Dk. Shein awataka wananchi na wanaCCM kuepuka kauli za upotoshwaji zinazosambazwa mitandaoni.

Written by  //  26/02/2017  //  Habari  //  Maoni 13

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 26.2.2017

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa yeye ndio Rais wa Zanzibar na kueleza kuwa hakuna Baraza la Wawakilishi linalovunjwa ndani ya mwaka mmoja na kiutaratibu Baraza hilo huvunjwa baada ya miaka mitano kwa sheria, taratibu na kanuni zake.

Hivyo Dk. Shein aliwataka wananchi na wanaCCM kuepuka kauli za upotoshwaji zinazosambazwa mitandaoni.

Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika ukumbi wa CCM, Mkoa wa Mjini iliopo Amani mara baada ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vijana kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Mpira wa Miguu kwa Timu 18 za Unguja.

Katika maelezo hayo Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anayoiongoza yeye itaendelea kuwa madarakani na kueleza kuwa mazungtumzo aliyoyafanya leo kati yake na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni mazungumzo ya kawaida baada ya kumwita kwa lengo la kubadilishana mawazo na kueleza changamoto zilizpo katika Majimbo yao.

Dk. Shein alisema kuwa yeye akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi pia, ni sehemu ya Baraza hilo na kwenda kuzungumza na Wajumbe wa Baraza hilo sio jambo jipya kwani ameshawahi kufanya hivyo kutokana na taratibu na kanuni zilizopo.

Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwasisitiza wanaCCM na wananchi kuwa hakuna Baraza linalovunjwa asubuhi hivyo kauli hizo zinazozungumzwa na zinazosambaa ni za upotoshaji na zisizo na ukweli.

Aidha, Dk. Shein aliwaeleza wanaCCM wakiwemo vijana waliohudhuria katika hafla hiyo kuwa Mihimili mitatu iliyopo ikiwemo Mahakama, Serikali na Baraza la Wawakilishi hakuna muhimili hata mmoja unaomshurutisha mwenziwe bali hufanya kazi kwa mashirikiano ya pamoja ili kufikia malengo yaliokusudiwa katika nchi.

Nae Balozi Seif Ali Idd Makamo wa Pili wa Rais alieleza kuwa uzushi unaosambazwa katika mitandao hauna maana na kueleza kuwa amepokea simu nyingi kutoka kwa wananchi kutokana na kauli hizo za mitandaoni ambazo si za msingi kuwa Dk. Shein leo anakabidhi nchi kwani maneno hayo hayakuanza leo bali ni kawaida kwa wapinzani.

Hivyo aliwataka wanaCCM na wananchi kupuuza kauli hizo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Zenzinews

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 13 katika "Dk. Shein awataka wananchi na wanaCCM kuepuka kauli za upotoshwaji zinazosambazwa mitandaoni."

 1. salali 26/02/2017 kwa 6:22 um ·

  Kama hataki kun’gatuka sababu umeahidiwa ulinzi kutoka kwa (mkononi mlevi) wapo wenye uwezo wakumtowa na huyo anae mtegemea akabaki kama beberu alokosa jike . Sio wakwaza wewe kujigamba kwamba wewe ni kiongozi halali uliowekwa kwa misimgi ya shiria na katiba, ambayo hata huijuwi na huifati.

 2. Mwinyi Mkuu 26/02/2017 kwa 6:46 um ·

  siasa za cuf zinazingua

  • sale 26/02/2017 kwa 9:16 um ·

   Kivipi?

 3. MAWENI 26/02/2017 kwa 6:54 um ·

  Ubabe na unyanyasaji ndio unao usumbuwa umma wazazibar.
  Karibu watangamuwa kuwa ufumbuzi wa dhlma wanazo zipata kila uchao wanao wenyewe.

 4. Piga nikupige 26/02/2017 kwa 7:03 um ·

  Mbona maneo yao siyo makali kama walivyo zoeleka? Mimi naona sio bure ipo namna.

 5. zamko 26/02/2017 kwa 9:19 um ·

  @ Wazalendo

  Kwanza tujiulizeni Suali 1 makubwa tuu nalo ni hili:

  Kama hakuna kitu kinachoendelea kwanini kahutubia BLW leo Jumapili Kulikoni?

  Kwanini anasema kila Siku yeye ndie Raisi, Kwani mbona 2010 alipopewa Uraisi hakuwa anasisitiza kusema hivi?

  Hivo Bado Wanaona Njama zao zitafanikiwa?

  Jambo Lipo, waache Wala wasijigambepo.

 6. Elbattawi 26/02/2017 kwa 11:18 um ·

  Mlotangulia hapo juu, nyote mmechangia maoni kwa hoja za msingi sana na hasa zamko, amegonga msumari moto juu ya kidonda.

  Mimi bado nakubalia na kauli za Maalim Seif alizozitoa hivi karibuni katika mikutano yake ya Pemba. Akizungumza Pemba, Maalim Seif alikula kiapo kuhusu mabadiliko ya utawala Zanzibar.

  Mimi sikumsikia, lakini waliyokuwepo wanasema kuwa Maalim Seif, kaapa na kurudia kiapo chake mara tatu. Kwa hivyo, naki na ahadi za kiapo cha Maalim Seif, wala sina shaka hata chembe.

  Ifahamike kwamba Dk Shein anajuwa kuwa anazungumza ‘fools’ ndiyo maana anasisitiza kuwa yeye ndiyo rais. Kwa ufupi, anajuwa kuwa urais si haki yake ndiyo anajitangaza kuwa yeye ndiye rais, kwa sababu anaowambia ni wajinga.

  Nasema ni wajinga kwa sababu tangu Dk Shein akae madarakani kwa kupitia mbinu za Machi 20, 2016 sasa ni mwaka mmoja kamili. CCM wanashindwa kumuuliza kama wewe ni rais, mbona kila kunapokucha Zanzibar, inazama katika shida na umasikini. Hata mishahara ya wafanyakazi inatoka Tanganyika.

  Maalim Seif, kawaahidi Wazanzibari kuwa haki yao karibuni itarudi na kaeleza kwa muwala. Kuwa iwapo uongozi wa Zanzibar, watakataa kumkabidhi serikali, Muungano watamkabidhi na ikiwa Muungano hawakufanya hivyo, mataifa yatafanya hivyo.

  Maalim Seif, amekula kiapo mara tatu kuhusu hilo, na anajuwa hazungumzi na ‘fools’ anazungumza na ‘Intellectual’ maana ma-CUF ni watu werevu, wanaoweza kumwambia bila kumuonea muhali kuwa, kauli na kiapo chake havikuwa sahihi. Kwa hivyo, akatafute mavi ya kuku abanje.

  Lakini, naamini kwa jinsi Dk Shein anavotoka povu kila akipata jukwaa sina shaka na kauli za Maalim Seif. Dk Shein, ngoma nzito ndiyo maana anajitekenya na kucheka mwenyewe.

  Nilikuwa sijui kuwa Dk Shein, anajuwa kuwa si rais halali wa Zanzibar. Leo katika hotuba yake ya kukabidhi vifaa vya michezo, nimehakikisha kuwa Dk Shein, anawababaisha ma-CCM na kumbe anajuwa kuwa ni mwizi, urais anaojidai kuwa yeye ni rais si wake.

  Kwa maalim Seif na kwa Dk Shein, ukweli utabainika kwa muda mfupi ujao, muhimu kwa wananchi ni kuwa na subira maana subira inavuta kheri..

 7. zenji_forever 27/02/2017 kwa 2:40 mu ·

  Inakuwaje kama ule ni mkutano wa kawaida kwanini wakaufanya in closed doors na wakawafukuza waandishi WA habari na wajumbe wote kupokonywa simu zao ?

  Nakubali hata lugha zao so xa matusi tena na muhimu mikutano ya Pemba ilikuwa kama ya hadhara lakini hakuguswa Mara hiIi.

  Hili siki limemganda Balahau Sheni halipandi halishuki na ameamua kupigana nalo akiwa chooni na akitoka nje hujikaza kisabuni akisubiri arudi chooni tena

 8. Jino kwa Jino 27/02/2017 kwa 4:45 mu ·

  CCM au Sheni Wanajaribu kubuy time pengine kaambiwa akawaaambie ukweli wwakilishi wake wajitayarishe yy kenda kuwambia pumba zake kwa sababu ni rogy na anataka kutingisa kibiriti itakuwa nini maana viongozi wa kiafrika umtoe madarakani kama anatoka chooni si rahisi ,yule wa gambia alifanya kama hivi anavofanya sheni lkn wanaume walipomwambia twajaa basi alijua njia ya kutokea .Kama kweli hili Jambo lipoo basi si Sheni wala makufuli watakao kubali isipokuwa hayo hayo mataifa Walete Jeshi halafu uone kama hakutokaa kwa domo kaya tu hatoki wala haachii ngaziii.Na itakuwaje wwikilishi wakati wote ni ccm wanyanganye simu au waandishi wa habari wasiruhusiwe kwa hivyo difinetly kuna kitu kizitoo na pengine ule warka wa state house ni kuwababaisha tu ccm wa nje ili ionekane bwana wao anajikaza lkn time will tell.

 9. sadimba 27/02/2017 kwa 5:16 mu ·

  Napenda kuungana na waliotoa maoni hata wale wenye mtizamo wa kuwaona CUF ni wenye kuzingua kwa vile sio dhambi kuwa na mtizamo tofauti. Hivi kama baba katika nyumba akinadi kila siku mimi ni baba utafikiria kuna walakini kwa wale wenye upembuzi yakinifu ila kwa wale wenye vichwa vya kaa wanaoneshwa mgomba na kuambiwa huu ni mnazi na akakubali na kushangira watasitikia ndio mzee.

  Kuna marais wa aina nyingi hata timu za mpira zina marais, kwahiyo tusipinge bila kutafakari mjukuu wa Mtopea kakusudia nini, kwa mtizamo wangu Shein ni Rais wa tume ya Jecha aliyesimikwa na mkoloni mweusi na Maalim Seif amechaguliwa na wananchi hii ndio tofauti yao kubwa. Hii kunadi mimi rais inanikumbusha kisa mlevi mmoja alilewa chakari na kubururwa na wenzake hadi nyumbani kwake alipofikishwa nyumba kwake akaanzakufoka kwa ukali fungueni mlango au nauvunja wakati yuko chini hajiwezi.

  Historia inatupa mafunzo kwa mambo yaliyopita ndio hutuwezesha kuwaza yajayo hata rais Mabutu Seseseko Kabanga wa ilyokuwa Zaire alijiita rais wa maisha na mpaka siku ya mwisho anakimbia aliwahutubia watu wake kwamba mimi ni rais kumbe anatokea mlango wa nyuma. Sasa ikiwa rais wa maisha alinadi na kuondoka vipi Kuhusu mjukuu wa Mtopea ambae kaekwa tu, maana wazee wanasema ukimtaka ng’ombe mkamatie mwanawe hata kama hana kamba atakuja tu.

  Mapoja na kujigamba kwamba mungu anamtambua hajafikia hata robo ya firauni ingawa wanafuata mfumo wake lakini firauni ulipofika muda si aliondoka. Kwahiyo, na ninavyowajua siseme kwa wanavyotumia nguvu kukandamiza wapinzani hasa wazanzibar Maalim azungumze yale kwanini wasimkamate au kumshitaki tutumie vigezo hai badala kukata tamaa, mkuu wa jumuia moja ya ccm (jeshi la polisi) alitangaza kumkamata maalim vipi kafanya au kamuonea huruma. Huyo anaejinadi rais wa zanzibar alisema ataongeza mishahara vipi katoa nyongeza kiasi gani, alisema ng’ombe wanaozurura watakamatwa lakini wamekwenda kuwanyang’anya maskini ng’ombe wao zizini. Kwahiyo, wanayosema wao ni kinyume kabisa ila moja tu alisema kweli kuigeuza zanzibar kuwa Dubai hilo amesema kweli ila hatukumfahamu tu maana alikusidia Dubai ya zamani iliyokuwa ya jangwa, tuangalie darajani, kijangwani na kwengine kunafuata ni mifano hai kuelekea kwenye azma yake. Heko rais

  nawasilisha

  • kSingga 28/02/2017 kwa 1:02 um ·

   Napenda mnavopeana moyo yaani ata mgojwa wa Ukimwi anafaa akutane na watu kama nyie, mnarefusha maisha vijana.

 10. rasmi 27/02/2017 kwa 8:39 mu ·

  Ya KANU yanaikabili CCM, kuna rafiki yangu tokea uchaguzi nilimwambia wakati wa hiki chama kuekwa kwenye boksi ya kumbukumbu umefika, na wataokiweka ni wao wenyewe, huko kwenye chama wenyewe hamkani sasa hivi pata shika nguo chanika, hawaelewani, kama wanakutegemea huko basi wamebugi stepu, hata Wema amewakimbia.

  Wamechagua raisi ambae anawasomesha nambari! Nilishauri yule staringi wa madawa ya kulevya aka mzaba makofi wazee, aachiwe aite wauzaji wa dawa za kulevya aonekana ustaringi wake , si kumbe kageuka hata jina anaitwa Daudi!

  Wengine wameanza kubusu mikono ya EL! CCM chalii wao wa kifo cha mende aka Bwana yule, mchoro wao umefeli pia!

  Sasa habari maelezo wanashughulika na mzalendo! Sisi viatu tunavyovaa ni vya Mzee Moyo, Mansuri, Jussa, Amani Karume na yoyote mwenye kuitetea Zanzibar bila ya kujali itikadi yake. uchochezi kwetu mwiko – HAPA HAKI TU HADI IPATIKANE.

  Ikiwa CCM wenyewe wanajua kwamba Shein sio raisi aliechaguliwa na Wazanzibari ni kazi bure kujaribu kutumia nguvu ya ziada kutuaminisha sisi ambao sio wafuasi wa chama. Dk Shein alinde heshima yake kwa kukubali yaishe, Wazanzibari ni waungwana na wepesi wa kusamehe kama walivyosamehewa wengi tu.

  wazanzibari hawajali chama, wanachojali ni wenye kuketea maslahi ya nchi yao…

  • kSingga 28/02/2017 kwa 1:00 um ·

   Acha kuota mchana kijana

Comments are now closed for this article.