2008 Kosovo declaration of independence,why not Zanzibar to be independence from Tanganyika colonize?

Written by  //  18/02/2016  //  Habari  //  Maoni 13

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 13 katika "2008 Kosovo declaration of independence,why not Zanzibar to be independence from Tanganyika colonize?"

 1. mzeekondo 18/02/2016 kwa 10:06 um ·

  Kwa wale wanaojua “kizungu mkuti” tunawaomba watu tafsirie maneno ya huyu muungwana wengine bado tuna ongea kisukuma nafikiri kuna mambo mazuri kaongea huyu lakini nitajuaje kama sisikii.

  wasomi wetu tafadhalini.

  Mzeekondo.

 2. Alhabib 18/02/2016 kwa 11:15 um ·

  aaaa comredi weeee mara ngapi hapa tushaona heavy language unaiporomosha hapa jamvini yakhe, tutafsirie tu ammi

 3. mzeekondo 18/02/2016 kwa 11:56 um ·

  @Alhabib na shakush

  Ha hah hahah Walahi ami yangu @alhabib huachi kweli naisikia kwa mbali hii lugha na lazima niwe mkweli maneno mazima kazungumza huyu muungwana kama nimekifahamu “kizungu mkuti” japo kidogo,nafikiri tumuombe Bwana Muungwana Sahib Shakush atutafsirie hii lugha kwani Shakush kiingereza kwake kama kiarabu yaani ana useremala nacho ana uwezo Allah kamjaalia wa kukichoonga kwa mshono wowote.

  Nasisitiza tumuombe japo kuwa inawezekana ana kazi nyingi lakini maneno yaliyo zungumzwa hapa na Rais Obama iko haja ya kumpata Mwalimu wa lugha atutafsirie ili wengi tunufaike kwani huyu mheshimiwa sio CUF wala CCM kwa hiyo kauli yake kwetu haina uwezekano wa kuegemea maslahi ya vyama vyetu adhimu,yuko “neutral” na huu ni ushauri kwa nchi za kiafrika mahsusi na watawala wetu wa jadi tunao takiwa tuudunishe kwa vigezo vya karne ya ishirini.

  Kazi muhimu kama hii hupewa mwalimu sio mwanafunzi, Bwana shakush nakuomba tuhudumie tafadhali ukijaaliwa.

  Mzeekondo.

 4. shawnjr24 19/02/2016 kwa 12:27 mu ·

  @mzeekondo
  Maneno alioyasema Obama mazima kabisa. Lakini kwa viongozi wetu hawa wa Africa haswa Mugabe, Museven na ccm hata hayawashuhulishi.

 5. SHAKUSH 19/02/2016 kwa 5:48 mu ·

  Bwana Mzeekondo
  Nashukuru kwa heshima uliyonipa japo sistahiki. Kwa vile umenitaka niiandike hotuba hiyo kwa Kiswahili sitosita ingawa ni mtihani. Kuzichanganya lugha mbili ambazo kwangu nimezisoma tu. Haiko moja ya ulimi wa mama yangu. Ni aina ya Mazoezi au Practice au Tamrin. Anasema, ” Niwe muamnifu kwenu mimi silifahamu hili. Niko katika safari yangu ya pili. Imekuwa ni fyrsa isiyo ya kawaida kwa mimi kutumika kama Raisi wa United States. Nashindwa kuikadiria heshima nilopewa au kazi bora au ya kuvutiya. Naipenda kazi yangu. Likini kutokana na katiba siwezi kugombeya tena. Siwezi kugombeya tena. nafikiriya mimi kweli ni raisi mzuri na nafikiriya nikigombeya naweza kushinda tena. Lakini siwezi Kuna mengi ningeweza kuyafanya kuifanya amerika iendlee kupiga hatua lakini sheria ni sheria. Na hakuna yoyote aliye juu ya sheria haiwi Hata Raisi mwenyewe. Niwe muaminifu kwenu natarajiya maisha yasiyokuwa na matatizo. Sitokuwa na ulinzi kama huu mkubwa kila wakati. Inamaanisha naweza kutembeya kwa mguu, naweza kukaa na familia yangu, naweza kutafuta njia nyengine za kutumikiya, nitaweza kuitembelea Afrika mara nyingi zaidi. Ukweli ni kwamba sifahamu kwa nini watu wanapenda kukaa muda mkubwa (kwenye uongozi) hasa wakishapata pesa nyingi.Wakati kiongozi akijaribu kubadilisha sheria katikati ya mchezo ili abakiye ofisini, inahatarisha utulivu na husababisha mapambano ya kutokukubaliyana kama tuonavyo Burundi. Na hii ni kawaida ya hatua ya kuporomoka. Na unaweza kumsikiya kiongozi akisema “Mimi ni mtu pekee ninaeweza kuliunganisha na kuliweka taifa hili pamoja”. Ikiwa hiyo ni kweli basi kiongozi huyo kweli atalijenga taifa? Muangaliyeni Mandella, Madiba kama George Washington walilazimisha kuwepo sheria siyo kwamba tu kwa yale waliyoyafanya ofisini lakini walikuwa tayari kuwacha ofisi na kukabidhi madaraka kwa amani. Na kama vile umoja wa Afrika unavyopinga machafuko na uadilifu wa kukabidhiana madaraka sauti za Waafrika zinaweza kuhakikisha kuwa viongozi wao wanabanwa na sheria na katiba. Hakuna yoyote atayekuwa Raisi wa maisha. Na nchi yenu ni bora ipatapo damu mpya na fikra mpya. Mimi bado ni kijana tu lakini naelewa kwamba mwengine mwenye nguvu mpya na mwamko mpya atakuwa mbora wa nchi yangu. Atakuwa pia mbora kwenu kwa baadhi ya mambo.”

  Bwana Mzeekondo. Kwa kadri nilivyojaaliwa na Allah hivi ndivyo nilivyofahamu huku ukizielewa kasoro zangu katika lugha hizi mbili.
  Allah awape kila la kheri. Ahsante kwa kunikumbuka.

 6. SHAKUSH 19/02/2016 kwa 5:51 mu ·

  Masahihiusha: Fursa isiyo ya kawaida

 7. SHAKUSH 19/02/2016 kwa 5:52 mu ·

  Naomba nisamehewe kwa makosa yangu kwani mimi bado mwanagenzi wa lugha hizi mbili.

 8. mpemba halisi 19/02/2016 kwa 6:48 mu ·

  @sakush
  japo tilimkimbia maalim eif mabanda na tukaona bora mabungo.uko juu ya msatari kosa.mkamilifu ni mungu tu.shwein na wakukurupuka kazi kwenu.

 9. Abdul Zakinthos 19/02/2016 kwa 12:58 um ·

  TAFSIRI

  ALI IDDI ,NA SHENI ACHENI UROHO WA MADARAKA ANAKWAMBIENI OBAMA

  Labda hamjafahamu kwa kuwa tittle yenyewe imeandikwa kwa lugha ya kimakosa lakini imefahamika uzuri

 10. mzeekondo 19/02/2016 kwa 1:13 um ·

  Bwana Shakush.

  Asante sana kwa kutuwekea tafsiri ya hii hotuba fupi ya Rais Obama na kuitikia wito wangu wa mradi huu kwani mara nyingi hapa jukwaaani panapotokea kuwekwa mada kwa lugha ya kiingereza hukosa wachangiaji wa kutosha sababu kubwa ni uelewa wa hii lugha wengi wetu huwa tunaisukuma tu kiasi lakini bado hatujaihifadhi na hii ni kutokana na mfumo wa elimu huku kwetu Tanzania nchi yetu ilijikita sana kwenye kiswahili huko nyuma sijui siku hizi kama hali ndio hiyo hiyo au vipi, sasa usistaajabu ukiona matusi mengi kwa lugha yetu kwani hapo tume fundishwa kwa bakora pia tustahmilie ukiona umevamiwa na lugha chafu sisi tuna kasoro nyingi lakini ni watu wa kufahamu makosa na kutubia na kuombana radhi.

  Mola atatujaalia rehma,afya,rizki zenye kheir mapenzi baina yetu na aila zetu wote wa oman na wa al zenj- bar inshaalah.

  Mzeekondo.

 11. Boriqua 19/02/2016 kwa 1:26 um ·

  Sijui huwa hawaoni aibu viongozi wababe wa ccm wakiangalia hotuba kama hii? Au huingia sikio hili na kutoka silie lile tu….

 12. Boriqua 19/02/2016 kwa 1:27 um ·

  Na sio viongozi tu.. hata hao wanaounga mkono chama cha ccm sijui hayawaingii haya?

 13. Abdul 20/02/2016 kwa 5:31 mu ·

  kosovo watu waliandamana lakini zanzibar maalim tulieni tulieni miaka inakatika khalas

Comments are now closed for this article.