Bado ni uvumi – lakini, ‘lililoko mkondoni lisubiriwe ufukweni’

Written by  //  18/05/2017  //  Habari  //  Maoni 10

18528023_1558258090887682_6522972390450944939_n

Na Nurdin Msati – ukurasa wa ‘facebook’

Alhamisi, May 18, 2017

MAPYA YAFICHUKA MGOGORO NDANI YA CUF.
BAADA PLAN A KUSHINDIKANA SASA MAADUI WAANDAA MBINU MPYA.

Ukiulizwa Nchi gani iliyojaa wasomi wenye kutia hasara mataifa yao Afrika Mashariki jibu lisilo na shaka utaitaja Tanzania.

Kwa utafiti wangu nimebaini mtaala wa maisha hapa Tanzania umetawaliwa na mfumo wa undugu hivyo kama kuna kiongozi katoka kanda fulani basi watu wote kutoka eneo hilo lazima watajiona wameula kwani uzawa ndio itakuwa CV kwao kupata riziki kupitia mtawala huyo.

Tunayaona haya yakijiri ndani ya CUF.
Nimeambiwa Bodi ya LIPUMBA na wafuasi wenzake walioasisi mgogoro huu ina lazimishwa kutambuliwa kwa msaada wa anayelindwa ili yafanyike mambo yafuatayo:-

1. Bodi halali ya CUF ifutike na kukosa watu wa kulinda mali na maslahi ya Chama.

2. Board HIYO ya LIPUMBA itakua na wajibu wa kufuta kesi zote zilizofunguliwa kwani kupitia board ya zamani watuhumiwa wanaweza kutiwa hatihani.

3. Kituko kikubwa baada ya kutabuliwa board hiyo inayoandaliwa na maadui wa CUF anatakiwa LIPUMBA atangaze kuitambua Serekali ya Dr. Sheni na kutangaza CUF kujitoa katika UKAWA!

Maajabu ya Dunia LIPUMBA sio mpiga kura na wala sio Mzanzibari, hata akitangaza kumtambua Sheni ndio wataweza kuzika HAKI ya Wazanzibari?

Baada ya kutekeleza maagizo hayo yanayosukumwa na ukanda na ukabila, CUF itaingizwa kwenye mgogoro mkubwa kuliko huu wa sasa.

Wana CUF tuwe makini kwani hata wale waliokua wanaushabikia mgogoro huu kwa sasa wamekua mateka wanaamuliwa kutekeleza kila kile wenye mgogoro wao wanachokitaka.

Vijana wa BENGHAZI walioasisi vurugu Libya wamekimbia Nchi kama walivyoanza kukimbia vijana wa CUF walioshiriki KUMPELEKA LIPUMBA BUGURUNI.

Kwa sasa maadui wanaivuruga LIBYA watakavyo na ndivyo kwa sasa maadui wanavyo ivuruga CUF watakavyo, huku hawa vijana mamluki wakibaki mateka.

Ndugu zangu, CUF tukijisahau LIPUMBA ataweza kutimiza lengo lake la kukidhoofisha Chama chetu.

MAPYA YAJA MGOGORO WA CUF LIPUMBA KUTOKA BUGURUNI MPAKA ZANZIBAR KUMTAMBUA SHENI.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 10 katika "Bado ni uvumi – lakini, ‘lililoko mkondoni lisubiriwe ufukweni’"

 1. Elbattawi 19/05/2017 kwa 12:08 mu ·

  Nakumbuka: Maalim Seif, alipokuwa akizungumza wiki chache zilizopita na Cloud tv, alisema: “Kuna taarifa za shinikizo kutoka mamlaka za juu za kuitaka NIDO kusajili BODI ya wadhamini ya Lipumba, kuipiku au kuifuta iliyopo.” (sina hakika kuwa nimemnukuu sawasawa – natanguliza kuomba radhi)..

  Sasa, zinapoanza kujitokeza tetesi na uvumi kuhusu jambo hilo linalofanana na ile kauli ya Maalim Seif akiwa CLOUD, naweza kuunganisha kanda kwamba, kuna kijungu chapikwa.

  Abdulrahman Babu (Kiongozi wa Umma Party) katika uhai wake akiwa London, akihojiwa na BBC kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, 1964 kwamba yalifanyika kimya-kimya yaani kwa siri kubwa sana.

  Lakini, Babu alisema kuwa Mapinduzi ya Zanzibar, hayakuwa siri yalivumishwa kwa zaidi ya wiki moja…na yalifanyika.

  Babu alisema hata majongoo na kadondo wa pwani ya Funguni, Unguja walikuwa wanajuwa kuwa Serikali ya UHURU ya Desemba 10, 1963 ya Mohammed Shamte, itapinduliwa usiku wa tarehe 11 kuamkia tarehe 12/1/1964.

  Babu alisema hakuna uvumi usiokuwa na ukweli. Alisema Mapinduzi ya Unguja, ni mfano kuwa kila uvumi haukosi kuwa na ukweli.

  Kwa hivyo, Maalim Seif anaposema kwamba kuna taarifa za kuishinikiza nido ili kuisajili bodi ya Lipumba, si taarifa za kuzibeza na kuzipuuza, inaweza kuwa ni kijungu kipo jikoni.

  Kilichofanywa na Serikali ya UHURU ya Mohammed Shamte, kuhusu Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ni uvumi uliopuuzwa kwa uzembe na dharau na kwa makusudi.

  Naamini kwa 110% kila lisemwalo lipo na kama halipo lipo njiani laja. Juhudi zinafanywa tena kwa gharama kubwa sana za kuuwa upinzani hasa CUF na hasa kwa upande wa Zanzibar.

  Kwa hivyo viongozi wa CUF, wasidharau kama walivyodharau akina Mohammed Shamte. Madhara yake yanaonekana hadi leo, wala haijulikani yatakwisha lini.

  Hili linanikumbusha kutokana na kauli za John Magufuli (Pombe), alizowahi kuzitoa kwamba hadi uchaguzi wa 2020 Tanzania, kutakuwa hakuna tena upinzania. Akimahanisha hakutakuwa na chama cha upinzani na hasa akikusudia vyama vya UKAWA.

  Mwenyezi Mungu, atusalim salama kwa kuwa ni yeye peke yake mwenye mipango yote isiyopanguka ya mbingu na ardhi ya dunia na akhera.

  Tunamuomba asiwape nguvu wale wote wenye dhamira ovu dhidi ya matakwa na nia zetu safi..

 2. abuu7 19/05/2017 kwa 5:26 mu ·

  Kifo cha mende.hili jitu ni vizuri tulivo linyaka mapema. Maalim kenda kwa gwajima. Lipunda kenda kwa the king of dens

  hii zanzibar kwa kweli tumebanwa kwa kila kitu. Kuna mbara mmoja anasema nyinyi wazanzibar hamtopata nchi yenu ikawa huru hata siku moja.haiwezekani.watu wa milioni 2 kuchafuwa watu wa milioni42.

 3. Papax 19/05/2017 kwa 1:27 um ·

  Mtaimbo umekugandeni, kwa kujifanya wajuaji , kili ushauri mlio pewa, mlikuwa hamuuamini, maadam, maalim,kansema, tunajua cuf, ndembe ndembe kifo chamende, dua zenu, zinakurudini

 4. chatumpevu chatumpevu 19/05/2017 kwa 2:21 um ·

  @ papax
  Unayejiita Papax Unafurahi kuona kuwa mgogoro wa cuf unaingia ktk hatua ya ugumu zaidi. jiulize nyinyi washenzi wa ccm/ smt/ smz mnapata faida gani kumtumia msenge na hanithi lipumba kuidhoofisha cuf?.

  Nikwambie mtaimbo umekuganda wewe kwenye matako yako; pumbavu. kama huna cha kuandika usilete ubaradhuli wako hapa ktk mtando wa wazalendo waliostaarabika. kacheze zumna hapo kisonge.

  Nikiachana na papax niungane na mtazamo wa Elbatawi na wengine wenye mtazamo chanya wa kadhia hii. Ukisoma body language ya lipumba,ndungai na msajili wa vyama vya siasa utaona kuwa jambo hili limepelekwa RITA wakijuwa kuwa wao ndo wenye mamlaka ya juu ya kusajili bodi za wadhamini za vyama vyama vya siasa.

  Kwa mujibu wa mtazamo huu, sijui kisheria kama RITA inaweza kuisajili bodi ya baradhuli lipumba na huku RITA wakijua kuwa CUF inayo bodi halali ambayo wao RITA ndio waliosajili. Sasa msingi wa kisheria hapa ni upi kwa kusajili boadi ya lipumba/ sakaya/ mnyaa et al? na huku bodi halali ya CUF ipo na inafanya kazi zake vzr tu. Wakifanya hivyo basi itakuwa wanasheria wa RITA watakuwa wameitukana taaluma yao ya sheria kwa kukidhi matakwa ya kisiasa kwa amri ya mkuu wa kaya.

  Kwa msingi upi Revocation ya usajili wa bodi halali ya CUF itolewe na kuipa nafasi baodi ya lipumba/ sakaya/ halifa/ mnyaa/ nassor seif? Ni suala gumu hasa kwetu tanzania ambako nguvu ya kisiasa inatawala kila kitu na woga walionao watendaji ktk awamu hii ya tano, basi lolote linaweza likatokea. Inavyoelekea suala hili linaratibiwa kutoka mjengoni pale magogoni na naamini ni suala la muda tu maamuzi yote yameshafikiwa. Ni kidongo kichungu kwetu cha chloroquene kwetu sisi CUF lkn yafaa tujipange kukabiliana na sinema hii yenye igizo dhima lisilokubalika.

 5. mzeekondo 19/05/2017 kwa 5:25 um ·

  Unaweza kuchimba kisima kwa gharama na juhudi kubwa, lakini usijaaliwe kuonja hata tone la maji unayoyakamia,badala yake kisima hicho kikawa ndio kaburi lako, yaani ukatumbukia humo ili upate kuyanywa kwa ufasaha zaidi.

  Wahenga ndio wakatuonya kwa msemo wa ‘mchimba kisima huingia mwenyewe’

  Sakata hili lina uwezekano mzuri wa kuangukia upande wowote, kati ya pande hizi mbili zinazo vutana,kila upande una hiari yake kudhani kuwa utakunywa maji ya baridiii, na wala sio ya moto, lakini mimi sitostaajabu pale mate yakisha kauka, na wino ukatumika kulutea taarifa rasmi, wengi tutafahamu kuwa mkamia maji kawaida huwa hayanywi.

  Napita tu.

 6. Elbattawi 19/05/2017 kwa 8:34 um ·

  Kabla ya kuanza maoni yangu mapya, katika maoni yangu ya juu nilikose taasisi inayosajili bodi za wadhamini wa vyama vya siasa. Mimi niliandika NIDO, badala ya RITA. Sijui nilikuwa na mawazo gani au nilikuwa nikifikiri kitu gani, najiuliza?. Labda nilikuwa na hasira.

  chatumpemvu

  Kwanza nakuomba kitu sheria usahau ndani ya utawala wa MAGUFULI kwa sababu mtu huyu hana utu wala ubinadamu, anatabia za kishenzi na utawala wake anauendesha kishenzi. Magufuli neno sheria hasa halijui.

  Mimi nna wasiwasi mkubwa kuwa CUF itasalimika kwa hali ilivyo. Lipumba, kapewa jukumu maalumu na kwa gharama yoyote kuiuwa CUF, kupitia taasisi zinazohusika na vyama vya siasa na polisi.

  Maoni yangu yaliotangulia, nimesema kwamba hakuna uvumi usiyokuwa na ukweli. Mwishoni mwa mwaka 1987 (miezi miwili…mitatu hivi) uvumi ulizagaa kote Unguja na Pemba, kuwa Maalim Seif ataondoshwa Uwaziri Kiongozi.

  Na ni uvumi huo huo ambao ulimfanya Maalim Seif, kupokelewa uwanja wa ndege wa Pemba na umati mkubwa wa watu na hatimaye kutembea kwa maandamano na umati huo hadi Uwanja wa Tibirinzi, Chake Chake ambako alitoa ahadi zinazomfunga kuwa kiongozi wa CUF, hadi leo.

  Kuvumishiwa kwa Maalim Seif kuachishwa Uwaziri Kiongozi, kuligeuka na kuwa kweli mwezi wa Januari, 1988. Kosa lake ni kwamba, alikuwa muwazi katika kuitetea Zanzibar na watu wake.

  Huu ni uvumi uliyochukuwa muda mrefu kabla ya kuonekana ukweli wake na tatizo la kuchelewa kutekelezwa kwa uvumi huu, Idriss Abdul-Wakali (Maalim Idriss – Rais wa Zanzibar awamu ya 4) aliziona hisia za Wazanzibari kwa Maalim Seif.

  Maalim Idriss Abdul-Wakil, alijuwa kuwa Maalim Seif ni kipenzi cha watu na hususan alipoangalia video za mkutano wa Maalim Seif wa Tibirinzi.

  Hata hivyo, kutokana na shinikizo kutoka kwa magaidi wa Zanzibar, mwisho wa siku Maalim Idriss Abdul-Wakil, alilivunja baraza lake la mawaziri na kumweka nje Maalim Seif na wenzake wengine.

  Tukiachana na uvumi huo, baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015 na baada ya Jecha kuufuta uchaguzi huo, uvumi wa uchaguzi wa marudio ulianza, wapo waliyopinga kwamba hakuna kitu kama hicho na wapo waliyoamini.

  Sababu za watu kupinga kwamba hakuna uchaguzi wa marudio ni kutokana na vile vikao vya Ikulu vilivyofanyika kwa lengo la kutafuta suluhu la mkwamo wa utata wa kufuta uchaguzi. Baadhi ya watu waamini kwamba suluhu itapatikana.

  Kuna watu walilinganisha mazungumzo yale ya Ikulu na mwafaka wa Novemba 5, 2009 baina ya Amani Karume na Maalim Seif. Kumbe, ilikuwa ni vitu viwili tofauti. Lakini, baadhi ya watu hawakujuwa hivyo. Mwisho wa siku Jecha, alitangaza tarehe 20 Machi 2016 kuwa ndiyo siku ya uchaguzi wa marudio. Ilikuwa ni uvumi na baadaye ikawa kweli.

  Kuhusu mgogoro wa CUF, baadhi ya taarifa zinazosikika ni kama zina muundo wa UVUMI. Lakini, ukweli ni kwamba, taarifa hizi za uvumi mwisho wake zitakuwa na matokeo kama taarifa za nyuma zilizowahi kuvumishwa na ukweli ulijiri.

  Miaka yote hiyo kupitia taarifa za uvumi na hatimaye kuibuka kuwa kweli ni kwamba, watu ni wale wale waliomo ndani ya CCM na serikali zake.

  Maalim Seif, akiwa CLouds tv kuhusu shinikizo la RITA kutoka mamlaka za juu dhidi ya BODI ya wadhamini ya CUF iliyochini ya uongozi wa kweli wa akina Mtatiro na Maalim Seif, si busara kupuuza na kusema ni uvumi tu.

  Picha ya Lipumba akiwa na Magufuli hapo juu, inaeleza wazi wazi kuwa alikuwa anapewa majukumu ya kuiuwa CUF kwa lengo la kuuwa UKAWA.

  Mimi naamini katika suala hili la Lipumba, kurudi kwa nguvu katika CUF hakuna salama na siamini hasa kuwa CUF iko salama.

  Kusema kweli moyo wangu umekuwa na uzito sana na hizi taarifa za uvumi ambazo nikizingalia zinaelekea kuwa na ukweli hasa kwa rais huyu chizi kwa nguvu anazopewa Lipumba. Lakin, lililoko mkondoni litaonekana ufukweni..

 7. MAWENI 19/05/2017 kwa 10:03 um ·

  CUF MUSHA PATA KIPIGO MARA TANO AU ZAIDI.
  Siku zote inanakuwa na taarifa ya mikakati ya ccm dhidi ya CUF kabla kutokeya ; lakini , inashindwa kuyazuiya .Mengine tunanusurika nayo kutokana na uwezo wa Allah (s.w.t).Kiislamu hutakiwi kutafunwa na nyoka pango hilolo mara mbili. Kwa CUF hizo mara zisha zidi.
  La muhimu ni , cuf imejitayarisha vipi kukabili na hilo kwa hali yoyote. Watawala washajuwa wao utakomeshwa na CUF, pamoja na UKAWA .Na ukoloni wao kuteketezwa Zanzibar.
  Umma lazima upiganiye haki yao kwa hali na mali. Mikakati lazima ityarishwe . Ikiwa ishatayarishwa .
  Umma uwe macho.
  Enough is enough.

 8. Abdul Zakinthos 20/05/2017 kwa 10:47 mu ·

  hi migogoro wala haitoiyumbisha cuf BALI Itachelewesha tu wazanzibari kupata haki yetu, Si dhani kama wanaweza hata kushinda mahakamani ila mahakama itapiga kalenda kila siku hadi 2020

 9. Jino kwa Jino 20/05/2017 kwa 12:00 um ·

  Cuf hivi sasa ni kama mfa maji tu hawachi kutapa tapa hayo mambo yanayozungumwa huenda yakawa ya kweli hata kama si kweli nini wamejiandaa Cuf kukabiliana na mambo hayo hili ndio gonjwa sugu waliokuanalo CUf ya kuamini sheria ,wamejisahau kama nchi hivi sasa haiendeshwi kisheria inaendeshwa kibabe tu na kiguvu guvu anayosema magu ni kweli ifikapo 2020 hakutakuwa tena na upinzani na si hasha ikawa serikali moja tu. SMZ watabanja mavi ya kuku .Cuf na mazumbu kuku ulimwengu uko huku hawana mikakati yyote na hawawezi kulazimisha mambo yyote kwa serikali ni chama jina tu ni decoration tu ambayo inaweza kubadilika wakati wwote .mikakati yote anayo pewa lipumba itafinyika na CUf hawatafnya chochote wataufyata kama mbwa koko na tutaona cku zijazo .Mpaka sasa hakujakuwa na srious upinzani tanganyika kuna waganga njaaa tu.

 10. Mzambarauni Takao 22/05/2017 kwa 2:04 mu ·

  This maybe a wishful thinking. But unless Tanganyika’s stability is weakened and implodes internally in turmoil like say Rwanda, or Mali or Libya or Syria, forget the liberation of Zanzibar. Zanzibar will remain an annexed colony of Tanganyika since it invaded it in 1964 for a long time to come. Tundu Lissu hakukosea alivyosema Zanzibar is militarily occupied b y Tanganyika. Tanzanian politics is the politics of who holds the gun. Haya mambo ya siasa ya CUF/UKAWA, CCM ni tunadanganyana tu.

Toa maoni

You must be logged in to post a comment.