BAADA YA ZANZIBAR KUPATA UANACHAMA WA CAF

Written by  //  17/03/2017  //  Habari  //  Maoni 10

BAADA YA ZANZIBAR KUPATA UANACHAMA WA CAF

Rashid bin Mwinyi

Awali ya yote nichukue fursa hii kuwapongeza wale wate waliofanikisha Zanzibar kupatiwa uwanachama wa CAF kwa namna moja au nyengine. Lakini pili tuwashukuru wanachama wote wa CAF waliopitisha adhimio la Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF. Pili nitoe maoni yangu juu ya Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF kama ifuatavyo:-

1) Tuanze na ZFA, Kuwa mwanachama wa CAF maana yake tumeingia katika ulimwengu wa Soccar, hivyo basi watendaji wa ZFA waache kufanya kazi kimazoeya na wafanye kazi kwa misingi ya uwazibikaji na uwazi ili kufikia lengo la kuwa wanachama wa CAF.

2) Kwa serikali, Serikali yetu ya Mapinduzi Zanzibar ni lazima ichukue jitihada za makusudi kuimarisha miundombini ya mpira wa miguu ili kuhakikisha kuwa mpira wetu unaimarika na kuweza kuingia katika ushindani wa kimataifa. Pia ipige jitihada ya hali ya juu kuweza kuandaa timu ambayo itaweza kushindana katika mashindano ya kimataifa. Sasa timu ya taifa iwepo muda wote na sio sio kuundwa ma kuvunjwa kwa kuwepo mashindano fulani au kumalizika mashindano fulani.

3) Kwa vyombo vya habari, ikumbukwe kuwa vyombo vya habari vinamchango mkubwa katika kukuza kiwango cha mpira kutokana na utendaji wao kazi. Kwa mfano Mpira wa Uengereza hauwezi kuulinganisha na Mpira wa Uhispania lakini mpira wa uhispania unaonekana kuwa juu kutokana na jitihada za vyombo vya hari kuutangaza mpira wao. Hivyo basi vyombo vya habari vya Zanzibar navyo vichukue jitihada za ziada kuutangaza mpira wetu ili kuutia thamani ndani na nje ya nchi.

4) Kwa wachezaji, Sasa Zanzibar imekuwa kwenye ulimwengu wa soka, mambo ya kitoto na yasiyoleta tija katika soccer yaachwe na wachezaji na wawe na ari ya kuletea mafanikio katika timu yetu ya taifa ili tuweze kufika mbali.

Kwa kumalizia napenda kuwashauri Wazanzibar wote wafurahie kitendo cha Zanzibar kupatiwa uwanachama wa CAF na kuungana kwa pamoja kwa lengo la kuleta mafanikio ya timu yetu ya taifa.

FB

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 10 katika "BAADA YA ZANZIBAR KUPATA UANACHAMA WA CAF"

 1. Calif 17/03/2017 kwa 8:37 mu ·

  Sasa bado uwakilishi wa umoja wa mataifa UN…tuupiganieni.

 2. Fuad Suleiman 17/03/2017 kwa 1:24 um ·

  Kwa hilo mpaka CCM ife kwa zanzibar ikiwa wapo akina balozi seif na wenziwe hapapatikani kitu roho mbaya tu walizonazo

  • Calif 17/03/2017 kwa 6:28 um ·

   Ndugu Fuad si si em haifi mpk tuiue sisi kwa nia moja bila ivo watatuhuzunisha sana hawa maana wanaendesha bila kuonesha kujali

 3. rasmi 17/03/2017 kwa 9:31 um ·

  Nikubaliane na mwandishi kwamba kitendo cha Zanzibar kupata uanachama wa CAF bado wengi wanakichukulia poa, ila kwa maoni yangu mlango ambao tukiutafuta wa alau kujulikana kwamba kuna sehemu inaitwa Zanzibar na ulimwengu tayari umefunguka.
  Leo hii kazini rafiki zangu wa Algeria wawili wamenipa pongezi kwa kuwa mwanachama wa CAF, rafiki yangu huyo aliniambia kwa shauku, “nimeangalia mumepewa uanachama!” Hakika nilishangaa maana mimi mwenyewe sijaona tukio hilo na kila nikilisachi youtube limeekwa kama kidakika tu!
  Ni ada kila niulizwapo unatokea wapi? Husema Zanzibar. Suala linalofuata hua iko sehemu gani?
  Ni tegemeo langu kwamba mpira wa miguu utatutangaza, maana atayeangalia akiona hio timu yetu atapatafuta na inapotokea pia.
  Sasa ZFA ijipange na kuangalia maslahi mapana zaidi ya vijana wetu.Ni nafasi kwao pia kupasua kimataifa kama Wanaigeria, Ghana nk…

 4. Ashakh (Kiongozi) 18/03/2017 kwa 8:21 mu ·

  Kuna Baadhi ya Watanganyika limewaudhi hili. Kwa wale wenye choyo na husda juu ya Zanzibar wamekuwa wakifanya ishtizai.

  Nimeona sehemu za FB, eti watangazaji hawawezi kuyatamka majina ya Kizanzibar. Ukweli nikuwa wameugulika nyoyoni kwani kama anavyosem Rasmi tayari hapo Africa Zanzibar itatajwa.

  • Ghalib 19/03/2017 kwa 7:38 mu ·

   @Ashakh

   Majina ya Kiislamu ni rahisi kuyatamka kuliko ya kikurya na kisukuma, sasa wazanzibari ni kutumia fursa hii nzuri tulio ipata, hili sio jukumu la ZFA wala wachezaji wala vyombo vya habari, ni letu sote, hivyo sasa ni kushajiisha kuwa kila mwenye mapenzi na timu ya taifa kutoa mchango kama mwanachama, pia ZFA iwalipe vizuri wachezaji wa mpira ili waweze kujituma zaidi na kuwajengea madhingira mazuri ya kimaisha, hapo mbeleni zaidi Tutapata vipaji vikubwa zaidi

 5. Ashakh (Kiongozi) 18/03/2017 kwa 8:26 mu ·

  Rasmi
  Mie kwa mtazamo wangu kuna kazi 3 kubwa.

  1. Maslah mapana kwa vijana wetu na maendeleo ya mpira Zanzibar
  2. Elimu kwa kila Mzanzibar kujinasibu, kutunza, kuhifadhia na kuutangaza utaifa wake
  3. Kuendelea na harakati kuyatafuta mengineyo, FIFA, UN

 6. mmatemwe 18/03/2017 kwa 8:46 mu ·

  Ashakh(kiongozi) hao wanaosema kwamba majina ya Kizanzibari yatakuwa magumu kuyatamka, ungaliwauliza je wale watu wa Egypt, Morocco,na Algeria na Wako kwenye mashindano ya CAF majinana Yao ya kiislamu hutamkwa vipi?

 7. Calif 18/03/2017 kwa 10:33 mu ·

  HASAD ni gonjwa la umma! na hawa watanganyika wanalo zaman dhid ya Wazanzibar kwaio “watu mbuzi” kama hao unawaambia “KUFENI KWA CHUKI ZENU”

 8. Jino kwa Jino 19/03/2017 kwa 7:56 mu ·

  Waache siasa roho mbaya na ubinafsi viongozi hao watakaokuwa wa CAF kwa kweli ni Faraja mno Kwa Wazanzibari kwani wazanzibari wanacho kipaji cha soka toka enzi na enzi .Vijana hishima ni kitu cha bure unataka kwenda mbele lazima ukubali taabu na changa moto zitakozowakabili.Kila la kheri Zanzibar Mungu ibariki Zanzibar na watu na usiwabariki Maadau wa zanzibar .

Comments are now closed for this article.