufanya, kitu, mungu wamekulaanini, sasa mnadanganyana ,na kusubiri serekali hewa

 3. Jino kwa Jino 21/05/2017 kwa 7:54 mu ·

  @ Papax Kweli usemayo mmn nakuunga mkono ktk ukweli lkn sikuungi mkono mkono ktk matusi au simuungi mkono yyote ktka matusi tushindaneni kwa hoja nafikiri ss sote tunaumwa na nchi yetu hata akiwa ccm akifanya vizuri tutamsifu na kumpongeza na sio cuf tu peke yao cuf wangapi wanaboronga vile vile >kiongozi mzuri ni yule anaependelea maslahi ya nchi na wananchi wake na sio maslahi binafsi ni kweli cuf walikuwepo ktk suki na kwenye baraza na hakijuulikani nini wamefanya na wameacha athari gani .Ushabiki wa vyama ni sawa na timu za mpira leo mchezaji yuko huku na kesho yuko kule.Tunataka viongozi wajue wajibu wao bila kupendelea au kubagua ss sote ni raia wa ZANZIBAR .

Toa maoni

You must be logged in to post a comment.