BARUA YA WAZI KWA MUHESHIMIWA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR

Written by  //  29/11/2016  //  Habari, Makala/Tahariri  //  Maoni 3

Muheshimiwa waziri wa elimu Zanzibar natumai kuwa umzima wa afya na unaendelea na majukumu yaliyokutiknga kwanza nikupe pole kwa majukumu yako mazito lakini pia nikupe hongera kwa kuwa waziri kijana kuliko mawaziri wote wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Mheshimiwa waziri wa elimu Zanzibar napenda nikuandikie barua hii nikiwa na wingi wa furaha iliyochanganyika na huzuni nafsini mwangu kwa yanayoendelea kutokea.
Muheshimiwa waziri wa elimu kama unavyojua elimu yetu ya juu ni suala la muungano miongoni mwa mambo ya muungano ya jamuhuri ya muungano wa tanzinia ni suala la elimu ya juu.

Muheshimiwa waziri tumeona mwanzoni mwa mwezi julai mwaka 2016 tume ya vyuo vikuu ilitoa tamko la kubadilisha vigezo vya kujiunga na vyuo vikuu kwa wanafunzi wa F6 na wale tuliopitia diploma sambamba na kukataliwa kwa pasi ya Dini kwa kidato cha nne pasi ambayo ndio kimbilio na kiengeza sifa kwa wanafunzi wa Zanzibar kutokana na uhalisia kuwa kwenye masomo ya sanyasi bado hatuja jiimarisha sawa sawa hivyo kufanya wanafunzi wengi wa kizanzibari kubakia katika masomo ya sanaa kuwa kimbilio lao na pasi ya dini ikiendelea kuwabeba.

Muheshimiwa waziri Sidhani kuwa wizara ya elimu Zanzibar ilishirikishwa katika mabadiliko hayo. Lakini kama hilo halitoshi muheshimiwa waziri wa elimu tumeona pia mambo yanayoenda kutolewa matamko na waziri mwenzako wa elimu wa Tanganyika kuwa nikinyume na Sera ya Elimu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 lakini pia sio sera ya muungano tu pia ni ukiukwaji mkubwa wa sera ya elimu ya Zanzibar ya mwaka 2006.

Muheshimiwa waziri leo tukilala tukiamka tunasikia mama Ndalichako anatoa matamko ya kupiga marufuku kuvaa majoho kwa wanafunzi wa diploma na certificate hatuja kaa vizuri tunatafuta wadaiwa sugu wa mikpo hatujatulia tunasikia kuwa ni marufuku kusomea shahada kwa kigezo cha kupitia diploma hatujatulia tena tunaambiwa nimarufuku kusoma pre university yaani foundation ya kujiunga na chuo kikuu kwa waliopungukiwa na sifa.

Muheshimiwa waziri ni wakati sasa wa kusikia sauti yako juu ya hili hasa hili suala la pasi ya dini, majoho, wanafunzi wa diploma na pre university. Tunataka tusikie kauli yako suala la joho hili naweza kuliita kama kichekesho lakini suala la Wanafunzi wa diploma kujiunga na shahada ya kwanza ni kinyume na sera ya elimu Zanzibar amabayo inazungumzia kuengeza vijana wa kujiunga na vyuo vikuu siku hadi siku na kuengeza idadi ya vyuo vikuu zanziabar suala hili la kuondoa pasi ya dini kuwa pasi ya ufaulu na suala la marufuku ya kujiunga shahada kupitia diploma inalisimamisha lengo hilo muheshimiwa waziri.

Muheshimiwa waziri wakati umefika wa kutuonesha wapi yanaanzia haya mashirikiano yetu kielimu hili pia tuna mashaka nalo ifike wakati tuende na mahitaji yetu je masharikiano hayo yanaaza na F4, F6, certificate na Diploma, Shahada au Master. Mbona sera yetu ya elimu inapingana na matamshi ya kila siku ya waziri huyu mama ndalichako. Muheshimiwa waziri inatupaswa sasa tuwe na msimamo juu ya hili tunakutaka utoke hadharini utuambie wewe kama waziri mwenye jukumu la kusimamia elimu Zanzibar msimamo wako ni upi juu ya mambo haya.

Muheshimiwa waziri vijano wako tulioko vyuoni tumechoka na matamshi haya tunasoma tukiwa na fadhaa kwani kesho yake hatujui mama ndalichako atatwambia nini. Muheshimiwa waziri wewe ndio mwenye dhamana ya elimu wazanzibari 100% tunasubiri utatwambia nini kwa mustakabali wa elimu yetu kumbuka kuwa vijana wengi wapo mtaani wakitafakari hatma yao kwa kukosa vyuo na kukosa mikopo angalau tusikie kauli yako muheshimiwa waziri ili tupate faraja.

Kumbuka maneno ya hayati karume kwamba tunahitji kujitawala tujiamulie mambo yetu wenyewe huo ndio uhuru tunaoutafuta hakusita tena akasema kwamba mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe, lakini pia kumbuka malengo ya mapinduzi kuwa ni mambo matatu kupiga vija adui ujinga, maradhi na umasikini na hili analolifanya ndalichako nikuturejesha ujingani.

Wako.
Mwanafunzi wa ZANZIBAR UNIVERSITY
First Year
SEIF HAMAD SULEIMAN.
Seif0772010217@gmail.com
Simu: 0655180217.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 3 katika "BARUA YA WAZI KWA MUHESHIMIWA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR"

 1. Tengoni 29/11/2016 kwa 10:25 mu ·

  Masikini mwanafunzi bado uko kwenye Marui rui ya muungano ule wa karume, kuwa kuna mambo ya muungano na yasio ya muungano, ya kale hayapo, hivi sasa kila kitu cha muungano, na hakuna wakusema kwi. Magufuli kazuia mikutano yq vyama, na Zanzibar tumefuata mkumbo na mambo yote itakuwa hivyo hivyo, Ndalichako kesha sema, hakuna na waziri Pembe, wala mabosi wake, Balozi na Sheni,. Usomi wote wameshidwa na kina Kaujore na Khamis Hemed. Nyerere aliona mbali, alijuwa kina Kaujore hawawezi kwa kutumia documents, lakini kitakuja kizazi cha wazanzibar wasomi, ambao wataekewa documents na watakubali kuitosa nchi yao, ndio hawa viongozi wa sasa, mazuzu, makasuku wanarejea kilichosemwa kuumeni, kwa hiyo ulie tu.

 2. Z.I.7 29/11/2016 kwa 8:36 um ·

  salam kwa wote poleni ndugu kwa nchi zilipofikia kutokana na njama inayoitwa muungano hali inazidi kuwa mbaya na hasa kwa ndugu zetu wazanzibari. nachukulia kwa alie toa maelezo ni kama taarifa tu lkn huyo anaemlalamikia hawashi wala hazimi si yeye si bosi wake kwasbb maana ya mbinu zote za kufuta uchaguzi kuzusha miswada na kubadili sheria mbali mbaliharaka haraka moja ya sababu ni kuwa zanzibar ibakie kwenye mikono yetu sasa nyinyi mkisoma mtatupa tabu na nyinyi ni waislam oneni sisi wenzenu huku baba na babu zetu walipigania uhuru lkn sisi ndio manamba eidha kwa ukarim au unafiq wetu.

  amma alietia zanzibar mikononi mwetu sijui niwakusifiwa au wakulaniwa milele! maana sisi tumefaidika na mengi mbali ya rasil mali na uchumi tunavyo hodhi lakni pia hata lugha ustaarabu na kufunguka macho tumepata kutoka kwa wazanzibari hata mengine ni aibu kusimlia, LKN nini zanzibar imeambulia? kufarakana kuchukiana kuhujumiana ufukara na kumalizika kwa zanzibar, wachache kwa tamaa zao wametuletea au kutekeleza kila tunachotaka mfano juzi hapa kiongozi wa watu hao anambiwa usaini , ah atamsikiliza nani kati ya mzanzibari na master wake. kwahiyo ndugu ulielalamika usitegemee nafuu yoyote kusudio hassa ni nyinyi na watu kama nyinyi, watu wetu huku tuna wapeleka vyuoni tunavopenda hata kama debe tupu lkn wakitoka madigiree na malaghai mengine tunawapachika nayo ndio maana leo sehemu zote za serikali ni mali yao sisi hatuhusiki, hatuna sifa,

  na nikigusia juu ya ulichokisema niliweza kuwaza kwamba mwelekeo ni mbaya zaidi na niliandika kablaa humu humu kuwa huyu ndalichako juu ya alioyafanya baraza la mitihani na kulalamikiwa mara nyingi lakini kwa kufanya yale badala yakuwa demoted ndio kapewa tuzo ya uwaziri na nilisema labda wanaweza wakalegeza huku madarasa ya chini lkn sasa wanakwenda kuzuia zaidi huko elimu ya juu.

  dunia hii imeshakwenda wewe unawaza umoja upendo uzalendo wenzako hawana hayo wanawaza udini na kukumeza. ndio maana kila leo kanuni za ajabu.

  MOLA WETU tunakuomba utubariki utuondoshee majinamizi haya.

  AMIN.

 3. Abdul Zakinthos 29/11/2016 kwa 8:50 um ·

  huyo mama Ndalitako jina limemfaa hasaa

  Hivi kwani elimu ni Form six tu? sasa ina maana gani kujengwa college duniani?

  tumpe mfano mdogo tu elimu Nchi za Ulaya tukianza na UK

  Elimu inaanzia ENTRY LEVEL HADI LEVEL 7 kwa maana mtu unaweza kusoma masomo hayo ya shule hadi kufikia University lakini je wanafunzi wangapi UK wanakosa kuingia chuoni? kwa kukosaa grade zinazotakiwa hufanyaje?

  Je wanafunzi wangapi hukosa kujisomesha kwa vyuo vikuu badala yake huamua kwenda college na LEVEL six ya college HND (HIGHER NATIONAL DIPLOMA ) ni sawa na B.A AU Bs.YA CHUONI.

  ukiwa na Level six basi unaingia vyuo vingi kuchukua MA wakati ukiwa na ordinary degree ya UNI still unafanya foundation kuingia MA au labda upate msamaha flani

  Level 7 ya college PGD ni sawa na Master degree– na hili ndio maana ukaona wanafunzi wengi wankwenda college kisha wanafanya top up tu ya honour degree kwa one year ambayo ni mwaka mmoja tu.

  Mimi binafsi nilisoma Hadi Level 6 COLLEGE (integrated diploma HND) na nikafanya Top up one year University of Newcastle kupata Honour Degree na wakati naomba ilitakiwa requirement ya GCSE GRADE B YA MATH Lakini mbona nilipata exemption kutokana tayari nishasoma level 6 ? wakati wenzangu waliosoma UNI wameshindwa kuingia nami.

Comments are now closed for this article.